Taasisi ya RITA Ni nyeti mno na ilistahili kuwa na wafanyakazi mahili na waadilifu.
Miezi miwili nafuatilia cheti Cha kifo Cha mwanafamillia hadi leo sijakipata.
Kabla yakuanza mchakato wa kufuatilia cheti hicho nilipiga simu huduma kwa wateja kuulizia utaratibu wa kufuata ,
Waliniambia kunahitajika nyaraka ya Hospitali inayothibitisha kifo cha marehemu , kunahitajika barua ya mukhtasari wa kikao Cha ndugu Cha kumteua msimamizi wa mirathi,barua ya utambulisho toka serikali ya mtaa inayothibitisha kifo Cha marehemu, na msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa ndiye anayepaswa kufuatilia hiko cheti.
Baada ya kukamilisha nyaraka hizo tulikwenda RITA lakini baada ya nyaraka zetu kukaguliwa tukaambiwa kunahitajika kopi ya kitambulisho Cha NIDA Cha kila mwana ndugu aliyehudhuria kikao Cha ndg Cha kumteua msimamizi wa mirathi ,
Tukarudi NYUMBANI kukusanya kopi ya cheti Cha NIDA Cha hao ndg. Baadhi ya ndg.walikuwa wamesafiri baada yamuda tukapata kopi zote tukarejea RITA ,
Baada ya kufika nyaraka kukaguliwa tukaambiwa hao ndugu wanahitajika kuwepo kuthibitishwa !!!
Tukarudi NYUMBANI tukatafuta baadhi ya ndugu siku nyingine tukarudi RITA na ndugu ,
Baada ya nyaraka kukaguliwa Tena tukaambiwa eti barua ya serikali ya mtaa haijaandika tarehe ya kifo !
Tukumbuke nyaraka ya Hospitali. Na mukhtasari wa kikao Cha ndg. Tarehe ya kifo ipo lakini mtoa huduma akasema lazima barua ya serikali ya mtaa iandike tarehe ya kifo Cha marehemu ,
Tukarudi NYUMBANI barua ikarekebishwa siku hiyohiyo na hatimaye tukatakiwa kulipia gharama ya cheti na tukapewa tarehe ya kurudi kuchukua cheti Cha kifo .
Tarehe ilipofika tukaenda RITA cheti Kiko tayari lakini tarehe ya kifo imekosewa imeandikwa tarehe ya kuzaliwa ya marehemu na sababu ya kifo imekosewa imeandikwa kifo kisicho Cha kawaida badala ya kifo Cha kawaida kwakuwa marehemu alikufa kwa ugonjwa .
Tukapewa Tena tarehe ya kurudi RITA ili cheti kirekebishwe , baada ya kurudi Tena RITA kukaa foleni masaa mawili baada ya kufika kwahudumu anatuambie eti cheti hakijatoka kwa sababu hatujalipia gharama za marekebisho !!
Ni Jambo la ajabu Sana makosa yamefanywa na RITA lakini gharama alipe aliyekosewa !!
Mbaya zaidi hatukuambiwa kabla tulipie gharama Bali tuliambiwa tarehe ya kurudi kuchukua cheti kilichorekebishwa ,
Baada ya kutaka kujua uhalali wa malipo hayo tukaambiwa ndiyo utaratibu wao.
Tumelipia tunasubiria cheti!!
Ndugu zangu waTanzania tuna safari ndefu Sana kupata maendeleo kwakuwa vikwazo Ni vingi Sana ,
Naomba mamlaka za juu ziichunguze RITA vyeti vinavyokosewa Ni vingi Sana tujue wanakosea makusudi ili wapate mapato ??
Kitengo Cha uchapaji kichunguzwe kama wafanyakazi wake Wana weledi wa kufanya kazi hiyo.
Nina mashaka Tukirudi Tena kuchukua cheti Kama hatutakutana na kikwazo kingine..
TANZANIA NCHI YANGU....ndu