Yaliyojiri Mkutano wa UKAWA na Wahariri, Makao Makuu ya CUF

Binafsi ni mwanachama wa chadema nakwa hili bado sijaamini,mpaka niskie kauli toka kwa Edo mwenyewe.

Pia nina wasiwasi kama kweli amejiunga na ukawa bhasi kwa muda sitajishungulisha name siasa,nikiwa na maana sitakiunga chama changu kwenye shughuli zake zote.maana huu utakuwa undumilakuwili au kuuma na kupuliza.

Naamini kuja kwa Edo ukawa kuna hali ya hatari katika uchaguzi huu,hii inatokana na hali tuliyoiona kwenye harakati za kutafuta mgombea kupitia ccm.

Naomba niwakumbushe kidogo,kulikuwa na makundi mawili hasimpu.kundi la EDO na Membe kumbuka pia membe anauhusiano gani na JK.

Pia kumbuka pia uhusiano uliokuwepo kati ya JK na EDO miaka 10iliyopita.ona usaliti uliokuja to kea,kati ya mafahari watatu waliokuwa kama ndugu ambao ni Aziz,Edo na JK.

Sasa anza kufanya tathmini.

Kuja kwa Edo ukawa kuna Hali ya hatari ndani ya nchi yet.

Jiulize kwa nini nasema hii.

1. Kushinda kwa ukawa ni kushindwa kwa team membe. Najua unalijua hilooo,anza kuchanganua mwenyewe.

Je unadhani team membe watakubali?
Je wasipo kubali watachukua hatua gani?

Tanzania jiulize nini kitatokea baada ya hapo.

2.kwa upande wa pili kushinda kwa ccm kushindwa kwa team lowasa.

Je unafikiri Edo atakuwa tayari kushindwa kwa Mara ya pili?.

Je unafikiri Edo anawadha nini kwa kile anachoamini kuwa rafiki yake kipenzi amemsaliti?.

Hakika mwaka huu tutaona na kusikia mengi,Ila watanzania tukumbuke kinachoendelea humo wanavijua wakubwa wenyewe na wanajuana.hvyo wasije wakayufanya na sisi tukavurugana kwa faida ya matumbo yao wao na familia zao.

Tuendelee kusikia na kuona,ila hali ya hatari imeanza kunukia nchini kwetu.

MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Hapana hatuna mwanachama kama wewe wala hatujawahi kuwa nae acha kutupakazia mauongo yako sisi ptuuuuuuuuuuu.
 
Yaani ukawa wametuangusha sana kwa uamuzi huu,Kumkaribisha El sijui niite kuchanganyikiwa au vipi?Maana ina maana kuwa ukawa hakukua na mtu mwenye sifa za kugombea nafasi ya rais?hizi siasa za tanzania mbona za kisanii hivi?kwahiyo hata huyu El kama atakua rais ni kweli atakua rais bora kwa watanzania?El nae amebadilika ndabi ya wiki mbili tu hivi kweli rais huyu hatayumbishwa na kuyumbisha nchi?hasa ukizingatia na yalotokea nyuma pamoja na makundi yalojengeka ndani ya chama chake,je tujiandae sasa kua na makundi ndani ya serikali?na watu wa ukawa mbona sasa ni kama mmeacha msimamo wenu na kasi yenu nyie kama nyie?kweli nimeamini siasa ni game chafu,ingawa el ana kundi kubwa lkn utulivu wake unatia shaka
 
Msiamini Mwanasiasa yeyote hata kama ni wa Upinzani -Zitto Kabwe, kila siku tunaambiwa tuwe tunaweka akiba ya Maneno tunakataa Lowassa na wanamtandao wote Falsafa yao ni kuongelea utendaji na kutozungumzia Kabisa Ufisadi, Chadema Falsafa yao kubwa ni kupinga Ufisadi na Mafisadi, najaribu kuangalia nguvu ipi itaimeza ipi! Jambo moja kubwa nakiri Mbowe ni Mfanyabiashara Mkubwa na ni Risk taker kweli kweli
 
Nashindwa kuwaelewa UKAWA katika hili....Mtu ambaye mlikuwa mnatuaminisha wananchi kuwa ni fisadi na hafai kuwa kiongozi wa umma....leo hii anakaribishwaje kwenye chama....kwa kweli nimepata ukakasi katika hili na nimebaki njia panda....hata sijui nielekee wapi...
 
