Kutumbuliwa DC na DED wa Mtwara Vijijini ni sawa na mauaji ya Demokrasia na Utawala Bora

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Kutumbuliwa DC na DED wa Mtwara Vijijini ni sawa na mauaji ya Demokrasia na Utawala Bora (murder of democracy and good governance)

1. Mama alijuaje huku juu? Fitna au kitu gani?

2. DC japokuwa hayupo kikatiba lakini jukumu lake la msingi ni usalama wa Wilaya. Hakuna ushahidi wa usalama kuzorota kwenye eneo lake.

3. Watu kurudisha kadi za CCM ni ishara ya ukomavu wa demokrasia ambayo ingempandisha DC kuwa RC.

4. DC siyo wa CCM tu, ni DC wa wote wenye vyama na wasio na vyama.

5. Vipi CHADEMA na CUF wakiamua kurejesha kadi kwenye vyama vyao na kujiunga na CCM pia DC na DED watatumbuliwa kwamba ni kwanini wapinzani wanajiunga CCM?

6. Rais alitakiwa amtumbue M'kiti wa CCM Wilaya ndiye hajafanya kazi yake vizuri siyo DC na DED.

7. Nadhani DC na DED waende kujisafisha Kortini.
 
Back
Top Bottom