Yaliyokubaliwa kwenye mkutano wa Rais na TPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyokubaliwa kwenye mkutano wa Rais na TPA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 16, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Yafuatayo ni mambo ambayo yamekubaliwa kufanywa baada ya uongozi wa Mamlaka ya Bandari, Wizara ya Miundo Mbinu na Ikulu kukutana jana. Hebu tuyaangalie na tuamue ni yapi yalimhitaji Rais na yasingeweza kupendekezwa au kuamuliwa kufanya kwenye uongozi wa chini.

  (a) Kuitaka Kampuni ya Kupakia na Kupakua Makontena (TICTS) katika Bandari ya Dar es Salaam kutekeleza wajibu wake ipasavyo kwa mujibu wa mkataba wake kwa kuongeza ufanisi na kuboresha kiwango chake cha utendaji kwa lengo la kupunguza mlundikano wa meli katika Bandari ya Dar es Salaam.

  (b) Kuchukua hatua nyingine za kupunguza mlundikano wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kuchukua mfululizo wa hatua ikiwa ni pamoja na:


  (i) Kuhakikisha kuwa mizigo inaondolewa haraka kwa kadri inavyowezekana katika Bandari, kwa kutumia taratibu muhimu zilizopo, ikiwa ni pamoja na kontena kupigwa mnada baada ya kuwa zimekaa bandarini kwa siku 21 kwa mujibu wa sheria.

  (ii) Ili kutekeleza jambo hilo la kuhakikisha kuwa mizigo inaondolewa Bandari haraka, TPA na TRA zimeagizwa kuhakikisha kuwa zinapiga mnada kiasi cha asilimia 30 ya makontena yaliyokaa zaidi ya siku 21 katika bandari hiyo, kama njia ya haraka ya kupunguza mlundikano wa mizigo katika Bandari hiyo.

  (iii) Kuhakikisha kuwa kuanzia sasa kontena zote zinazopakuliwa kwenye meli, zinapelekwa moja kwa moja kwenye Vituo vya Kuhifadhi Kontena Nje ya Bandari (ICD’s) na gharama za zoezi hilo zinakuwa sehemu ya kutoa mizigo katika Bandari hiyo.

  (iv) Kuchukua hatua za kupunguza muda wa meli kusubiri pwani ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kuhakikisha kuwa upakiaji na upakuaji mizigo unaharakishwa kwa TICTS kununua vifaa zaidi na pia kuhakikisha kuwa vifaa vya TPA vinatumika.

  (v) Kuhakikisha kuwa maarifa yanatafutwa kuondoa magari yaliyoko Bandarini kwa sasa yakisubiri kuchukuliwa na wenyewe, ili kupatikane nafasi zaidi ndani ya eneo la Bandari hiyo kwa shughuli na mizigo mingine. Hili lifanyike kwa kutafuta eneo jingine nje ya Bandari kuhifadhi magari hayo.

  (vi) Kuharakisha zoezi zima la kuondoa mizigo Bandarini kwa nyaraka muhimu za kufanikisha jambo hilo kujazwa na kupitishwa haraka iwezekanavyo na TRA.

  (vii) Ili kufanikisha uharaka huo, TRA imeagizwa kuhakikisha kuwa sehemu ya kushughulikia nyaraka ya long-room inafanywa kuwa short-room kwa maofisa wa Mamlaka hayo kufanya kazi kwa saa 24, ikiwa ni pamoja na siku za Jumapili.

  (viii) Kuongeza ushirikiano wa utendaji miongoni mwa taasisi mbalimbali zinazohusika na kuondoa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, ili kuongeza ufanisi wa Bandari hiyo na kuiwezesha kupambana ipasavyo na ushindani kutoka kwa bandari nyingine katika eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika.

  (ix) Kuchukua hatua za kuboresha ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam kwa miaka ijayo, hasa baada ya ongezeko kubwa la mizigo litakalokuwa linapitia katika bandari hiyo baada ya Reli ya Kati kufanyiwa matengenezo makubwa ya kupanua geji yake.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.
   
 2. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  MMK sasa tufanye nini na rais ndo ameenda wameamua hivyo? tunaweza kubatilisha maamuzi yake/yao?
   