Acha kutukuza mawazo ya marehemu wewe....Machiavelli ndo nani bwana! Mtu alishafariki miaka na wewe unataka mawazo ya marehemu ndio yatumike hapa? No!!!! Tunatumia mawazo hai ya watu walio hai.....

Malyenge;
Kweli kuna vitu hata kuviwaza inakuwa shida. Najaribu kukuwaza kuwa weye ni mtu sampuli gani wala hionekani. Hivi huyu aliye mnukuu Machiavelli umeona ana imani na marehemu, lakini wanaomnukuu Baba wa Taifa lako unaona wao ni safii, La haullaa laa kwat! Dah! Pole sana, hatufiki hivi
 
Kwa mbali naanza kushashika endelea tu mkuu nadhani kufika 25 Oct nitakuwa nimeelewa vizuri na kura yangu itaenda ukawa kwa El
 
Kamanda kwa faida ya wanaukumbi hapa JF unaweza kutuambia kwa nini Dr.Slaa alimuita Lowassa Fisadi?

Mbona wewe unalialia? Shukuru Mungu fisadi aliyetaka kukiua chama kwa ufisadi ameondoka... Umeacha mke kisa jirani kasema Malaya.. Jirani kamchukua unalialia
 
Magufuli ndiyo chaguo sahihi by far. UKAWA hawaaminiki itatokea yale ya Kibaki na Raila Kenya. Serikali ya nusu mkate.
 
Wana jf. Naleta masikitiko yangu makubwa baada ya tukio la leo la huyu fisadi kukaribishwa ukawa. Bado siamini macho yangu ni hawa hawa viongozi wa ukawa ambao kwa miaka yote wamekuwa wakitupigia kelele majukwaani kupinga maufisadi yote yanayoendelea Leo hii yote hayo wameyaweka matakoni.

Loooh! Kweli pesa ni mwanaharamu kwa sababu haiwezi kuwa bure bure tu. Maneno yanayosemwa kuwa bw. Mbowe na group lake wamekula mlungula naweza sasa kuyaamini. Lakini sitaki kuamini kwamba hata Dr Slaa naye kaingizwa kingi. Mama yangu weeeee. Nilikuwa pia walau nina imani na Prof Lipumba lakini leo nimekudharau kupindukia. Kweli unasema mzee siyo eti wanamsingizia ?????? Eti miaka mingi ishapita toka mwaka 2008. Nawewe dr Slaa list of shame yako umeiweka sandukuni au umeichoma moto ???

Basi sasa natangaza kuwa chadema ni CCM B na sio kama tulivyokua tunaaminishwa na viongozi wa chadema kuhusu CUF na ACT. Kumbe chadema ndio wanaowaongoza. Sitaki kuamini lakini ndio ukweli sasa hakuna namna.

What next sasa adhabu kubwa tunayokwenda kuwapa ukawa sasa mtajuta maisha yenu yote. Ikulu mtaionaga ndotoni na sio vinginevyo. Asalaaam aleikhum ! Takbih !!!
 
Dr Slaa amezungumza mara kadhaa kuwa ana ushahidi kuhusiana na maufisadi ya Lowasa. Tunaomba utueleze yote hayo ukiyakabidhi mahakamani au polisi au uliamua kufungia sandukuni. Na kama ulifungia sandukuni je una mpango gani wa kuyatoa ili yaje yawe na manufaa kwa Taifa. Naomba usituletee mambo yako binafsi na laiti kama umepewa mlungura tayari basi ni bora ukajitojeza hadharani utubu ili tukusamehe,. Vinginevyo labda sasa tukushtaki wewe kwa uongo wa kuaminiwa
 
Nadhani mmekuwa mkihangaikia sana Taifa hili kwa dhati kabisa na kujaribu kuteka mioyo ya wafuasi wengi. Lakini naona uvumilivu wenu hapa umefikia kikomo mkaamua kuukumbatia ufisadi sasa kiasi cha kudiriki kugeuza fikra sahihi za mageuzi yanayoendelea. Kwamba fisadi siyo mtu ni mfumo. Hivi mfumo unajiendesha wenyewe. Msitake kutuaminisha kuwa ndani ya ccm hakuna wazuri na waliotukuka katika utumishi. Ndio maana wale ambao siyo wasafi wamatolewa na kuchukuliwa hatua au wanajiuzulu.
Nimeamini kuwa hakuna msafi duniani. Sielewi tu nyinyi viongozi mlikuwa mnatudanganya vipi katika kuchochea mabadiliko. Kweli kabisa mmeanza na nyinyi kukumbatia ufisadi. Astakhafulilah... !!
 
Back
Top Bottom