Yaliyojiri matokeo ya Mbunge jimbo la Buyungu na uchaguzi wa madiwani kata 36 Tanzania bara

Habari wakuu, leo ni uchaguzi wa mbunge wa Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma na uchaguzi wa madiwani kata 79 Tanzania Bara. Katika uchaguzi wa mbunge jimbo la Buyungu kuna upinzani mkubwa sana kati ya mgombea kutoka CCM na CHADEMA.

=====

Fuatili kinachojiri hapa;
View attachment 834231
View attachment 834229
Mgombea wa CCM Christopher Kajoro Chiza, Kashinda Ubunge Jimbo la Buyungu (Kakonko),

BUYUNGU, KIGOMA: Zoezi la kuhesabu na kujumlisha kura kutoka vituo mbalimbali lamalizika saa 11:12 alfajiri ya leo

> Chiza C Kajoro wa CCM ameibuka mshindi kwa kupata kura 24,578 huku Elia F. Michael wa CHADEMA akipata kura 16,910. CCM 58% CHADEMA 40% others 2%

Update kutoka Arusha
Chadema wajitoa katika uchaguzi kata ya Songoro, Arusha baada ya mgombea wao na mawakala kupigwa. Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amethibitisha

MATOKEO
> Omari Mzee(CCM) ametangazwa mshindi udiwani kata ya Makorora, Jijini Tanga

> Juma Ramadhani(CCM) ametangazwa mshindi kata ya Mabokweni, jijini Tanga

> Alex Mwinuka(CCM) ametangazwa mshindi udiwani Kata ya Mwanganyanga, wilayani Kyela, Mbeya,baada ya kupata kura 867

> Emilian Siwingwa(CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa Udiwani katika Kata ya Mpona, Wilayani Songwe

> Apaikunda Naburi(CCM) ametangazwa kuwa mshindi katika Kata ya Mawenzi, Wilayani Moshi baada ya kupata kura 400 kati ya 569

> MATOKEO YA UDIWANI TARIME: Mgombea wa CCM Chacha Ghati ametangazwa mshindi wa udiwani kata ya Turwa Wilaya ya Tarime mkoani Mara baada ya kuibuka kidedea kwa kupata kura 1401 dhidi ya mgombea wa CHADEMA Charles Mnanka aliyepata kura 1121.
View attachment 834226
Pichani ni Agai, Gerald Mwita Martine na Emily Solo, wakiwa wameshikilia hati ya ushindi ya udiwani kata ya Turwa

View attachment 833576
Zoezi la upigaji kura likiwa linaendelea jimbo la Buyungu


View attachment 833604
Mgombea wa udiwani Kata ya Kaloleni(Arusha) kupitia CHADEMA akiwa amelazwa baada ya kupigwa vibaya
View attachment 833606
Yaani wapinzani waache waendelee na kupinga , ila Ukweli wanaujua. Wamepoteana hawajui watakutania wapi.
Eti mtu akishindwa kutafuta huruma eti kaibiwa kura. Shame on them
 
Endelea kujifariji mkuu!!
Yaani tupo ulingoni mimi na wewe, nimefungwa mikono na miguu, marefa umetoka nao kwenu, unashindwa kumaliza pambano kwa knock out kwenye round ya kwanza! Unapelekana na mimi mpaka ya 12 na unashinda kwa point chache! Je nikiachwa bila kufungwa na marefa usije nao itakuwaje.

CCM bila poliCCM na NEC hawawawezi CHADEMA hata kidogo. Pamoja na kununua wapinzani nchi nzima lakini bado hujaweza kuwafanya watanzania waipende CCM.
 
Lengo la chadema ni kuonyesha dunia yanayotendwa Tanzania

Pamoja na kuionyesha Dunia yanayotendewa Chadema...haya maumivu, vifo, ulemavu, majeraha nk wanaoupata wapinzani tunatakiwa tutumie ufahamu pia. Tungeachana na hizi chaguzi HATARI na badala yake tu-focus kwenye katiba mpya na tume huru !!!!!
 
Pamoja na kuionyesha Dunia yayotendwa Tanzania...haya maumivu, vifo, ulemavu, majeraha nk wanaoupata wapinzani tunatakiwa tutumie ufahamu pia. Tungeachana na hizi chaguzi HATARI na badala yake tu-focus kwenye katiba mpya na tume huru !!!!!
Mkuu Sahau kuhusu katiba mpya hivi unajua kuwa huko ikulu Leo wameteuliwa wasimamizi wakuu wengine wa Uchaguzi? Ukigusa katiba ujue unagusa Ugali wa watu
 
Dunia yenyewe ina huo mda? Kibaya zaidi hao wanaochaguliwa baada ya hizo sekeseke wanajiuzulu kirahisi kwenda kuunga juhudi. Sasa hivi tunaendesha kampeni za kutokupiga kura. Maana sisi wengine hata utushikie mtutu hatuwezi kuipigia kura ccm na hao cdm tunaowapa kura wanahongwa kirahisi.

Kabisa Mkuu.....
 
Mkuu Sahau kuhusu katiba mpya hivi unajua kuwa huko ikulu Leo wameteuliwa wasimamizi wakuu wengine wa Uchaguzi? Ukigusa katiba ujue unagusa Ugali wa watu

Nadhani ni hekima kuitafuta hata kama itachukua muda kuliko hizi vita vya wenyewe kwa wenyewe tunapambana hakuna demokrasia....ni heri kwenda kupata vipimo zaidi vya maradhi tunayougua kuliko kuendelea kumeza panadol kupooza maumivu.....
 
Mkuu Sahau kuhusu katiba mpya hivi unajua kuwa huko ikulu Leo wameteuliwa wasimamizi wakuu wengine wa Uchaguzi? Ukigusa katiba ujue unagusa Ugali wa watu
Katiba mpya mkuu mpaka kafara ya watu itolewe barabarani, hakuna namna, kwa maneno matupu hata miaka1000 mtaisikia kwa jirani zenu Kenya tu
 
Katiba mpya mkuu mpaka kafara ya watu itolewe barabarani, hakuna namna, kwa maneno matupu hata miaka1000 mtaisikia kwa jirani zenu Kenya tu

Nadhani kuliko kuwaumiza wananchi kwa ajili ya hizi chaguzi za kihuni ni heri tuingie mitaani kuitafuta katiba.
 
Tanzania mpaka Yesu aje ndipo tutapata akili vizuri cjui kwa kweli Mungu anajua tunakopita
 
Back
Top Bottom