Yameishia wapi mayai ya kware na ufugaji wa kware?

Yalipata kiki kama kikombe cha Babu wa loliondo
 
Tatizo lililopo ni kuwa mamruki wa vitu. Huwa tukisikia kama dili fulani linalipa basi wote tunataka kufanya hilo dili bila kujua kwamba wengine inabidi tubaki wahitaji wa hizo bidhaa. Inafika sehem kila mtu ana mayai ya kwale, unamuuzia nani sasa??

= mamluki
 
kware anapigwa menu kali ya kuku broila. Halafu eti tiba! kweli kuna watu hamnazo!
 
Mkuu jiulize hii habari ilianzia wapi?
Ilianzia namaingo business agency.
Sasa waliamia kwenye sungura na kilimo cha madodoki....
Namaingo Mungu anawaona yani watanzania wanadanganywa daily
Projects za hawa jamaa ni pasua kichwa.
 
Post bora kabisa

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
 
1.KIKOMBE CHA BABU,
2.DECI,
3.MAYAI YA KWARE,
4.BAADHI YA TIBA ZA ASILI NA MIMEA,
5.BAADHI YA IMANI ZILIZO NA UTATA,
6.RUPIA ZA MJERUMANI
Pamoja na Abracadabra zingine zote kwa kweli ni vitu vinavyozuka kwa mbwembwe nyingi na kwa bahati mbaya wale wanaovianzisha hutumia technics za hali ya juu kwa kugusa yale maeneo sensitive yanawagusa watu wengi kama vile masuala ya kiafya, kiuchumi na kiimani. Usipokuwa makini utaingia mkenge, haijalishi elimu yako, cheo wala nafasi yako uliyo nayo katika jamii.

Huwa vinachukua muda fulani tu na mara nyingi siyo mrefu sana and then watu wakishagutuka basi vinafifia na kuwa historia. Bora sungura nimeona pamoja na kwamba kuna kaharufuharufu ka mizengwe mithili ya hiyo hapo juu kwa baadhi ya wadau lakini kwa kiasi kikubwa miradi ya ufugaji wa sungura ina uhalisia, hata wapo watu wengi wanaofuga na faida huiona ila siyo kwa kiwango kinachotiwa chumvi na baadhi ya wadau.

Tujifunze siyo kila kitu ni cha kukurupukia, akili ya mwenzio changanya kwanza na yakwako.
 
Watanzania wanapenda sana kuishi kwa mihemko

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
umenikumbusha lina kwenye interview ya powerjams ya sam enzi izo
 


Tunaendeshwa na masalia ya tamaduni zetu.... Kila tunachofanya kimekaa kiganga ganga....!! Can you imagine hadi maprofeseri, phd holders, ministers, prezdars walikwenda kwa babu..
 
Wameamia kwenye VUMBI LA MKONGO.

"PAMBANA NA HALI YAKO"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…