Yaliyotaka kutokea leo uwanja wa Taifa,ndio matokeo ya "siasa" za Vita ya madawa ya kulevya

Tunaweza kuwa tumeingizwa mkenge,kujua mbinu za "black market" inahitaji kuwa makini sana!

Berluscon PM wa Italia miaka hiyo,akiwa kama mshirika wa Mafioso,wale Mafia wa Kisiwa cha Sicilia,akina Salvatore Capello na Luigi Giaccomo,aliona hatari ya kuja kufungwa siku moja,kama atakuja kutokea PM "katili" Italia aliyetaka kuidondosha "Cosa Nostra"ya Parelmo,Catania na Aggrigento miji ya kisiwa cha Sicilia kusini mwa Italia.Walikojaa wauzaji wa madawa ya kulevya na uharamia wote wa dunia.

Alichokifanya Berluscon ni kuhakikisha anatakatisha pesa yake ktk miradi inayogusa maisha ya watu,furaha za watu na starehe za kila siku za watu wa masikini na matajili,ili kila anapotaka kuguswa basi nchi nzima ilipuke kwa kauli moja "ANAONEWAAAA"

Aliamua kuanzisha TV maarufu sana inaitwa "TeleMilano",akaajiri watu wengi sana,akaanzisha Gazeti na kuajili watu wengi sana,akanzisha mahoteli na Casino na mwisho akainunua timu ya mpira kubwaaa pale Milani ya AC Milan,na mwanae wa kike ndio akawa kiongozi wa timu

Mpira ni utamaduni wa Wataliano,ukitaka wakuuwe,basi haribu mpira.Hapa ndipo mioyo ya wanazi wa mpira wa Milan ikawa kwa Silvio,akajitahidi kusajili wachezaji wa kiwango cha dunia,akachukua vikombe vya ndani na nje ya Italia.Akaweka furaha ya watu wa mpira katika kilele cha mafanikio.

Ikawa ukimgusa Berluscon basi umemgusa shabiki wa Milan,ukimgusa tena basi umemgusa mwandishi wa habari wa gazeti analomiliki,ukimgusa tena basi umegusa mtangazaji wa Tv ya TeleMilano,ukienda huko na kumgusa,basi umegusa wafanyakazi wake wa hotel na Cassino au washirika wake wa kisiasa na kibiashara.Hivi ndivyo "Cosa Nostra" na jamii yao walivyojiimarisha.

Alipenya katika siasa za Italia kuanzia ngazi ya chini na akawa mwanasiasa mahili na hatimaye PM wa Italia.

Kila ulipotaka kumgusa Berluscon,ujue unamgusa Gatusso na Paul Maldin wachezaji wa AC Milan,unamgusa Mtangazaji wa habari za michezo na burudani,unawagusa mashabiki wa AC Milan kote duniani,mwandishi wa habari na hata wafanyakazi wa kampuni za simu alizokuwa anamiliki.Huu ndio ujanja wa hawa watu.

Yanga na Ngaya watu wanataka kuingia na mabango uwanjani,wanataka kufikisha ujumbe kwa serikali kuwa iachane na Rais wao na timu yao,wanaamini kwa Rais wao kuguswa,basi imeguswa furaha yao ktk mpira,unaguswa ubingwa wa Yanga wanaouwania,unatikiswa ushiriki wa Yanga katika mashindano ya klabu bingwa Afrika.

Gazeti la Jambo Leo na wafanyakazi wake wanaguswa,kuanzia mhariri mpaka "maripota".Mchora vibonzo wa gazeti mpaka msanifu wa kurasa za gazeti.Hawa wote ajira zao ziko shakani.Achilia mbali wafanyakazi katika viwanda na kampuni tanzu zote chini ya kampuni mama.

Washirika wa karibu wa RC wa Dsm nao ni watu wanaowekwa ktk mizania mbaya katika usafi wa biashara wanazozifanya.Toka kubadili jina la kampuni na kuanza na jina jipya.Tuhumu zao kwa jina lao la zamani la kibiashara haimaanishi zimeisha baada ya wao kuchukua jina jipya.

