Yaliyotaka kutokea leo uwanja wa Taifa,ndio matokeo ya "siasa" za Vita ya madawa ya kulevya

Kumbe mleta uzi huwa anajitoa ufahamu na akili safi kabisa anazo?Thread hii ipo smart area kwa mwendo mkakamavu.
Lini nilijitoa ufahamu!!Mi huwa napongeza na kukosoa pale napoona kwa binafsi yangu panastahiki kati ya hayo mawili
 
kumbe zile cartel zipo hadi bongo duuh ngoja tuone mwisho wa huu mziki sasa
Kama uliskia mahojiano ya Kamishna wa Tume ya Kuzuia Madawa Ya kulevya,alisema zile "cartel" unazozisikia Brazil na Mexico,basi hata bongo zimejaa
 
American Gangster haisogelei mziki wa Corleone wa Sicily

Organized crimes za hawa jamaa wa Sicily ni za kutisha na kutakatisha pesa haramu kupitia kanisa nk
Sasa si unaona ndio wale wale wamempokea South Africa?
 
Msaada tafadhali- kirefu cha GSM
GSM NI KIFUPI CHA MAJINA YA HUYO MYEMENI MSHENZI ANAYETAKIWA KUFUKUZWA NCHINI MARA MOJA, NI GHALIB SAID MOHAMED, ZAMANI ALIKUA ANA GARI LINA HIZO LETTERS, NDIO KATUMIA HIVYO KU REPLACE PROPERTIES WALIZOIBA WAKATI WAKIWA HOME SHOPPING CENTER, HAWA MWISHO WAO UMEFIKA, WALE WAAJIRIWA WAO WOTE WALIOTAPELIWA NSSF ZAO TAFADHALI PELEKENI MALALAMIKO YENU LABOR HARAK IWEZEKANAVYO HAWA WATU WATATOROKA ANY TIME MANAKE MAKONDA AKICHAMBULIWA HUMO NI BALAA, HALMASHAURI ZOTE ZA DAR KUPITIA MAKONDA ZINA MABOMU KIBAO YA UCHUMAJI HELA WA HAWA WAYEMENI NA MAKONDA, HILI TUMELIKATAA HATA WAKILINYAMAZIA NCHI NI YETU, UCHUMI NI WETU, KODI NI ZETU, GO GO GO TANZANIA
 
GSM NI KIFUPI CHA MAJINA YA HUYO MYEMENI MSHENZI ANAYETAKIWA KUFUKUZWA NCHINI MARA MOJA, NI GHALIB SAID MOHAMED, ZAMANI ALIKUA ANA GARI LINA HIZO LETTERS, NDIO KATUMIA HIVYO KU REPLACE PROPERTIES WALIZOIBA WAKATI WAKIWA HOME SHOPPING CENTER, HAWA MWISHO WAO UMEFIKA, WALE WAAJIRIWA WAO WOTE WALIOTAPELIWA NSSF ZAO TAFADHALI PELEKENI MALALAMIKO YENU LABOR HARAK IWEZEKANAVYO HAWA WATU WATATOROKA ANY TIME MANAKE MAKONDA AKICHAMBULIWA HUMO NI BALAA, HALMASHAURI ZOTE ZA DAR KUPITIA MAKONDA ZINA MABOMU KIBAO YA UCHUMAJI HELA WA HAWA WAYEMENI NA MAKONDA, HILI TUMELIKATAA HATA WAKILINYAMAZIA NCHI NI YETU, UCHUMI NI WETU, KODI NI ZETU, GO GO GO TANZANIA
Naona kashfa aliyoiibua yule dada Insta ya kuhongwa magari mkuu wa mkoa!!Inakamilisha kile ulichoandika na nilichoandika mimi ktk uzi huu
 
Niliwahi kuandika humu kuwa Mako vema akakaa kando ili aepuke makaburi yaliyobaki kufukuliwa na pia kuleta heshima kwa serikali ya bosi wake,lakini waapi!
 
Ulichokieleza ni kweli kabisa yaani hawa ma drug lords wanatumia ufinyo wa mawazo ya watanzania wengi ambao akili za upambanuzi hawana.
 
Tunaweza kuwa tumeingizwa mkenge,kujua mbinu za "black market" inahitaji kuwa makini sana!

Berluscon PM wa Italia miaka hiyo,akiwa kama mshirika wa Mafioso,wale Mafia wa Kisiwa cha Sicilia,akina Salvatore Capello na Luigi Giaccomo,aliona hatari ya kuja kufungwa siku moja,kama atakuja kutokea PM "katili" Italia aliyetaka kuidondosha "Cosa Nostra"ya Parelmo,Catania na Aggrigento miji ya kisiwa cha Sicilia kusini mwa Italia.Walikojaa wauzaji wa madawa ya kulevya na uharamia wote wa dunia.

Alichokifanya Berluscon ni kuhakikisha anatakatisha pesa yake ktk miradi inayogusa maisha ya watu,furaha za watu na starehe za kila siku za watu wa masikini na matajili,ili kila anapotaka kuguswa basi nchi nzima ilipuke kwa kauli moja "ANAONEWAAAA"

Aliamua kuanzisha TV maarufu sana inaitwa "TeleMilano",akaajiri watu wengi sana,akaanzisha Gazeti na kuajili watu wengi sana,akanzisha mahoteli na Casino na mwisho akainunua timu ya mpira kubwaaa pale Milani ya AC Milan,na mwanae wa kike ndio akawa kiongozi wa timu

Mpira ni utamaduni wa Wataliano,ukitaka wakuuwe,basi haribu mpira.Hapa ndipo mioyo ya wanazi wa mpira wa Milan ikawa kwa Silvio,akajitahidi kusajili wachezaji wa kiwango cha dunia,akachukua vikombe vya ndani na nje ya Italia.Akaweka furaha ya watu wa mpira katika kilele cha mafanikio.

