Nadhani umesoma andiko langu lakini hukuelewa msingi wa hoja yangu.
Nami nimelisoma andiko lako kwa umakini.
Hongera kwa kuhusisha matukio, ukayajumlisha, ukayachanganya, ukayajumuisha kisha ukayachambua kufikia hitimisho kwamba
"CCM kuna watu (viongozi) wanapenda kuwa karibu na Rais (kujikomba)". Kimsingi hao kwangu nawaona kama watafuta
'Political Power' (Nguvu Kisiasa).
Hakika hilo ni hitimisho zito sana, lakini linakosa ushahidi wa moja kwa moja zaidi ya hisia zako.
Ni imani yetu, wanao hisiwa (viongizi wa kisiasa CCM) kufanya hivyo, au kama ni kweli wanafanya hivyo, iwapo wanasoma JF, warekebishe tabia hiyo kwa kuwa Rais Magufuli ni tofauti na Marais waliomtangulia, kutokana na mazingira ya utawala yalivyotofautiana sana, kama ifuatavyo:
1) Baba wa Taifa, kama mwazilishi wa Taifa hili, alikuwa na wajibu wa kujenga Umoja wa Kitaifa dhidi ya utawala wa kitemi. Kitu alichofanikiwa, tofauti na majirani zetu. Hivyo maamuzi yake mengi (ikiwemo uteuzi na utenguaji wa wasaidizi wake) yaliongozwa na dhamira yake ya Utaifa kwanza. Kwa sababu hiyo wateuliwa wake hawakuwa na 'political power' kwa kuwa alihodhi hiyo nguvu.
2) Rais Mwinyi, amekuta nchi ikiwa na amani kutokana na kazi iliyofanywa na Baba ya Taifa,
"Utaifa Kwanza" kisha utajirisho. Hivyo pamoja na kuwa Taifa moja, wateule wake walitamani utajirisho. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuiingilia Taasisi ya Urais kwa mbinu chafu
(RUKHSA) hadi kiasi cha 'First Lady' kuitwa shemeji, na kuzikwa rasmi kwa Azimio la Arusha.
3) Rais Mkapa, alikuwa Waziri kidiplomasia (mwandishi wa habari na waziri wa mambo ya nje) katika vipindi vilivyopita, hivyo haikuwa ajabu kwake kupokea mageuzi ya kisiasa na kiuchumi yaliyojitokeza dunia wakati wake (globalisation & privatisation). Isitoshe alingia madarakani kwa nguvu ya Baba wa Taifa na siyo kwa makundi (kwani wakati huyo ubinafsishaji na kifo cha Azimio la Arusha kilikwisha jenga viongozi wenye fedha haramu na siyo tena nguvu ya kisiasa ilihitajika). Hivyo basi, yeye bahati yake hakuwa na watu wa kujikomba kwake kwa kuwa wateule wake walishindana kununua/ kuuza mashirika ya umma. Hawakuwa na muda wa kutafuta 'political power'.
4) Rais Kikwete, kama ulivyoeleza, aliingia madarakani kwa nguvu ya pesa (makundi) iliyokuwa imechumwa kifisadi. Fedha huendana na kutafuta nguvu ya kisiasa (political power). Ni katika awamu yake ndiyo tunaona kuongezeka kwa wafanya biashara matajiri na wasomi kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa. Siasa ikawa ni mtaji mkubwa wa siyo tu kupata nguvu za kisiasa lakini pia 'utajirisho'. Mazingira ya hali hii yalikwisha wekwa na Rais Mkapa, kwa makusudi au la. Kesi ya mgodi wa makaa ya mawe, ni moja ya mifano hiyo. Hivyo, viongozi wa kisiasa walipishana kwenye korido za Ikulu na kugongana mabega kuwa karibu na Rais.
5) Rais Magufuli amejipambanua kuwa tofauti na waliomtangulua kwa kutokuwa karibu na kundi lolote kisiasa na hili analiweka wazi kila siku (
hakusaidiwa na tajiri yoyote na alichukua fomu mwenyewe kugombea na hatimaye kuteuliwa Rais. Na haya maneno yanatokana na dhamira yake ya dhati (utashi wa kiasa) kuirudisha Tanzania katika utawala wa kisheria, ambao wapinzani wanauona wa kidikteta.
Hivyo kuhusu Makonda, au kiongozi yeyote mteule wake atatengua uteuzi wake, siyo kwa shinikizo la kisiasa, kama wewe 'MsemajiUkweli' unavyotaka tuamini.
Kwa Rais Magufuli, nionavyo mimi, na kwa uthibitisho wa kauli na matendo yake, kwake ni
kazi tu, siasa zinabaki ndani ya vikao vya vyama vya siasa kutengeneza sera. Inathibitishwa pia kwa aina ya wateuzi wake kushika nyadhifa mbalimbali, kwani kiasi kikubwa ni wasomi siyo wanasiasa, ingawa wapinzani wanajitahidi kuwaaminisha tofauti Watanzania.