Watu ni walewale,nia ni ileile na malengo ni yaleyale.

Nao walijitakasa vizuri,wakajipenyeza katika siasa na kuwa na watu wenye ushawishi katika siasa za nchi.Walijenga shule ya msingi Mwabepande na kuigawa bureeee!!Hawa siku ukiwasema,wale wazazi na watoto wanaosoma shule hiyo lazima wakuvamie.

Waliamua kuujenga msikiti na jengo la makao makuu ya dini moja maarufu.Mbele ya kiongozi wa dini kitaifa na waandamizi wake,ahadi nyingi zilitoka.Unapoanza kuwagusa,ujue unawagusa mpaka wale waliojengewa nyumba ya ibada.Hii vita hutaiweza.

Waliamua kujenga jengo la tiba ya Mama na mtoto hospital ya Mwananyamala,na kumkabidhi Makonda akiwa DC wa Kinondoni.Ukiwagusa hawa,basi umewagusa kina mama wajawazito na watoto wanaofaidika na jengo hili.Tegemea lawama kila unapowasumbua kwa tuhuma yoyote.

Huduma ya Afya bure pale viwanja vya Mnazi Mmoja zilizotolewa buree kwa hisani yao na uratibu wa RC Dsm.Walitoa pesa ili kuhudumia huduma ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mdomo sungura,hii ilikuwa huduma iliowagusa wananchi wengi wasio na uwezo na wasiokuwa na nafasi ya kuwafanyia tiba hiyo watoto wao.

Unapowagusa hawa,unakuwa umewagusa kina mama masikini waliopata huduma hii ya kuokoa maisha ya watoto wao.Unakuwa umewagusa wazee na vijana waliojitokeza kupata huduma ktk viwanja vya Mnazi Mmoja.

Hizi ni pande mbili...ni kama vile "Cosa Nostra".Unampata kiongozi wa kisiasa,unamkamata na unampa uwezo na nafasi ya kuhakikisha,anakutengenezea mazingira ya kutawala "soko" na kuwaweka wengine ktk ramani ya "utuhumiwa" ili wewe uendelee kufanya yako bila bugudha.

Hii ndo dunia,hii ndio Afrika,being a political leader in Africa is a synonimous of being rich.Vita dhidi ya mihadarati ni vita ya kuungwa mkono,iendelezwe na ipigiwe chapuo.Lakini isiwe tu,watu wanatuingiza mkenge kwa ushindani wa ku-dominate soko,iwe katika "black market" au ushindani mwingine wa biashara za wazi.
Imasemwa wakati mwafaka. Wenye masikio na wasikie.
 
Andishi matata sana hili japo kuna hayawani walioshikiwa akili wao watapinga kwa mayowe na matusi yote duniani.
 
Siku Rais Alipowaita Wahariri Wa Vyombo Vya Habari Pale Ikulu Mkuu Barafu Ulikuwa Wapi ?
Hii Thread Yako Nayo Inakwenda Kuwa The Best Thread Never Seen Before.

Tulipeleka Wahariri Mizigo Pale Ikulu Hata Kuuliza Maswali Hawajui.
Next Time Rais Akiita Watu Uende Ukajitambulishe Kuwa Wewe Ni Barafu Wa Jf
Halafu Shusha Nondo Ya Swali Makini
Naamini Hutatuangusha Kamwe

mkuu umesema kweli kabisa nondo za mkuu Barafu ni hatareee.......
 
Ahsante barafu uwa na kuheshimu sana katika maandiko yako ingekua katika kazi za fasihi ningekuita muhusika duara, sababu ya unyumbufu wako, unanyumbulika vizuri penye chanya unaeleza chanya, penye hasi unaeleza hasi
 
Wanamshangilia Manji Leo waende wakasome historia kina Duduz walinunua wananchi wote, na walikua karibu na jamii kuliko serikali lakini wauza poda
 
Tunaweza kuwa tumeingizwa mkenge,kujua mbinu za "black market" inahitaji kuwa makini sana!

