Yaliyojiri, Mgomo wa Madereva wa Mabasi nchini - Aprili 10, 2015

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,203
5,043
Leo, Madereva wa Vyombo mbalimbali vya Usafiri na hasa Mabasi na yale yafanyayo safari za ndani ya miji (maarufu kama Daladala) wamegoma na kupelekea usumbufu mkubwa kwa wananchi waliokuwa na safari mbalimbali.

Fuatilia thread hii ili kupata updates za kinachojiri...

===== Updates =====



Mgomo ulioanza rasmi leo asubuhi baada ya madereva kuwa na malalamiko, umeisha baada ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, kufuta Agizo la Madereva kusoma upya katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)
.
Mgomo wa Madereva wazimwa na Waziri Kabaka



Kituo cha mabasi Ubungo


Juu hapo ni Kituo cha Mabasi - Nyegezi, Mwanza


Hapa ni Mbezi, Mabasi ya UDA Yalikuja kutoa msaada lakini yamezuiliwa kupakia abiria hivyo milango imefungwa.

=> Mtwara Magari hayakutoka kwenda Dar kwasababu hawajui hatma ya huko Dar ila walikuwa tayari kusafieisha abiria, daladala na magari ya wilayani hakuna.

=> Kuna magari yamezuiwa Chalinze, wamepewa taarifa kuwa waliotangulia mbele Chalinze wamepigwa mawe.

=> Hapa stendi ya Njombe mabasi hayajaondoka mpaka muda huu.

=> Kuna zaidi ya mabasi zaidi ya 15 kutoka kanda ya ziwa, yamezuiwa/yamekwama Wilaya ya Kibaha, wamepewa taarifa kuwa waliotangulia mbele ya Chalinze wamepigwa mawe. Wanahofia Vurugu zinazo endelea Dar es Salaam

=> Hapa Tabora, mabasi ya kwenda mikoani mpaka sasa abiria hawajui mustakabali wa safari

=> Hapa Mbagala Rangi 3, kuna baadhi ya daladala zimeamua kuendelea kuchukua abiria lkn zinavamiwa na madereva wanaoshinikiza mgomo. Wanawashusha abiria toka kwenye daladala


Niko kituoni hapa mitaa ya Segerea, hakuna gari hata moja abiria tumeduwaa kituoni! Jinsi ya kufika kibaruani haieleweki! Je, huko ulipo hali ikoje?



Abiria wana pata shida ya ajabu Morogoro, bodaboda ndio zinatoa msaada ila kwa wale wenye uwezo. Wale wenzangu na mie wapo vutuoni hawana lile wala hili, sijui migomo hii ni mpaka lini, Abood Ndio Wakati Wako Wakutoa Msaada Sasa Sio Kwenye Kuzika Tu.

Hali ni tete kwa usafiri leo DSM!! Imenibidi nichukue bajaji toka simu 2OOO/Sinza mpaka maeneo ya posta!!
Hali ni mbaya

Wakuu hadi saa hizi hakuna basi hata moja lililoondoka kwenda mikoani kutokea hapa Kahama.

View attachment 241880

View attachment 241881

View attachment 241882
 

Attachments

  • ubungo8.JPG
    49.9 KB · Views: 18,782
  • ubungo7.JPG
    56.8 KB · Views: 18,503
Hata mimi nimeona morogoro road nyeupe road hakuna daladala no foleni, ila vituoni watu wengi sana, huu mgomo upo kimtindo
 
Boko huku tunateleza tu cjui watakaofuata huko kama watakutana na mgomo lakini tayar nmesikia konda anazungumzia hilo swala
 
twafwa migomo,migomo,migomo,migomo,migomo migomo migomo migomo migomo migomo migomo maana jana maduka yalifungwa huwi
 
Mi nilisoma alama za nyakati tangu juzi so niliwahi kuamka nikakuta daladala zinazotafuta pesa ya kula then zikapaki, sasa niko ofisini kwa raha zangu.

Ccm hoyeeeeeeeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…