Yamenikuta ndugu zangu. Je, nilichokifanya ili kumsaidia Bwana harusi nilikuwa sahihi?

Ulifanya vizuri sana na kama dogo ni kichwa hatakaa akisahau katika maisha yake yoote yaliyobaki katika dunia kwanza umempa uhakika wa ndoa yake kudumu maana chakula kitakuwepo cha kutosha na maisha yatakuwa mazuri ya kupendeza katika familia yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JE NILICHOKIFANYA NI SAHIHI ?

Nilichaguliwa kuwa ktk kamati ya harusi ya jamaa yangu mmoja hivi , ktk kamati hiyo mimi nilikuwa muweka hadhina ,
Kikao cha kwanza tulikaa na kupanga bajeti ya sherehe nzima ya harusi hiyo , bajeti yetu ilikuwa inatakiwa tupate 12,500,000/= ( milion kumi na mbili na laki tano ) ili kufanikisha sherehe hiyo.

Tukapanga viwango vya michango , tukatengeneza card na kuanza kusambaza kwa ndugu , jamaa , na rafiki . Kwa bahati nzuri watu walitoa michango kwa wakati , na kuvuka malengo ya bajeti yetu hadi tukafikia 13,200,000/= ( milion kumi na tatu na laki mbili)

Baada ya kukusanya michango na kupata kiasi hicho cha pesa , mimi binafsi nilimuangalia
(1) bwana harusi je ana kazi ? Jibu hana kazi ,
(2) bwana harusi ana biashara ? Jibu hana biashara.

Mimi ninavyo mjua bwana harusi maisha anayo ishi ni ya kudanda danda tu ili siku zisonge mbele.

Nikajiuliza kama bwana harusi maisha yake ndio haya kwanini tupoteze pesa nyingi kiasi hicho kwa starehe ya siku moja na kuacha bwana harusi akitaapita ktk maisha ?

Ilipofika siku ya kikao cha mwisho ili tupange na kuzigawa zile pesa ktk kamati ndogo ndogo ili kila kamati pesa zao mfano : chakula , vinywaji , usafiri , n.k

Mimi ndio muweka hadhina na pesa zote ninazo mimi , sikutokea ktk kikao , simu nikazima na nikasafiri kabisa , pesa zote nikaziweka ktk account yangu .

Tarehe ya harusi ilifika bila ya mimi kuonekana sura yangu , ikawabidi wafanye mchango mwingine mdogo wa dharura na kupitisha sherehe ndoa tu.

Niliposikia ndoa imeshapita , nilirudi mjini na nikamtafuta bwana harusi nikamuomba msamaha ila nilimueleza nia na dhumuni la mimi kutoroka na zile pesa . Nia yangu yeye ( bwana harusi ) apate mtaji.

Nikamkabidhi pesa zake zote 13,200,000/= nikamwambia dogo fanyia biashara uendeshe maisha yako sherehe ni kitu cha kupita tu.

Maoni yako kwa nilicho kifanya

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni chai bila vitafunwa, pia ni hazina sio hadhina
 
Yeye alichukuliaje hilo Jambo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na kuwa hii ni hadith swali ni je ungekuta amekufa kwa sababu ya presha ungesaidia nini?
 
Katika hiyo 13.5M,kuna baharia mmoja alitoa mchango wa 50k,sidhani kama angewaelewa endapo sherehe isingefanyika.

Usijejaribu kusepa na hela zinazotokana na michango, utajuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom