Yamemkuta, anaomba ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yamemkuta, anaomba ushauri

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MAGISAC, Jan 27, 2012.

 1. M

  MAGISAC Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wana JF. Nina rafiki yangu na ni jirani yangu wa karibu ambaye katika story mara nyingi alipenda kumsifia mumewe kuwa ni mwaminifu kupita kiasi hawezi kumcheat. Kumbe inaonekana jamaa alikuwa na mazoea ya kutoka nje lakini alikuwa anazingatia vigezo na masharti ya kuwa na nyumba ndogo. Jana ikatokea km bahati mbaya jirani akawa anachezea simu ya mumewe mara akaingia katika inbox na kukutana na sms za mapenzi toka kwa hawala kuwa anamshukuru kwa penzi tamu alilompa kwenda kwenye sent item akakumbana na jibu la mumewe kuwa hiyo ilikuwa cha mtoto ngoja wakutane tena. Bibie akatoka amepanic na kuja kwangu huku analia anaomba ushauri afanye nini. Nimeamua kuwashirikisha ili walau nipate mawazo yenu nijue nimshauri nini kwa sababu hajajiunga JF.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kapata alichokua anakitafuta.. Mwambie ameze Kama tamu Kama chungu ateme...na akome kupekura simu ya mumewe..
   
 3. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  kwani yeye alidhani kufunga ndoa ndio kupewa hati miliki ya mtu mwingine?

  a grow up aache kulia lia.
   
 4. M

  MAGISAC Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini asiwe huru kusoma si ni ya mumewe?
   
 5. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  wewe una nyumba ndogo ngapi?
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  utamsaidia nini hapo.

  Mwambie ajifunze kufanya maamuzi magumu inapohitajika.
   
 7. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mshauri kwanza ajiunge JF, then ndio nitoe ushauri kwa mhusika.....!
   
 8. M

  MAGISAC Member

  #8
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushauri wako kwa sasa ni muhimu zaidi lakini nitamsahuri pia ajiunge
   
 9. M

  MAGISAC Member

  #9
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa ushauri wako umefika huo.
   
 10. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Kua uyaone, mwambie hilo tu..Halafu huyo jamaa hakuzaliwa kwa ajili yake tu!
   
 11. M

  MAGISAC Member

  #11
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanaume kama hawa ukishika tu simu yake waweza ambulia kipigo
   
 12. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mwambie hayo niyakawaida sana,atazoea tu
   
 13. M

  MAGISAC Member

  #13
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hebu jaribu kuvaa uhusika kidogo. So kwako mume kucheat ni jambo la kawaida?
   
 14. M

  MAGISAC Member

  #14
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru dada, kwa hiyo aendelee kuvumilia asifanye lolote kwa kuwa ni kawaida?
   
 15. pinkmousse

  pinkmousse JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndoa ni ya muda gani?,kupanic ni kawaida atatulia, kwa sasa usitoe ushauri wowote kwa sababu there's nothing you can do about it hayo mambo ni yao wawili na mumewe, baada ya muda kidogo yeye mwenyewe atapata jibu aendeshe vipi ndoa yake. Hebu fikiria kama mko kwenye ndoa miaka ishirini,anything is bound to happen! Mara nyingi tunajiwekea nadhiri ngumu wakati tunaolewa kwamba mume hatanicheat na kila wakati tunaishi kwa kuhakikisha hilo halitokei lakini bahati mbaya sana sio reality ya maisha haya!
   
 16. M

  MAGISAC Member

  #16
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yeye mwenyewe anajuta kusoma na hakuwa na mazoea hayo ndo maana mumewe hakuwa makini kuzifuta kama wengi wafanyavyo.
   
 17. segere

  segere JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 518
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  ..atulie tu aongee vyema na mmewe huku akitafuta wapi palipata nyufa na apazibe,hawala ni kiumbe asiye na haki ingawa ni mwerevu na makini ktk usafi wa mwili,akili na mtundu wa mambo flani..kitu ambacho hata walio kwenye ndoa wanaweza kuwa navyo..nachoogopa ninyi wamama wa leo umekosa kabisa nafasi za ku-update ufahamu wenu juu ya maisha na mahusiano,kiasi mwafanya studio zenu zikose mvuto,acheni usanturi/kunenepa bila mpangilio,ongezeni kiu ya kuyaboresha maisha yenu kila ki2 kitakuwa pouwa..
  Angalizo: YALIYOMKUTA NI YA KAWAIDA SANA HUKU NJE TUKO SIYE AMBAO TUNAUMIZA ZAIDI KO ASIJARIBU KUJA ASIJE OMBA SUB NA PIPO ZA AHERA BURE..
   
 18. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  mwambie atafute kidume cha mbegu akigawie na yeye ili ngoma iwe draw
   
 19. M

  MAGISAC Member

  #19
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nshukuru kwa busara na maoni yako. Ndoa ina miaka minne.
   
 20. M

  MAGISAC Member

  #20
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ni jino kwa jino au siyo?
   
Loading...