Berluscon PM wa Italia miaka hiyo,akiwa kama mshirika wa Mafioso,wale Mafia wa Kisiwa cha Sicilia,akina Salvatore Capello na Luigi Giaccomo,aliona hatari ya kuja kufungwa siku moja,kama atakuja kutokea PM "katili" Italia aliyetaka kuidondosha "Cosa Nostra"ya Parelmo,Catania na Aggrigento miji ya kisiwa cha Sicilia kusini mwa Italia.Walikojaa wauzaji wa madawa ya kulevya na uharamia wote wa dunia.

Alichokifanya Berluscon ni kuhakikisha anatakatisha pesa yake ktk miradi inayogusa maisha ya watu,furaha za watu na starehe za kila siku za watu wa masikini na matajili,ili kila anapotaka kuguswa basi nchi nzima ilipuke kwa kauli moja "ANAONEWAAAA"

Aliamua kuanzisha TV maarufu sana inaitwa "TeleMilano",akaajiri watu wengi sana,akaanzisha Gazeti na kuajili watu wengi sana,akanzisha mahoteli na Casino na mwisho akainunua timu ya mpira kubwaaa pale Milani ya AC Milan,na mwanae wa kike ndio akawa kiongozi wa timu

Mpira ni utamaduni wa Wataliano,ukitaka wakuuwe,basi haribu mpira.Hapa ndipo mioyo ya wanazi wa mpira wa Milan ikawa kwa Silvio,akajitahidi kusajili wachezaji wa kiwango cha dunia,akachukua vikombe vya ndani na nje ya Italia.Akaweka furaha ya watu wa mpira katika kilele cha mafanikio.

Ikawa ukimgusa Berluscon basi umemgusa shabiki wa Milan,ukimgusa tena basi umemgusa mwandishi wa habari wa gazeti analomiliki,ukimgusa tena basi umegusa mtangazaji wa Tv ya TeleMilano,ukienda huko na kumgusa,basi umegusa wafanyakazi wake wa hotel na Cassino au washirika wake wa kisiasa na kibiashara.Hivi ndivyo "Cosa Nostra" na jamii yao walivyojiimarisha.

Alipenya katika siasa za Italia kuanzia ngazi ya chini na akawa mwanasiasa mahili na hatimaye PM wa Italia.

Kila ulipotaka kumgusa Berluscon,ujue unamgusa Gatusso na Paul Maldin wachezaji wa AC Milan,unamgusa Mtangazaji wa habari za michezo na burudani,unawagusa mashabiki wa AC Milan kote duniani,mwandishi wa habari na hata wafanyakazi wa kampuni za simu alizokuwa anamiliki.Huu ndio ujanja wa hawa watu.

Yanga na Ngaya watu wanataka kuingia na mabango uwanjani,wanataka kufikisha ujumbe kwa serikali kuwa iachane na Rais wao na timu yao,wanaamini kwa Rais wao kuguswa,basi imeguswa furaha yao ktk mpira,unaguswa ubingwa wa Yanga wanaouwania,unatikiswa ushiriki wa Yanga katika mashindano ya klabu bingwa Afrika.

Gazeti la Jambo Leo na wafanyakazi wake wanaguswa,kuanzia mhariri mpaka "maripota".Mchora vibonzo wa gazeti mpaka msanifu wa kurasa za gazeti.Hawa wote ajira zao ziko shakani.Achilia mbali wafanyakazi katika viwanda na kampuni tanzu zote chini ya kampuni mama.

Washirika wa karibu wa RC wa Dsm nao ni watu wanaowekwa ktk mizania mbaya katika usafi wa biashara wanazozifanya.Toka kubadili jina la kampuni na kuanza na jina jipya.Tuhumu zao kwa jina lao la zamani la kibiashara haimaanishi zimeisha baada ya wao kuchukua jina jipya.

Watu ni walewale,nia ni ileile na malengo ni yaleyale.

