MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 714
- 1,137
Taarifa za kutengua uteuzi wa DC na DED wa Malinyi zinapaswa kuwa starting point ya kuanza kujadili na kushughulikia migongano ya kiutawala inayoendelea katika sekta ya utumishi wa umma hasa kwenye position hizo mbili.
Wote wakiwa ni wateule wa Rais lakini job description zao kama zinashindwa kuweka mipaka ya utendaji wao na kama upo basi unatenganishwa na mstari mwembamba sana ambao mara nyingine mtu anashindwa kuelewa uko wapi.
Hayo ya Malinyi sio mapya kwa DC na DED wake kutunishiana misuli, kwani nakumbuka waziri mkuu Kassim Majaliwa aliwahi kufanya ziara moja mkoa wa Kagera wilaya ya Bihalamuro akakutana na scandal kama hiyo hiyo sema tu, tofauti ya Malinyi na Bihalamuro ni kwamba Malinyi ni wanaume tu wakati Bihalamuro walikuwa akina mama watupu.
Kuna mbishano kati ya nafasi hizo mbili huko mawilayani kwani DC anaona kama ndio kiongozi mkubwa na kauli yake inatakiwa kuwa ya mwisho, huku DED nae akiona ana nguvu sana kwani miradi yote ya halmashauri yeye ni last approval na anamiliki watumishi wa idara zote pale wilayani na mara nyingine DC anaweza omba mafuta ya kuendeshea gari lake kutoka kwa DED na kusema kweli DED anamiliki raslimali watu na fedha .
Ni kutokana na mstari huo mwembamba sana wa majukumu yao, utawakuta wakizozana kwa mambo ambayo wangekaa na kuyamaliza kwenye vikao vyao.
Hapo cheo Cha DC kinabakia kuwa tu cha ukuu wa kamati ya Ulinzi na Isalama huku mambo mengine ya miradi yakitekelezwa na Mkurugenzi kwa kushirikiana na watalaam wake huku DC akiangalia kwa macho tu.
Japo sheria inampa mamlaka DC kuingilia kati kwa jambo lolote ndani ya wilaya yake lakini bado kuna loopholes nyingi sana za yeye kufanya mambo mengi ndani ya halmashauri.
Ni wakati sasa wa kuvunja cheo kimoja kati ya hivyo viwili ili halmashauri na wilaya zipate ku settle.