Hess
JF-Expert Member
- Feb 27, 2012
- 593
- 674
Tunaiunga vita ipi? Kuna aliyetangaza vita Tanzania ya sembe? Uwe unatazama mambo with your eyes wide open.Mwanzoni RC alikuwa na nia njema ila alipoanza na orodha kuzitangaza hadharani palikuwepo na "handbrake" kidogo kuna tetesi kuwa zile sio orodha kamili (yaani zimefanyiwa editing)
Ingawa orodha zile zimetikisa lakini sio ule mtikisiko mkuu ambao ulianza kuwafanbya baadhi ya watu kwenda hadi kwenye vyombo vya habari kuanza kujieleza ( sio Manji).
Lakini kiujumla mzee Adadi na Siang'a tayari wamesema kuhusu utaalam ulivyo na nafasi yake katika vita hii, tena Adadi akasema kwamba kuna shshsda ya mambo ya uchunguzi wa masuala haya.
Tatizo kubwa watanzania ni wanafiki sana maana wanafahamu kila mhusika wa biashara hii na wengine wanajitokeza hadharani na katika JF kupinga juhudi za serikali.
Pia mkulu alisema wazi (rejea hotuba kwa wafanyabiashara) kwamba ndiyo maana yeye hakutaka fedha zozote za michango.
Lakini labda alisahau jinsi baadhi ya nguli wa biashara hii walikoanzia biashara yenyewe sawa tu na bwana Berlusconi aka mzee wa totoz ziitwazo "bongabonga girls".
Watanzania wana budi kuhakikisha twaunga mkono vita dhidi ya biashara ya mihadarati popote pale tulipo.