Ikawa ukimgusa Berluscon basi umemgusa shabiki wa Milan,ukimgusa tena basi umemgusa mwandishi wa habari wa gazeti analomiliki,ukimgusa tena basi umegusa mtangazaji wa Tv ya TeleMilano,ukienda huko na kumgusa,basi umegusa wafanyakazi wake wa hotel na Cassino au washirika wake wa kisiasa na kibiashara.Hivi ndivyo "Cosa Nostra" na jamii yao walivyojiimarisha.

Alipenya katika siasa za Italia kuanzia ngazi ya chini na akawa mwanasiasa mahili na hatimaye PM wa Italia.

Kila ulipotaka kumgusa Berluscon,ujue unamgusa Gatusso na Paul Maldin wachezaji wa AC Milan,unamgusa Mtangazaji wa habari za michezo na burudani,unawagusa mashabiki wa AC Milan kote duniani,mwandishi wa habari na hata wafanyakazi wa kampuni za simu alizokuwa anamiliki.Huu ndio ujanja wa hawa watu.

Yanga na Ngaya watu wanataka kuingia na mabango uwanjani,wanataka kufikisha ujumbe kwa serikali kuwa iachane na Rais wao na timu yao,wanaamini kwa Rais wao kuguswa,basi imeguswa furaha yao ktk mpira,unaguswa ubingwa wa Yanga wanaouwania,unatikiswa ushiriki wa Yanga katika mashindano ya klabu bingwa Afrika.

Gazeti la Jambo Leo na wafanyakazi wake wanaguswa,kuanzia mhariri mpaka "maripota".Mchora vibonzo wa gazeti mpaka msanifu wa kurasa za gazeti.Hawa wote ajira zao ziko shakani.Achilia mbali wafanyakazi katika viwanda na kampuni tanzu zote chini ya kampuni mama.

Washirika wa karibu wa RC wa Dsm nao ni watu wanaowekwa ktk mizania mbaya katika usafi wa biashara wanazozifanya.Toka kubadili jina la kampuni na kuanza na jina jipya.Tuhumu zao kwa jina lao la zamani la kibiashara haimaanishi zimeisha baada ya wao kuchukua jina jipya.

Watu ni walewale,nia ni ileile na malengo ni yaleyale.

Nao walijitakasa vizuri,wakajipenyeza katika siasa na kuwa na watu wenye ushawishi katika siasa za nchi.Walijenga shule ya msingi Mwabepande na kuigawa bureeee!!Hawa siku ukiwasema,wale wazazi na watoto wanaosoma shule hiyo lazima wakuvamie.

Waliamua kuujenga msikiti na jengo la makao makuu ya dini moja maarufu.Mbele ya kiongozi wa dini kitaifa na waandamizi wake,ahadi nyingi zilitoka.Unapoanza kuwagusa,ujue unawagusa mpaka wale waliojengewa nyumba ya ibada.Hii vita hutaiweza.

Waliamua kujenga jengo la tiba ya Mama na mtoto hospital ya Mwananyamala,na kumkabidhi Makonda akiwa DC wa Kinondoni.Ukiwagusa hawa,basi umewagusa kina mama wajawazito na watoto wanaofaidika na jengo hili.Tegemea lawama kila unapowasumbua kwa tuhuma yoyote.

Huduma ya Afya bure pale viwanja vya Mnazi Mmoja zilizotolewa buree kwa hisani yao na uratibu wa RC Dsm.Walitoa pesa ili kuhudumia huduma ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mdomo sungura,hii ilikuwa huduma iliowagusa wananchi wengi wasio na uwezo na wasiokuwa na nafasi ya kuwafanyia tiba hiyo watoto wao.

Unapowagusa hawa,unakuwa umewagusa kina mama masikini waliopata huduma hii ya kuokoa maisha ya watoto wao.Unakuwa umewagusa wazee na vijana waliojitokeza kupata huduma ktk viwanja vya Mnazi Mmoja.

Hizi ni pande mbili...ni kama vile "Cosa Nostra".Unampata kiongozi wa kisiasa,unamkamata na unampa uwezo na nafasi ya kuhakikisha,anakutengenezea mazingira ya kutawala "soko" na kuwaweka wengine ktk ramani ya "utuhumiwa" ili wewe uendelee kufanya yako bila bugudha.

Hii ndo dunia,hii ndio Afrika,being a political leader in Africa is a synonimous of being rich.Vita dhidi ya mihadarati ni vita ya kuungwa mkono,iendelezwe na ipigiwe chapuo.Lakini isiwe tu,watu wanatuingiza mkenge kwa ushindani wa ku-dominate soko,iwe katika "black market" au ushindani mwingine wa biashara za wazi.
Kwani mbowe na wema ni wa cartel gani? Cartel chawema!!!
 
Hivi hao wauza ngada si waanzishe shule za sekondar waniajir najua watanilipa vizur na uhakika wa matibabu kuliko hii ajira ya kikuda ya kupandishwa daraja baada ya mafunzo maalum, si bora hata wauza ngada wangejenga hospital ambazo zingeajir madaktar wanaozurula kwa kukosa ajira na wengine kwenda kuhatarisha maisha huko jirani na al- shabaab kenya mbona tumbaku inaendelea kuua watu na bado ina tbs?
 
Nilipomsikiliza Makonda akiulizwa suala la vita ya madawa kaanzisha ili kuwatetea rafiki zake,namna alivyojibu,nikaikumbuka hii thread ya bwana mkuu barafu
Mkuu barafu uliona mbali sana
 
Back
Top Bottom