Yaliyojiri, Matokeo ya maeneo yaliyorudia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 21 Disemba, 2014

Matokeo yametoka muda si mrefu hapa kata ya liwiti mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa s/mtaa kwa ukawa kupitia cdm amepata kura 290 dhidi ya 279 za ccm.wajumbe wote ni ccm, viti maalum cdm.hata hivyo cha kuhuzunisha sana ni mgombea wa nccr kushawishiwa na ccm kugombea hali akijua kuna makubaliano ya ukawa kusimamisha kwa pamoja na hivyo kupunguza kura za ukawa.
Mfano kura za m/kiti 24 zimeharibika baada ya wananchi kupigia kura kwa ku-tick sehemu 2 yaani ya mgombea wa cdm na nccr wakidhani kwa kufanya hivyo wanapigia muungano wa ukawa.hata kura za wajumbe wa ukawa zimepungua kwa sababu hiyohiyo, kwa sababu wote wameshindwa kwa kura chachechache sn.laiti kama wagombea wa nccr wasingekuwepo nao wengepita pia.

Mitaa mingine ukawa walioshinda m/kiti na wajumbe wake wote ni mtaa wa amani kupitia cdm na mfaume kupitia cuf. Mtaa wa msewe nafasi ya m/kiti ccm wameshinda kwa tofauti ya kura 11, na wajumbe wote ni ccm,
 
Nimetoka Sinza nikapita maeneo ya Buguruni na Tabata na sasa na mimi niko hapa Kwetu Pazuri Segerea. Naona Ukawa mmefanya vizuri jimbo la Segerea lakini bado CCM wako juu sana jimbo hilo. Kwa mujibu wa matokeo niliyokusanya mpaka mwisho saa 6 usiku huu kati ya mitaa yote 60 ya jimbo la Segerea matokeo ni kama ifuatavyo:

CDM 12
CUF. 13
CCM. 35
 
Safi sana tuwamwage tuwamwage ooooo mafisadi tuwamwage

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Dar na Pwani bado hawajanifurahisha... bado wanafurahia kula Ngwara za kuku!!! Wanafurahia maji ya chooni maana visima vyote vinamchanga !!! Dar wanamatatizo sana lakini hawajaamka hawajielewi kuwa CCM ndo yenye kuwapa mateso yote haya! Hawatambui kuwa kuna uwezekano wa kufanya fumigation na kutokomeza Mbu badala ya kuwaua kwa Vyandarua vyenye Sumu ...
 
Huku mwanza mtaa wa ibungiro chadema wameshinda cha ajabu wametangaza matokeo uchaguzi ukiwa unaendelea et CCM wameshinda watu hawajakubali cjui utaludiwa tena

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
utabiri wangu wa ccm kufa mlalo wa chali kifo cha mende asante Mungu limetia hii inaonyesha kiasi gani wananchi hawana imani na ccm
 
Mjini Kigoma Mtaa wa Ujiji Rubuga ambao Jumapili iliyopita ACT ilifungana kura na CCM na hivyo kusababisha uchaguzi huo kurudiwa leo kati ya vyama viwili (ACT na CCM), kura zimeshahesabiwa na ACT imeshinda kwa kishindo. Mjini Kasulu kati ya mitaa 5 ambayo matokeo yake tayari yameshatangazwa, ACT - 2, CCM - 3, CHADEMA - 0, NCCR - 0 na CUF - 0. Kata ya Usinge wilayani Kaliua Mkoani Tabora, kijiji cha Mabaha kati ya vitongoji 7 ACT tumeshinda vitongoji 5 na tumeshinda pia mwenyekiti wa kijiji hicho na wajumbe wa serikali ya kijiji.

ACT n CCM hawana tofauti ni wahuni na wezi wa pesa pesa inaonekana wananchi wa huko hawana uchungu na ccm kwa sababu mgao wa pesa za escrow umefikia watajuta baadaye
 
murufiti, ipo mamlaka ya mji kasulu:-
1. ukawa=03
2. ccm 02
3. mtaa mmoja haujafanya. kuna pingamizi lkn ukawa wana matumaini makubwa.

wajumbe kwa mitaa yote wamekuwa ni ukawa isipokuwa mjumbe mmoja ndo ccm.
 
Back
Top Bottom