Yamenikuta ndugu zangu. Je, nilichokifanya ili kumsaidia Bwana harusi nilikuwa sahihi?

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
JE, NILICHOKIFANYA NI SAHIHI?

Nilichaguliwa kuwa ktk kamati ya harusi ya jamaa yangu mmoja hivi, katika kamati hiyo mimi nilikuwa muweka hazina ,
Kikao cha kwanza tulikaa na kupanga bajeti ya sherehe nzima ya harusi hiyo, bajeti yetu ilikuwa inatakiwa tupate 12,500,000/= (milion kumi na mbili na laki tano) ili kufanikisha sherehe hiyo.

Tukapanga viwango vya michango, tukatengeneza card na kuanza kusambaza kwa ndugu, jamaa, na rafiki. Kwa bahati nzuri watu walitoa michango kwa wakati, na kuvuka malengo ya bajeti yetu hadi tukafikia 13,200,000/= (milioni kumi na tatu na laki mbili)

Baada ya kukusanya michango na kupata kiasi hicho cha pesa , mimi binafsi nilimuangalia

(1) Bwana harusi je ana kazi? Jibu hana kazi.
(2) Bwana harusi ana biashara? Jibu hana biashara.

Mimi ninavyo mjua bwana harusi maisha anayoishi ni ya kudanda danda tu ili siku zisonge mbele.

Nikajiuliza kama bwana harusi maisha yake ndiyo haya kwanini tupoteze pesa nyingi kiasi hicho kwa starehe ya siku moja na kuacha bwana harusi akitaapita katika maisha?

Ilipofika siku ya kikao cha mwisho ili tupange na kuzigawa zile pesa katika kamati ndogo ndogo ili kila kamati pesa zao mfano: chakula, vinywaji, usafiri, n.k

Mimi ndio muweka hadhina na pesa zote ninazo mimi, sikutokea katika kikao, simu nikazima na nikasafiri kabisa, pesa zote nikaziweka katika account yangu.

Tarehe ya harusi ilifika bila ya mimi kuonekana sura yangu, ikawabidi wafanye mchango mwingine mdogo wa dharura na kupitisha sherehe ndoa tu.

Niliposikia ndoa imeshapita, nilirudi mjini na nikamtafuta bwana harusi nikamuomba msamaha ila nilimueleza nia na dhumuni la mimi kutoroka na zile pesa. Nia yangu yeye (bwana harusi) apate mtaji.

Nikamkabidhi pesa zake zote 13,200,000/= nikamwambia dogo fanyia biashara uendeshe maisha yako; sherehe ni kitu cha kupita tu.

Maoni yako kwa nilicho kifanya.
 
Back
Top Bottom