Planett
JF-Expert Member
- Mar 20, 2014
- 10,470
- 16,121
Wassalaam wanaJF,
Nimekuwa nikisikia tuu maswahibu yanayowakumba watu pindi wanapoenda kushughulikia mambo yao katika ofisi mbalimbali za ardhi lakini nilikuwa sijawahi kutana na vitimbi vya huko, leo yamenikuta nduguzanguni.
Mkasa upo hivi.
Jana nilikutana na mtu anauza kiwanja ili apate hela ya kumpeleka mwanae shule nikaona sio mbaya hata kama sina mahitaji nacho wacha nikinunue kwani kinaweza kunifaa baadae. Nikaondoka na mmiliki wa kiwanja hadi mahakamani tukaandikiana fresh (within 10 minutes tukamaliza issue ya nahakamani, hongera kilwa primary court). Baadae mida ya saa 4 tukaenda ardhi huko tukaambiwa tulipie 10% ya gharama tyliyouziana ndio suala letu lishughulikiwe nasi bila khiyana tukaenda bank tukalipia.
Baadae tukapeleka risiti ofisini ili watuandalie hati na hapa kasheshe ndio ilipoanzia. Kuna mfanyakazi mmoja tumempa risiti na hatu ili atubadilishie jina akaweka mezani na kuendelea kuchat na simu yake.
Kuona vile muuzaji akasema nitoe chochote kwani tunachelewa na mwanae anachelewa kwenda shule, nikatia hela na yule mfanyakazi akaipikea bila aibu then akavuta file akaliangalia baadae akaondoka hadi jioni hajarudi tena.
Leo asubuhi tumemfuata akasema kunamtu ambaye alimkabidhi ile kazi kasafiri na doccument zote hajui zilipo. Tukatafuta namba yake tukampigia jamaa akasema yeye anazo picha tuu ila file liko kwa huyu wa mwanzo.
Tukamfuata na kumuuliza vipi mbona tumeambiwa kuwa file lipo kwako isipokuwa picha tuu ambazo tunaweza kwenda kutafuta nyingine? Akasema tafuteni picha niifanye hii kazi. Basi tumeenda kutafuta picha nyingine tumempelekea anatupa jibu SINA UTAALAMU WA KUTENGENEZA HATI?
Kwa kweli huku kwenye halmashauri majipu ni mengi sana ndugu zangu.