Yaliyotokea, yasiyosemwa, kutoka Dar hadi Vamizi Island

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Miaka saba iliyopita nilisafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kwenda katika Kisiwa cha Vamizi ambacho ni himaya ya nchi ya Musumbiji, Kisiwa hiki kipo katikati ya bahari ya Hindi kikipakana na Comoro kwa upande mmoja na Msumbiji kwa upande wa pili, Kisiwa hiki kina maajabu mengi, lakini ajabu kuu ni kuwa wakazi wote wa kisiwa hiki ni wazungu/watu weupe kutoka Uingereza na kwingineko. Daraja la chini kabisa la watu pale ni jamaa flani hivi wanne raia wa Filipino ambao ni wahandisi wa mitambo na ujenzi. Na nilipofika mimi nikawa binadamu pekee mweusi kisiwani hapo kwa siku 15 nilizokaa pale.

Safari yangu ilikuwa ni ya kihandisi zaidi pamoja na mambo mengine, nilipata kazi wa kujenga kinu cha kufua umeme na kuusambaza katika kisiwa hicho chenye nyumba kama miamoja hamsini hivi, Nakumbuka vema, makubaliano na vikao vya mradi huu yalifanyikia katika kisiwa cha Jersey Uingereza na Mbutu Kigamboni.

Tukirejea katika kisiwa hiki, Jambo la pili kisiwa hiki watu hawamiliki hela, yaani kila kilichopo ndani ya kisiwa hiki hautakipata kwa hela mkononi, biashara ya hapo kisiwa inafanyikia katika Jersey Uingereza au Dar es Salaam. Hapo unakwenda kuishi na kula na kunywa utakavyo bila kuwa na pesa mkononi. Kisiwa hiki chote ni hoteli, kinaukubwa kama vile uunganishe posta yote, mnazimoja yote na kariakoo yote hadi mchikichini.

Kisiwa kina uwanja wa ndege ndogo, kina bandari ndogo, kina hospitali na kina kituo cha polisi na vyote vinaongozwa na wazungu. Nilipofika katika kisiwa hiki binadamu mweusi rijali nilikuwa pekee yangu tu. Nilikabidhiwa nyumba yenye kila kitu na mhudumu mmoja wa kizungu.

Kisiwa kina wanyama kama nyani, tumbili, swala, simba na tembo, nk. Sehemu kubwa ya wageni/wateja wanaofika hapo ni watu mashuhuri zaidi duniani, mfano siku ya kwenda katika ndege nilikuwa pamoja na Sylvester Stallone, Matthew Marsden, Julie Benz na wengine siwakumbuki vizuri lakini walikuwa watano.

Nilikutana na msimamizi wa mradi ule niliokwenda kuufanya pale, aliitwa Teodor huyu ni Mfilipino ndio alikuwa mwenyeji wangu, tulizungumza mengi, nikamchokoza juu ya mambo kadhaa hasa uendeshaji wa kisiwa hicho na namna nchi ya Msumbiji inavyonufaika, jamaa alikuwa mzoefu pale alikuwa ameaminiwa sana na Waingereza.

Aliniambia Waingereza wako kama kampuni ya uwekezaji katika mahoteli duniani wanamiliki visiwa vingi kama vile Ibiza, Bahamas, nk na kote nikuwa nchi yenye kisiwa inachukua 30% ya faida, (Gawio),. Na vilevile kodi ya serikali inafuata utaratibu na sheria za nchi husika. Mfano ingekuwa Tanzania, nikuwa 18% ya kodi ya ongezeko la thamani ingetozwa na ukijumlisha mrahaba wa 30%, hivyo kungekuwa na faida ya gawio la jumla ya 48% kwa nchi.

Baada ya siku 15 nilimaliza kilichonipeleka, sikutaka kurudi kwa ndege wala sikutaka wazungu wale wanisindikize wakati wakuondoka, nilichomoka saa nane usiku nikavuka mageti manne yote yenye ulinzi mkali nikafika sehemu kuna wavuvi weusi huwa wanapumzika katika safari yao ya uvuvi, usiku ule nilikuta mtumbwi wa upepo mmoja uko pale na kuna wavuvi wawatatu, pembeni yao palikuwa na mzee mmoja wa makamo alivaa nadhifu kama shekhe hivi, nikawauliza gharama ya kukodi mtumbi unipeleke hadi pani ya mkoa wa Pemba, wakasema Mitikashi 600, sikuwa na hela hata mia, lakini nilikuwa na laptop na simu aina ya black berry curve, niliwambia haya twendeni hela ninayo, nilijibu kiujasili tu.

Wakati tunataka kuondoka yule mzee aliyevalia kanzu safi aliongea kireno mie sikumuelewa wale wavuvi wakaniambia kwa kireno hivyohivyo ila kwa vitendo wakionyesha kwa mikono kwamba mzee yule anaomba lifti.

