MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Kwa wale wanafahamu siasa za Tanzania hawawezi kushangaa sana kile kinachoendelea katika sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Kinachoendelea ni mapambano ya wanasiasa ndani ya CCM wakisaidiwa na baadhi ya wanasiasa kutoka nje ya CCM.
Hiki kinachotokea kwa sasa hakina tofauti sana na kile kilichomtokea Edward Lowassa wakati akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania mara baada ya Utawala wa Rais Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005.
Sitaki kwa sasa kuwagusia kina Ukiwaona Ditopile Mzuzuri na Kitwana Kondo ambao pia walipata misukosuko ya siasa za ndani za CCM kwa kuwa karibu sana na Jakaya Kikwete.
Historia inatuonyesha mara utawala mpya unapoingia madarakani huwa kunakuwa na msuguano mkali wa wanasiasa wakipambana ili kuwa karibu na Rais wa Tanzania. Hata kinachoendelea kwa sasa ni kile kile cha kutafuta kuwa karibu na Rais wa Tanzania, ndio maana unasikia sauti za baadhi ya wanasiasa wakidai wamekipigania chama kwa nguvu zao zote mpaka Rais Magufuli akachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.
Baada ya utawala wa Rais Kikwete kuingia madarakani, Edward Lowassa alikuwa na nguvu ndani ya serikali kutokana na kuwa karibu na Rais Kikwete kiasi kwamba hakuna maamuzi ya kiserikali yaliyokuwa yanafanyika bila mkono wa Lowassa.
Kuaminiwa sana kwa Lowassa kuliwafanya baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM kujihisi kuwa mbali na Rais huku wakiamini kuwa wamefanya kazi kubwa zaidi ya Lowassa katika kuhakikisha Jakaya Kikwete anakuwa Rais wa Tanzania.
Wanasiasa walianza kutafuta madhaifu ya Lowassa ili wamsulubu kisiasa katika lengo la kuharibu mahusiano yake ya karibu na Rais Kikwete. Moja ya madhaifu ya Lowassa ilikuwa ni kutumia madaraka ‘vibaya’ na kumiliki mali nyingi bila maelezo sahihi/ufisadi .
Wanasiasa wa ndani na nje ya CCM walitengeneza kikundi cha kumsulubu kwa kutumia fimbo ya ufisadi wake mpaka akaundiwa tume ya bunge kuhusu sakata la Richmond ili kummaliza kisiasa.
Mbaya zaidi, Lowassa aliamini kuwa Rais Kikwete atamkingia kifua waziwazi bila kujua kuwa moja ya haiba ya Rais Kikwete iliyochanganyika na uzoefu wa kidiplomasia ni kupenda kufurahisha/kuridhisha makundi yote. Rais Kikwete alimtosa kimyakimya ambapo kitendo hicho kilileta mtafaruku mkubwa ndani ya bunge kiasi kwamba ilibidi Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kuunda tume iliyokuwa inaongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya kutafuta chanzo cha uhasama na chuki baina ya wabunge wa CCM. Mengine ni historia.
Tukio hilo lilimfanya Rais Kikwete kutokuwa na mtu wa karibu zaidi mpaka mwisho wa utawala wake. Kwa maana nyingine, aliusoma vizuri mchezo mchafu wa wanaCCM.
Utawala wa Rais Magufuli pia umeanza kupitia njia ile ile ya utawala wa Rais Kikwete baada ya kuingia madarakani mwaka 2005.
Baada ya kugundua kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles Kitwanga ni mtu wa karibu sana na Rais Magufuli, wanasiasa waliunda kikundi kuhakikisha wanavuruga ukaribu wao. Madhaifu ya Charles Kitwanga yalitambulika kuwa ni mahusiano yake na Lugumi na pia ulevi wa 'kupindukia.
Kelele za mahusiano yake na Lugumi zilianza kupigwa kwa nguvu mpaka tume ya bunge ikaundwa ili kumsurubu kisiasa . Baada ya muda mahasimu wake waligundua kuwa Rais Magufuli hawezi kumwajibisha kwa sababu ya tuhuma za Lugumi kwa vile hazina uzito.
Wajanja wakatumia udhaifu mwingine wa ulevi wake kumsulubu kisiasa baada ya kumshawishi kunywa naye pombe mpaka alfajiri halafu wakamweleza Waziri Mkuu, Majaliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Charles Kitwanga ameingia bungeni huku amelewa. ‘’Mission accomplished’’ mengine ni historia.
Kwa sasa amejitokeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ambaye wanahisi pia anaaminiwa sana zaidi yao.
Wanasiasa wameunda kikundi ili kuhakikisha uhusiano huo unafutiliwa mbali kama ilivyokuwa kwa Charles Kitwanga.
Madhaifu ya Paul Makonda yametafutwa na kupatikana. Madhaifu hayo ni pamoja na utata wa vyeti vya shule/chuo, mali zake na utumiaji 'mbaya' wa madaraka ambapo anawashughulikia wabaya wake kwa kutumia vyombo vya dola.
Ieleweke kuwa waliomsulubu Kitwanga ndani ya CCM ndio walewale wanaomsulubu Paul Makonda huku wakisaidiwa na wanasiasa wa upinzani/UKAWA kwa sababu Makonda amewabana sana UKAWA kisiasa katika mkoa wa Dar es Salaam wakati kisheria wao ndio wanaongoza Jiji.
Baada ya hoja ya vyeti na mali kutokuzaa matunda mazuri kwa sasa wanasiasa wanapiga kelele kuhusu kuundwa tume ya bunge kuchunguza suala la TISS lakini mlengwa ni Paul Makonda. Amini ninakuambia kama Makonda akiondolewa leo hii kwenye Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hata hoja ya kufanya uchunguzi kuhusu TISS itakufa kama ilivyokufa hoja ya Lugumi baada ya Charles Kitwanga kuondolewa Uwaziri wa Mambo ya Ndani.
Je, Spika atamtosa Makonda na kuunda tume ya kuchunguza TISS wakati mlengwa mkuu ni Makonda kama Marehemu Sitta alivyomtosa Lowassa na kuunda tume ya bunge kuchunguza Richmond wakati mlengwa mkuu ni Lowassa.
Je, Rais Magufuli atamtosa Makonda kama alivyomtosa Kitwanga baada ya kuingia kwenye mtego wa ulevi.
Je, Rais Magufuli atadhihirisha kuwa yeye ni tofauti na Rais Kikwete ili kumkingia kifua Paul Makonda.
Je, Rais Magufuli atapata faida au hasara gani kisiasa kwa Paul Makonda kama atafukuzwa au kuendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Je, Rais Magufuli ana la kujifunza kutoka kwa Mzee Kikwete kuhusu hii mivutano inayotokea kwa sasa ndani ya CCM.