Nao walijitakasa vizuri,wakajipenyeza katika siasa na kuwa na watu wenye ushawishi katika siasa za nchi.Walijenga shule ya msingi Mwabepande na kuigawa bureeee!!Hawa siku ukiwasema,wale wazazi na watoto wanaosoma shule hiyo lazima wakuvamie.

Waliamua kuujenga msikiti na jengo la makao makuu ya dini moja maarufu.Mbele ya kiongozi wa dini kitaifa na waandamizi wake,ahadi nyingi zilitoka.Unapoanza kuwagusa,ujue unawagusa mpaka wale waliojengewa nyumba ya ibada.Hii vita hutaiweza.

Waliamua kujenga jengo la tiba ya Mama na mtoto hospital ya Mwananyamala,na kumkabidhi Makonda akiwa DC wa Kinondoni.Ukiwagusa hawa,basi umewagusa kina mama wajawazito na watoto wanaofaidika na jengo hili.Tegemea lawama kila unapowasumbua kwa tuhuma yoyote.

Huduma ya Afya bure pale viwanja vya Mnazi Mmoja zilizotolewa buree kwa hisani yao na uratibu wa RC Dsm.Walitoa pesa ili kuhudumia huduma ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mdomo sungura,hii ilikuwa huduma iliowagusa wananchi wengi wasio na uwezo na wasiokuwa na nafasi ya kuwafanyia tiba hiyo watoto wao.

Unapowagusa hawa,unakuwa umewagusa kina mama masikini waliopata huduma hii ya kuokoa maisha ya watoto wao.Unakuwa umewagusa wazee na vijana waliojitokeza kupata huduma ktk viwanja vya Mnazi Mmoja.

Hizi ni pande mbili...ni kama vile "Cosa Nostra".Unampata kiongozi wa kisiasa,unamkamata na unampa uwezo na nafasi ya kuhakikisha,anakutengenezea mazingira ya kutawala "soko" na kuwaweka wengine ktk ramani ya "utuhumiwa" ili wewe uendelee kufanya yako bila bugudha.

Hii ndo dunia,hii ndio Afrika,being a political leader in Africa is a synonimous of being rich.Vita dhidi ya mihadarati ni vita ya kuungwa mkono,iendelezwe na ipigiwe chapuo.Lakini isiwe tu,watu wanatuingiza mkenge kwa ushindani wa ku-dominate soko,iwe katika "black market" au ushindani mwingine wa biashara za wazi.

Mwanzoni RC alikuwa na nia njema ila alipoanza na orodha kuzitangaza hadharani palikuwepo na "handbrake" kidogo kuna tetesi kuwa zile sio orodha kamili (yaani zimefanyiwa editing)

Ingawa orodha zile zimetikisa lakini sio ule mtikisiko mkuu ambao ulianza kuwafanbya baadhi ya watu kwenda hadi kwenye vyombo vya habari kuanza kujieleza ( sio Manji).

Lakini kiujumla mzee Adadi na Siang'a tayari wamesema kuhusu utaalam ulivyo na nafasi yake katika vita hii, tena Adadi akasema kwamba kuna shshsda ya mambo ya uchunguzi wa masuala haya.

Tatizo kubwa watanzania ni wanafiki sana maana wanafahamu kila mhusika wa biashara hii na wengine wanajitokeza hadharani na katika JF kupinga juhudi za serikali.

Pia mkulu alisema wazi (rejea hotuba kwa wafanyabiashara) kwamba ndiyo maana yeye hakutaka fedha zozote za michango.

Lakini labda alisahau jinsi baadhi ya nguli wa biashara hii walikoanzia biashara yenyewe sawa tu na bwana Berlusconi aka mzee wa totoz ziitwazo "bongabonga girls".

Watanzania wana budi kuhakikisha twaunga mkono vita dhidi ya biashara ya mihadarati popote pale tulipo.
 
Hata Katibu mkuu kiongozi aliyepita aliaminiwa sana kuja kushitukia maneno ya kwenye magazeti aaah nae kumbe anamtandao wake.
 
Good analysis, well presented piece of argument... We need jf GT to come out with analytical issues like this... I like it
 
Back
Top Bottom