 3. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  maana ninachokiona kwenye hayo mambo yote uliyoyaainisha yangeweza kutekelewa na hao hao wahusikwa wa bandari/Ticts bila hata kuelekezwa na rasi, may be aliamua kwenda kuongezea msisitizo maana watu wengine wanaamka once wanapoona mkubwa wake amemuelekeza assignment fulani.
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Jan 16, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hayo makubaliano yaliyokuwa yameshaandaliwa au waliyaandaa pale p
   
 5. D

  DURU JIPYA Member

  #5
  Jan 16, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee wa Kijiji
  Yatatekelezeka? Ala kulli hali.....

  Huu ndio ufanisi tunaolilia. Ikiwezekana hapa, kupitia na kurekebisha fomu zote ikiwa pamoja na utumiaji wa teknolojia ya computer.

  Uchambuzi yakinifu unahitajika kupitia mfumo mzima wa nyaraka hizo.

  Kwa wale wenye kufanya uchambuzi wa mifumo, huu ni wakati wa kujitolea na kusaidia maeneo kama haya, siyo bandarini peke yake, bali hata kwenye Wizara mama.

  Kwa lugha nyingine pia wametoa ruhusa za fedha kutumiwa, kuhakikisha hayo juu yanatendeka, na sio kufikiria njia za kufisadi mwongozo huo.

  Vile vile upo uwezekano wa kuwa na ajira-This is a good thing

  Bravo Kikwete.
  Duru hili nipo na wewe.

  DJ
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hiyo part "a" mbona iko too vague!
   
 7. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Part A ni mkataba Nyambala huruhusiwi kuuona, Lakini tatizo kubwa ambalo hakugusia au kulitolea ukali ni part B- V, V1, na V11 hapo rushwa inanuka na ndipo chanzo cha mizigo kuchelewa, say mtu umeleta gari lako la mwaka 2001 na umejiandaa vizuri tu kulipia kama ulivyobajeti ghafla hao jamaa wanakukomalia kuwa seat belt ni ya 1999 hivyo wanataka ulipe makadirio ya juu zaidi wakati hujajitayarisha? au umeagiza remanufuctured or used engine ukitaraji kulipa kidogo jamaa wanadai ni engine mpya hapo ni lazima ukajipange upya wanamaudhi kweli kweli kwa kung'ang'aniza uwape chochote au wanakuumiza ili wapate sifa kuwa wamekusanya kodi kuvuka malengo yao, kwao mzigo kuchelewa si tatizo, ni bora kungekuwa na track check list ya kila mfanyakazi kuona utendaji wake, pia wanatakiwa waanzishe fastrack service kwa walionazo , yaani hapo mtu akikubabaisha basi ruksa kumuona Top boss fasta fasta nafikiri wataogopa kuzembea, ila sasa kupata Boss mwaminifu, mnyenyekevu na mchapa kazi hapa Tanzania ni sawa na Ndege kuanguaka abiria wote wakapona
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Halafu unajua nini mkuu Kite Munganga, cha kushangaza katika hili suala la kuclear mizigo ni karaha tupu uunaweza kupiga hiy mizunguko ya bndarini - Ilala - Posta kama mara 20 hv. Lakini vitu vyote vingekuwa kule port ingerahisisha mimi nimeona nchi zzingine ni kwmba kila kunapokuwa na masualla ya customs basi pembeni yaker kuna benki, sasa sijui bandari yetu kama kuna benki siku hz????
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Rais ni msimamizi mkuuwa shughuli zote za serikali nchini, hakuna ajabu yoyote kwa Rais kukagua na kutoa maagizo kwa idara za serikali. Tuache kudhani kuwa Rais anatakiwa atoe maamuzi ya ''kimungu'' ambayo binadamu wengine watashindwa kuyafikiria.
  Maamuzi haya mengi yake ni mazuri lakini bado sijaelewa kwanini TICTS inaendelea kukumbatiwa wakati imeshashindwa kutekeleza aricles za mkataba. Kwanini serikali isitangaze tenda ili kampuni nyingine zije kusaidiana na TICTS iwapo wao TICTS hawana vifaa vya kutosha???
  Uamuzi wa kupiga mnada mizigo iliyokaa hauko fair kwa wamiliki wa mizigo, uzoefu nilio nao ni kwamba mizigo inacheleshwa na utendaji wa bandari na si uzembe wa wamiliki. Sasa kwanini wamiliki wapewe hasara kwa mizigo yao kupigwa mnada, wakati wao wako tayari kuigomboa???
  Na kwanini serikali isikubaliane na reality kuwa bandari yetu ni ndogo kuliko mahitaji hivyo kuweka mkakati maridhawa wa kuipanua au kuboresha bandari mbadala kama ya Tanga?
  Maswali ni mengi sana katika sakata hili la bandari!!!
   
