habari zenu wana JF. Ngoja niwaelezee changamoto niliyoipa leo kama msaka ajira. Kama mnavyojua ajira ni ngumu, basi kuna siku nimeingia zoom tanzania nikaona kazi ya kukusanya taarifa kampuni ya Neema Herbalist kwa malipo ya Tshs 5,000/= kwa kila taarifa ya mtu mmoja mwenye matatizo ya kitambi, unene uliozidi na matatizo ya lishe, na mkusanya taarifa anatakiwa akusanye taarifa za watu 100 kwa siku 20 hivyo ukifanikiwa unalipwa laki 5, nikaona ni kazi nzuri so nika apply baada ya siku nikatumiwa email na attachment nijaze then niende ofisini kwao changanyikeni tar 8/10, basi leo nikaenda na mzuka wangu wa kazi. Bahati mbaya nikachelewa kama nusu saa, so nikakuta ofisi imefungwa, nikapiga namba zao zote hazipatikani, nikafika jirani kuulizia ndo wakaniambia kua jamaa alikuwepo hapo kuna watu walikuja wakaongea nae then waasepa nae. Nikaanza kuwadadisi kuhusu huyo jamaa, nikagundua jamaa ni mtu wa mambo mengi nasikia alifungu darasa la ujasiria mali akazinguana na wanafunzi wake, mara ofisi yake anabadilisha jina kila mara. Nakaona kweli watu wanajua kutumia fursa za tatizo la ajira kutaka kujinufaisha wao