Yaliyonikuta Leo

Yaliyonikuta Leo

Hata Ridhiwani alisema anaishi kimjinimjini. Ndio tatizo linaanzia hapo, kama mtoto wa Rais anaishi kimjinimjini unadhani wale wengine wasio na ajira watafanyaje? Tunakoelekea ni kubaya zaidi kuliko tunavyodhani
 
Pole sana mkuu, ila ningekuwa mimi ningemuondoa na vibao mpaka angesahau jinsia yake. Hana haya huyo mzee, ni mwivi tu huyo.
 
Duh! Umekuwa mstaarabu sana. Kuna mmoja nae alijigongesha kwa bro mmoja akajifanya kaumia sana. Yule bro akamwambia panda nikupeleke hospitali. Akamchukua akaenda kumbwaga kibamba ndani ndani.
 
Nikiwa naendesha kariakoo kaja mwanaume wa makamo hivi namuona makusudi anajigongesha kwenye kioo
cha gari cha pembeni.

Mie nikasimama mara anadai nimpeleke hospital kaumia nikamwambia umeumia wapi na gari haikuwa kasi sanasana umegusa kioo .
Kashupaa nimpeleke hospital au nimpe pesa akatibiwe.

Nikampa 10,000.00 ili yaishe bwana wee nimeenda kupaki nazunguka kariakoo na kutana naye anadunda swafi kabisa!

Jamani hali ya uchumi hii itatupeleka pabaya mtu mzima kama yeye nimesikitika sana.
so ukiwa kariakoo uwe mwangalifu sana.
Watu wanabuni njia mbalimbali za kujipatia pesa kiurahisi.
Una bahati haukuibiwa maana ndo mbinu zao hizo... mmoja anajifanya kukusemesha kwenye kesi huku upande mwingine wengine wanafanya vitu vyao
 
Nilishuhudia mkasa mwingine kama huo, eneo la kwa Mtogole, Tandale mwaka jana. Ilikuwa ni asubuhi sana nikiwa ndani ya basi la daladala naenda Ubungo bus terminal, tuliwakuta wazee wawili bibi na babu, kondakita alivyotaka kuondoa gari wale wazee wakaja mbio kama wanataka kupanda basi, ghafula wote wakaanguka chini.

Abiria wakapiga kelele dereva akasimama, wale wazee wakachachamaa na kudai kondakita amewasukuma, kondakita aliwaomba radhi na kuwaachia pesa, ajabu hawakuingia tena kwenye basi lile kuendelea na safari yao.

Wanafunzi wa shule waliokuwa ndani ya lile basi wakasema huo ndio mchezo wa hao wazee kila siku asubuhi, basi linapoanza kuondoka nao hujitokeza kama wanapanda, kisha hujiangusha chini kama wamesukumwa na kondakita na kudai pesa za kwenda kutibiwa.
 
"Ukimgusa" mtu na gari halafu ukasimama (hasa maendeo kama k'koo kwenye watu wengi) unajitafutia matatizo.

Kama unadhani umemuumiza mtu angalia ustaarabu wa kumbeba na kumpeleka hospitali (kama unaona kuna usalama) ukatoe taarifa kituo cha polisi (ndani ya saa 12 kama sikosei). Kama mtu hajaumia ni bora uwe mkali na uondoe gari mara moja maana yanaweza kukupata makubwa.

Kuna mtaa huku kwetu, akigongwa mtu na gari, basi hakuna gari zitakazopita hapo kwa saa kadhaa maana kila gari itapigwa mawe! Kitu cha ajabu ni kwamba wadanganyika wengi wanadhani kila anayeendesha gari ana hela nyingi ambazo zipozipo tu.

Trafiki akiona huna kosa lolote, utasikia "bosi nisaidie ya chai basi"!Kisa hiki kimenikumbusha jamaa yangu wa arusha anayetembea na sime kwenye gari yake tayari kwa kuwashughulikia madereva wa daladala wanapomchomekea!
 
Nikiwa naendesha kariakoo kaja mwanaume wa makamo hivi namuona makusudi anajigongesha kwenye kioo
cha gari cha pembeni.

Mie nikasimama mara anadai nimpeleke hospital kaumia nikamwambia umeumia wapi na gari haikuwa kasi sanasana umegusa kioo .
Kashupaa nimpeleke hospital au nimpe pesa akatibiwe.

Nikampa 10,000.00 ili yaishe bwana wee nimeenda kupaki nazunguka kariakoo na kutana naye anadunda swafi kabisa!

Jamani hali ya uchumi hii itatupeleka pabaya mtu mzima kama yeye nimesikitika sana.
so ukiwa kariakoo uwe mwangalifu sana.
Watu wanabuni njia mbalimbali za kujipatia pesa kiurahisi.