 10. J

  Jitume Senior Member

  #10
  Jan 17, 2009
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata ngazi za Mikoa, Halmashauri nk, hakuna mahamuzi wala utekelezaji makini.

  Wanangoja Rais atoe maelekezo hata yaliyo kwenye kanuni na sheria. Si wakitekeleza watajichonganisha kwa wenzao/washirika wao!

  Kitakachofuata ni Hatuna namna ni Rais kaelekeza!!!!!!
   
 11. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,660
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  Jamani, without prejudice, hivi Mh Rais ataendela kuwapeti peti hao watendaji hadi lini? I mean, sijaona hata moja lililomfanya afunge safari hadi pale.....la sivyo, watu watakuwa hawafanyi kazi hadi rais aje na akishaondoka mwendo mdundo!

  Nina imani kuwa hao watu wa TPA watakuwa 'wanapumua' manake zamu yao imepita....hivi waziri mzima naye akaguliwe? kwanini yuko pale in the first place? Rais angeweza kuwa ndo anaongoza wizara zote hizo, akishirikiana na makatibu wakuu,, kama ambavyo Malawi Rais anashikilia baadhi ya wizara yeye mwenyewe. tena hii ingepunguza kweli matumizi!
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Karibu yote aliyoyasema ndiyo yalipaswa kufanywa na taasisi hizo, ndio wajibuw ao wa msingi. Kwa rais kufikia hatua ya kusema hivyo, inamaana kuwa hayajafanyika. Kwa maana nyingine taasisi hizo zimeshindwa kazi. kama ndivyo hivyo, rais alipaswa kuwakumbusha wajibu wao au kuwawajibisha kwa kushindwa kuterkeleza wajibu wao?
   
 13. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2009
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu, kuna TISCAN-COTECNA, kabla hujatoa mzigo lazima IDF form zako zipitiwe na hawa jamaa upate kadirio la kodi ndio ulipe TRA utoe mzigo, sasa usumbufu wa hawa jamaa, sidhani kama kuna mtu anayeweza kutoa mzigo chini ya miezi miwili, msishangae huo mlundikano wa magari na container bandarini.
   
 14. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Suala la kupiga mnada mizigo bandarini sio rahisi kama ilivyoagizwa na Rais. Sheria ya Forodha inalinda kikamilifu suala hilo. Hizo siku 21 zinazozungumzwa ni ambazo Mamlaka ya Bandari inatakiwa kuijulisha TRA kuwa mzigo huu na huu tayari una siku 21. Kuorodhesha pekee kunaweza kuichukua TPA mwezi mzima. Halafu TRA intakiwa kutathmini mizigo hiyo na kuipangia bei (Reserve Price) kwa ajili ya kupigwa mnada. Hili pia laweza kuchukua mwezi mwingine. Hapo ndipo Kamishna wa Forodha anatangaza kwenye Magazeti kuwa mizigo hiyo isipochukuliwa kihalali ndani ya siku 30 ataipiga mnada. Kisheria lazima zipite siku 30 tangu siku ya tangazo na siku ya kupiga mnada. Kwa mantiki hiyo inaweza kupita miezi 3 tangu siku ya orodha kupelekwa TRA kutoka TPA mpaka kupigwa mnada. Na sidhani litakuwa suluhisho.
  Kwa utaratibu wa sasa wa TICTS inahamisha makontena yote yenye zaidi ya siku hizo 21 kwenda ICD Ubungo. Hayakai bandarini, lakini bado bandarini kuna msongamano.
   
Loading...