Yaliyojiri SAUT-Tawi la Tabora

Yaliyojiri SAUT-Tawi la Tabora

nexus white

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2011
Posts
210
Reaction score
81
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kusababisha watu kushangaa ni pale usalama wa taifa kutaka kufanya mambo yaliyoshindwa kuzuilika kwa wanachuo na wananchi wengine wa kawaida waliohudhuria mdahalo chuoni hapo. Na hii ni baada ya mgeni mwalikwa ambaye ni naibu waziri January Makamba kusema kwamba hoja katika mdahalo huo zitakuwa ni ni muundo wa serikali na hoja nyingine ni mambo yahusuyo sayansi na teknolojia

Ndipo wanachuo wakaanza kuongea kwa kutoa vielelezo thabiti ili kutetea hoja zao, ndipo mkuu wa mkoa Bi Fatuma Mwassa alipoona wanachuo wanatoa hoja za kupinga serikali mbili na zikiwa zimeshiba kwa uthibitisho wao na kwenda kinyume na matarajio yao(mkuu wa mkoa, usalama wa taifa na makamba) ikabidi watake kuwaongoza na ndipo vijana wakakataa na usalama wa taifa kutaka kuwakamata ambapo wanachuo walisema hakuna aliyefanya vurugu wala kutukana hivyo hakamatwi wala kuonewa mtu. Kwa busara za January Makamba ndipo hali ikatulia baada ya kusema hii ni demokrasia na kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake na hapo mkuu wa mkoa na usalama wakawa wapole

katika mdahalo huo pia walikuwepo TBC1 na TBC taifa lakini nashangaa kutokuitoa habari hii

MY TAKE: Huu mjadala wa katiba ni mjadala wa kitaifa hivyo viongozi acheni watu wazungumze ya moyoni cha muhimu wasivunje sheria tu, vyombo vya dola mpo kwa ajili ya usalama na si kuwafundisha watu waseme nini na pia TBC1 acheni kubagua habari

Nitasema kweli daima uongo kwangu mwiko

Nawasilisha

Source: Mimi mwenyewe nilihudhuria
 
Inawezekana kwa kuwa ni Tabora walidhani wahudhuliaji niwanyamwezi wa kule Igarula tu
 
Duhh ccm bado wanataka tufunike kombe mwanaharamu apite hapana aseeeh ni ngumu kwa karne hii
 
Nawapongeza sana wana SAUT.
Maneno ya Lisu yanatimia walizoea vya kunyonga vyakuchinja ni shida kwao. Komaeni na mwaka huu tutawatoa kamasi.
 
Wewe Ni mwehu

wewe mi kichaaa

Mh Fatma mwasah yuko dar Kikazi wiki mbili

hivvi Bavicha Gongo mtaamini lini kuwa inaharibu akili?

Ukichaa wako na mtambo wenu wa kutengeneza uongo utawaua.huu uzushi mpelekee mama yako na mkeo

Mods ondoeni huu uharo haraka sana
 
.mods huyu kichaa Ni mwongo nimeulizia Tabora hakuna upuuzi huo wala Mh Mwasa hakuwepo kulinda heshima ya Jukwaa lambisha,ban,kwa mnywa gongo,huyu
 
Vijana waamkia bar na kuzimua viroba mapema mapema hawa. Habari za umbea umbea tu
 
Wewe Ni mwehu

wewe mi kichaaa

Mh Fatma mwasah yuko dar Kikazi wiki mbili

hivvi Bavicha Gongo mtaamini lini kuwa inaharibu akili?

Ukichaa wako na mtambo wenu wa kutengeneza uongo utawaua.huu uzushi mpelekee mama yako na mkeo

Mods ondoeni huu uharo haraka sana
Cc.
mods , kwa hatua zenu stahiki kwa mleta mada ya uongo
 
.mods huyu kichaa Ni mwongo nimeulizia Tabora hakuna upuuzi huo wala Mh Mwasa hakuwepo kulinda heshima ya Jukwaa lambisha,ban,kwa mnywa gongo,huyu

Wewe ndiyo hujielewi. Huo ndiyo ukweli ccm hamkubaliki kwa watu wenye ufahamu na elimu,kijijini huko ndiyo mnatumia ujinga wao kuwahadaa. Huyo mama alikuwepo kwenye mdaharo huo na wote waliyotajwa na hayo aliyoyaandika mtoa maada ni ukweli asilimia 100% maana nilihudhuria.
 
Tanganyika ni nchi ya ahadi kwa watanganyika,iachwe ije,kuizuia kwa kuwatumia psychomotors haitasaidia
 
Nasikia Rage aliambiwa live kuwa ni mwongo,na alipozidiwa hoja na wanafunzi akaanza kuleta mambo ya simba akazomewa.

Si SAUT-TABORA tu waliokuwepo bali na TEKU,CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA,VETA,TTC na watu wengine wengi.
 
Wewe Ni mwehu

wewe mi kichaaa

Mh Fatma mwasah yuko dar Kikazi wiki mbili

hivvi Bavicha Gongo mtaamini lini kuwa inaharibu akili?

Ukichaa wako na mtambo wenu wa kutengeneza uongo utawaua.huu uzushi mpelekee mama yako na mkeo

Mods ondoeni huu uharo haraka sana

jazba ya nini sasa??
 
Tulia wewe hapa ni Tanganyika kwanza..
 
.mods huyu kichaa Ni mwongo nimeulizia Tabora hakuna upuuzi huo wala Mh Mwasa hakuwepo kulinda heshima ya Jukwaa lambisha,ban,kwa mnywa gongo,huyu

Wacha kujipendekeza kwa mods wewe,jadili mada iliyopo.
Serikali mbili haiuziki kwa jamii ya waelewa wewe.
Mods yenyewe serikali tatu sasa tafuta mahala pengine pa kulilia.
 
safi sna walifikiri wapo kalenga na chalinze.hamkubaliki kw wasomi hata siku moja.kaz yenu n kuwahonga tishrt na kofia wasiojielewa
 
kwa hao wanaobisha wawaulie hao mabosi wao kuwa jumamosi 3/5/2014 walikuwa wapi na akina nani na wanajadili nini..........hata ukitumwa wakati mwingine ishia njiani si lazima ufike
 
Back
Top Bottom