Ha ha ha!!
Sasa hivi kuna wazee wa mjini wanajua sana jinsi ya kuwatoa vijana ili siku iishe. Jana jumamosi hiyo hiyo, mzee mmoja kaja ofisini kwangu akidai anatoka idara fulani ya serikali tunayofanya nayo kazi.

Akaeleza kuwa ana mgonjwa muhimbili ana ana ukimwi na madaktari wameshauri arudishwe tu nyumbani.
Huyo mzee amejiita jina ambalo najua ni la kipare lakini lafudhi yake ya kichagga.

Yeye akaeleza kuwa amestaafu muda si mrefiu kutoka idara hiyo ya serikali na anomba msaada.

Mimi nikampiga masuali machache kwamba kwa nini asiende kutafuta msaada toka idara hio hiyo alikostaafu, na je hana uhusiano mzuri na waliobaki?

Alipoanza kubwabwaja nikampiga na 10,000 na kumueleza kuwa sina cha kusaidia zaidi.

Mara akaingia ofisini jamaa ambaye anamfahamu fika huyu mzee na kumsalimia kichagga , jamaa akaeleza kuwa wanatoka kijiji kimoja Machame.

Nikashamgaa sana na yule mzee na kwa aibu akaaga haraka haraka kabla sijamdai ile 10,000 yangu.
Mjini kuna mambo
 
Mi ningemshukia na bonge la panga' kudadeki angenitambua.

Hata mimi maana kila nikiingia kwenye gari lazima nihakikishe lipo mahala pake..ni PANGA tu kwa nini kama anashida asiombe na sio kuleta ulaghai
 
Inaonekana wewe ni mwepesi sana hata kutoa rushwa. na unaweza kutapeliwa kirahisi.

But pole sana.
 
Uwizi huo upo D'Salaam kwa sababu watuwa huko mnapenda politic sana. Arusha umfanyie mambo ya kipumbavu kama hayo unalimwa mabao tu. Mimi natembea na sime kabisa ukileta za kuleta nakuarrest moja kwa moja kwa kamanda Andengenye.

Nashukuru mtoamada uliona kheri nusu shari kuliko shari kamili ukaassume umeeka lita 4.6 hivi ili kumtoa tapeli hilo ambalo labda lilikuwa na jamaa zake hapo tayari kukubabaisha.
 
Naona wameadvance. Zamani walikuwa wakiona unapita wanamwaga nyanya mbovu halafu wanadai umepandia nyanya zao. Watakubana mpaka uzilipie. Sasa wewe uwe unatembea na bakora kwneye gari. Akijidai umemgonga, wewe toka ndani kiulani na bakora uone jinsi atakavyotoka nduki.
 
Nikiwa naendesha kariakoo kaja mwanaume wa makamo hivi namuona makusudi anajigongesha kwenye kioo
cha gari cha pembeni.

Mie nikasimama mara anadai nimpeleke hospital kaumia nikamwambia umeumia wapi na gari haikuwa kasi sanasana umegusa kioo .
Kashupaa nimpeleke hospital au nimpe pesa akatibiwe.

Nikampa 10,000.00 ili yaishe bwana wee nimeenda kupaki nazunguka kariakoo na kutana naye anadunda swafi kabisa!

Jamani hali ya uchumi hii itatupeleka pabaya mtu mzima kama yeye nimesikitika sana.
so ukiwa kariakoo uwe mwangalifu sana.
Watu wanabuni njia mbalimbali za kujipatia pesa kiurahisi.
Lol...
 
pole mkuu!!!! kwa siku labda huyo mdingi anasanya pesa ya kutosha,ila kunasiku atagongwa kiukweli af ndo atakoma ubish
 
hahaha pole mkuu .... Kuna signature ya mdau flani ni one of my Fev inasema hivi "MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO" uwezo wa kubuni njia za kutuingizia kipato ni mdogo sana....

Too bad! Very good symptoms of a "well matured negative self esteem of the writer/thinker"

Tatizo mnasoma vya darasani tu ili uje upate "A" kwenye mtihani, nje ya hapo vingine vyote unakuwa uko NIL. Fuatilieni pia historia za social sytems, especially zilizoendelea, zinavyo-sail ili muweze kuwa na uhakika kwamba hivi vitu vinafanyika hapa kwetu Africa tu, na havijawahi kufanyika sehemu nyingine yeyote duniani, au la!

Watu wamefanya vitu vikubwa duniani, na si hivi vya kujigongesha kwenye gari kisa elfu kumi,.... halafu unabwabwaja "miafrika ndibvyo tulivyo,....

I hate the statement, especially, its inventor!
 
Ungempakia ukampeleka dispensary tu usingempa ki2, lengo lake linge'disolve"
 
pole sana, hata dada yangu yalishamkuta, kariakoo mitaa ya ndani ndani kule, wabaya sana wanajua kabisa ni uongo lakini watu wanashupalia umpeleke hosp. ilibidi amtoe na kitu kidogo. shida bana
 
Back
Top Bottom