Yaliyojiri Kutoka Ufipa: Mkutano wa CHADEMA na waandishi wa habari, maandamano ya UKUTA yaahirishwa

CDM mbona waoga hivo ! JWTZ wamesema wanafanya usafi tu…! Nyie andamaneni haina shida
 
Kwa hiyo gharama kubwa sana jeshi la polisi na JWTZ wameingia CHADEMA watalipa..?

Gharama za mafuta ya gari na ndege, nchi nzima CHADEMA italipa.?

Pressure nchi nzima CHADEMA watalipa..?

Nitarudi..!!
 
Unaona sasa agenda zenu zilivyo za kip.mbavu! Yaani lengo lenu kukwamisha maendeleo ya mtu aliyechaguliwa kihalali!!!! Uzuri JPM huwa anapitapita hii mitaa na ndo anazidi kujua anadeal na wapinzani wa aina gani. Atawakong'ota sana nyang'au nyie!
Ha ha ha acha kupanic maendeleo mnayakwamisha wenyewe .hivi kuzuia watu wasifanye siasa unaona ni sawa? Serikali inatumia gharama kubwa kuandaa majeshi kukabiliana na upinzania badala ya kufanya kazi za maendeleo ndo sawa hiyo? Na mkija kushtuka 2020 hii hapa msifikiri wananchi wajinga hakuna atakaewaelewa watu watauliza tuliwatuma mkajenge viwanda au kuwakamata wapinzani? Shtuka mapema chukua hatua.
 
Chama pekee kisicho na longo longo kinapoamua kufanya maandamano pasi na kuhofia polisi ni CUF
Hahaha,aisee hawa CUF achana nao,wakisema huwa hakuna mjadala,na huwa hawabahatishi.

Nawajua vizurii,na ndio maana huwa wapo makini saana kuhamasisha maandamano,maana hawataki kukurupa,na walijua kabisa kwamba UKUTA hautakiwa na jipya zaidi ya kuachia,wakaona wakae kimyaa waone jinsi watoto wanavyocheza ngoma ya kitoto.
CUF show nyingine kabisa wakitaka kufanya maandamano
 
Ingenja [HASHTAG]#506[/HASHTAG]......Wimbo huo ni ujumbe mzito sana si tu kwa Watawala wa nchi zetu za Afrika lakini pia kwa sisi Watawaliwa. Mkoloni alishaondoka zamani, lakini huo uhuru mbona bado hatuna? Hayo maendeleo mbona hatuyaoni?

Ni wimbo mzuri na muafaka kwa zama hizi tunazoishi.
 
Ha ha ha acha kupanic maendeleo mnayakwamisha wenyewe .hivi kuzuia watu wasifanye siasa unaona ni sawa? Serikali inatumia gharama kubwa kuandaa majeshi kukabiliana na upinzania badala ya kufanya kazi za maendeleo ndo sawa hiyo? Na mkija kushtuka 2020 hii hapa msifikiri wananchi wajinga hakuna atakaewaelewa watu watauliza tuliwatuma mkajenge viwanda au kuwakamata wapinzani? Shtuka mapema chukua hatua.
Aisee kweli mnajifariji Ujinga.
Hembu hizi gharama mnazo sema wekeni hapa tujue ni gharama gani.Au jipya lipi ambalo jeshi huwa hawalifanyi.Au huwa hamuoni mafunzo yao nini.Mmekulia wapi msipoona mafunzo ya kijeshi.
Budget ya jeshi ipo pale pale,na hata hao Chagadema wanalipa kodi vile vile.

CCM haitumii nguvu kubwa kukabiliana na Upinzani,maana kuna watu wadogo tu wanafanyakazi hiyo,na kubwa zaidi ni kwamba nyie kwa nyie mnaisaidia CCM huku mkijua ila mnajitoa faham.
2020,wengi mmeishakuwa vizee ndio mtapigwa vibaya mno,maana hakuna jipya kwa Chadema
VIVA Zitto Kabwe kwa kusoma alama za Nyakati
 
Kuna dhana mpya imejitokeza hasa kwa Mbowe,Lowassa, Mbatia na Wenzao wanapanga mipango halafu inapoonekana kuwa imeshindwa wanakuja kwa waandishi wa habari na kuhadaa umma eti viongozi wa dini wamewashauri waache.

Mbatia alikuja na tangazo kuwa wameamua kurejea bungeni kwa ushauri wa viongozi wa dini licha ya kuapa kuandamana mfululizo..

Mbowe naye leo kaahirisha ukuta eti kwa ushauri wa viongozi wa dini,licha ya kuapa kutohudhuria bungeni.

Ni viongozi gani hao ambao wao wanawaheshimu sana.
 
Chadema wamekula pesa ya Sementi na matofali..... UKUTA haujengwi tena.
 
1472653469315.jpg
 
Hatimaye wale mabingwa wa uongo na unafiki chadema wameogopa dola na kuamua kuwadanganya wafuasi wao wasio tumia akili na kuwaambia eti kesho hakuna maandamano. Sasa vichwa vya habari kesho itakuwa:
  1. Ukuta wanywea kimya kimya
  2. Mbowe aogopa polisi
  3. Viongozi UKUTA wajisalimisha polisi
Chezea dola wewe, wananchi tunamuunga mkono rais kwa asilimia 100%. Aendelee na kupambana na wala rushwa, mafisadi na wazembe.
mkuu unatamani sana uharibifu ukitokea? unaweza usiandamane lakini matokeo ya vurugu hizo zikakufuata sebuleni kwako. ni uamzi wa kupongezwa hasa kwa sisi tunao ombea amani ya nchi hii
 
Back
Top Bottom