Nikasema twendeni wote hata kama kuna wengine huko waambieni waje, nami nikizungumza kwa ishara za mikono tu maana lugha yao nilikuwa siipati vizuri, tuliingia ndani ya mtumbwi ule manahodha wawili, abilia wawili mimi na yule mzee, wakati tunaingia yule mzee alikuwa na mizigo, alikuwa na kiroba cha unga, mchele, na ndoo ya mafuta ya kula, vyote aliingia navyo.

Tulianza safari saa tisa kasoro hivi, katikati ya mwendo manahodha wakawa wanavua pweza kwa ndoano zao hivi, nilishuhudia pweza wengi na wakubwa sana wakivuliwa huku chombo kinakata maawimbi balaa, tulipofika katikati ya bahari kabisa yule mzee akasema yeye ameshafika, mtumbwi ukasimamishwa kidogo kwa kutia nanga, akaanza kupakua viroba vya mchele na unga akavirusha baharini, na ndoo ya mafuta akairusha pia, nikashangaa akisema kwa kireno tembeeni salama nashuruni kwa msaada, akatumbukia na yeye (nilielewa aina ya ishara alizotoa nikajua ni shukrani).

Tuliendelea na safari tulifika pwani mida ya saa tano mchana hivi, na baada ya kukiegesha chombo pembeni ya mti hivi, nilimfuata yule nahodha nikamuuliza, kwamba kile nilichokioona usiku ni ndoto au ni kweli? Nilimwambia yule nahodha kuwa sina pesa ya kumlipa, lakini namwachia simu yangu ya blackberry, alifurahi sana akasema hii ni bahati kwake.

Jamaa akajibu wale ndio wenye bahari, ungekataa lifti jana tungepata majanga njiani. Nilistaajabu lakini niliimarika kiroho sana sana kwakuwa kwa imani yangu ya mizimu huo ni utukufu na talanta ya mwafrika. Nilimaliza safari ya majini nikaingia nchi kavu, nikauliza wenyeji sehemu ya majimbo ya madini ni wapi? Wakanielekeza kuwa kunaitwa Mtipwesh, nikatafuta mteja wa laptop nikauza palepale nakushika mkwanja wa Msumbiji, nikapanda gari land cruiser mkonge zinatokea Maputo kwenda bandari ya Beira kwenda mji wa Mocimboa De Praia na mwisho zinafika boda ya Tanzania na Msumbiji inayoitwa De Namoto, nilifurahi kwakuwa gari ile ilikuwa ikiendeshwa na jamaa Mtanzani mchaga wa Moshi nakumbuka jina lake aliitwa Julius, tulipiga stori sana safari ilikuwa ndefu sana, Kuna sehemu tulifika, Nilishuka na kupanda gari zingine zinazokwenda huko machimbo,

Nilikuta huko watu wengi ni Watanzania, na ni matajiri wakubwa sana, Wachaga huko kumekuwa kama nyumbani, lakini kubwa zaidi lilikuwa ni suala la usalama wao na mali zao, walisema kila kukicha polisi wanakuja kuwapora mali zao na kuchanachana vibali vyao vyakuishi nchini humo, ilikuwa ni moja ya huzuni inayowakabili pale, na kukaa kwangu siku tatu pale niliyashuhudia matendo hayo kwa macho yangu, wanawake walibakwa na kunyanyaswa wazi, mamlaka za msumbiji zilikuwa ndio maharamia wakubwa wa usalama wa watanzania. Sikuona hata haja ya kutafuta maisha hapo, bora nirudi bongo tu ambako bamia zangu zilikuwa zinanisubiri...

Nilipanda gari kuelekea boda ya mpaka wa Tanzania, hapo kuna kituo cha uhamiaji cha msumbiji kinaitwa De Namoto, hapo tulifika kama saa nne usiku tukazuiwa kuvuka mto Ruvuma usiku ule tukalala pale, kisha kesho yake asubuhi tukakaguliwa na kugongewa pasipoti zetu na tukaruhusiwa kuvuka kuja boda ya Tanzania inayoitwa Kilambo, baada ya kutoka hapo sasa ilikuwa nimefika nyumbani kwenye ardhi ya mafuta na gesi leo ikiitwa koro-show......

Acha kupenda vya bure, changamsha akili kwakusoma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kwa Ofa ya 50,000 tu badala ya bei halisi ya 80,000/=.

Nunua kwa M-Pesa au Tigo-Pesa

0715865544
0755865544

Na Yericko Nyerere
IMG_20190825_103329_995.jpg
 
wewe jamaa chai sana, hata hicho kitabu chako cha ujasusi inaweza kuwa chai tupu, alafu 80,000/= ni bei kubwa sana.
 
Na Yericko NyerereView attachment 1189539
Mkuu bado unatumia laini ya Vodacom?
 
Back
Top Bottom