Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,856
WAZANZIBARI leo wanasherehekea miaka 52 ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964, ambayo yaling’oa utawala wa Sultani kutoka Oman na kuwezesha wazalendo wengi kushika hatamu ya kuongoza nchi.
Katika kilele cha sherehe hizi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein atahutubia taifa katika uwanja wa Amaan.
Matukio mengine makubwa yaliyofanyika katika uwanja huu ni Rais Shein kukagua gwaride la heshima la vikosi ya ulinzi na usalama, vikiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Amepokea maandamano ya wananchi wa mikoa mitano ya Unguja.
Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu na Viongozi wastaafu, Mzee Mwinyi, Benjamin Mkapa Aman Karume na Wengine Wengi wa Kitaifa, wamewasili uwanja wa Amani katika sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Z'bar.
Vilevile Mkuu wa Majeshi Mwamnyange amehudhulia. Viongozi wengi wa Kitaifa wamehudhulia.
Maalim Seif Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar amekwepa Sherehe hizi.
Hizi sherehe za mapinduzi leo zimepoa. Hii inadhiirisha tatizo kubwa la mkwamo wa kisiasa lilipo Zanzibar, Si kama miaka ya nyuma.
=========
Shein: Kwa upande wa Zanzibar, kama sote tunavyofahamu, tume ya uchaguzi ilifuta uchaguzi wa Zanzibar tarehe 28 October mwaka jana baada ya kubainika kutokea kasoro kadhaa kama zilivyoelezwa na tume ya uchaguzi ya Zanzibar. Kadhalika uamuzi huo wa tume ulitangazwa katika gazeti rasmi la serikali tarehe 6 November mwaka 2015 kwamba tume ya uchaguzi ya Zanzibar imeyafuta matokeo yote ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar na kwamba uamuzi wa tume kutangaza tarehe nyingine ya kurudia uchaguzi mkuu wa Zanzibar utatangazwa baadae.
Nawaomba wananchi waendelee kuishi kwa amani na waendelee kupendana huku tukisubiri tume ya uchaguzi ya Zanzibar itangaze tarehe nyingine ya kurudia uchaguzi wa Zanzibar. Kwa hio uchaguzi kwa mujibu wa katiba na sheria ya Zanzibar ya uchaguzi utarudiwa.
Kwa Hotuba kamili, Soma hapa chini.
HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHE. DK. ALI MOHAMED SHEIN, KATIKA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, AMAAN STADIUM TAREHE 12 JANUARI, 2016.