Yaliyojiri Jijini Arusha: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dk. Magufuli – Oktoba 6, 2015

Una uhakika hizi picha ni za tukio la jana?

wewe unadhani za wapi hapo ndo Arusha wamewapa robo uwanja what i mean kusini na kusini mashariki na kaskazini mashariki mwa uwanja ila the rest palikuwa hakuna watu
 
Moja ya masharti ya hizi ID za kimkakati nikupinga tu!! Mnakuwa mbumbumbu mpaka mnakuwa kama mazombie vile, hizo bus zisombe watu toka Dar nyinyi ukawa msione wala msipige picha hata moja na tecno zenu?

Usifuate mkumbo fuata uhalisi wa jambo. Ukihitaji ufafanuzi omba msaada. Ndivyo waungwana tuishivyo.
 
wewe unadhani za wapi hapo ndo Arusha wamewapa robo uwanja what i mean kusini na kusini mashariki na kaskazini mashariki mwa uwanja ila the rest palikuwa hakuna watu
Yes, CCM ilishakufa Jijini Arusha!

attachment.php
 
A,to Z.walisombwa wote wakafunga kampuni kumsindikiza makufuli je!kura watalazimishwa???
 
Hizo hadithi zako na ndoto za alinacha, za kubeba watu kwa fuso na kuwashushia uwanjani bila aibu, kufunga viwanda vya A-Z na Sunflag na kuwavisha wafanyakazi t-shirt na kuwalazimisha waende uwanjani kwa kuwapa elf kumi kumi , kubeba watu toka longido na vijijini ili kujiliwaza, tar 25 ndo utaijua Arusha sio ya kuchezea. Dream on lofa...

It's OK, let's wait and see. Lakini nakuomba sana tarehe 26 October usikimbie humu JF, nakusubiri kwa hoja mkuu.
 
A,to Z.walisombwa wote wakafunga kampuni kumsindikiza makufuli je!kura watalazimishwa???

Hizo ni propaganda za kisiasa tu ndugu, ukweli utajitenga muda sio mrefu ndugu, zimebakia siku 17tu Watanzania kuamua. Sasa tusubiri tuone, mimi ninachokuomba kuanzia tarehe 26 October tukutane hapa JF tujadili matokeo kwa hoja. Kikubwa mtakachokuja nacho hapa ni wimbo ule, ule wa miaka yote wa kusema "tumeibiwa kura" Nakuomba sana wewe na wenzako UKIWA mjiandae kisaikolojia.
 
Yes, CCM ilishakufa Jijini Arusha!

attachment.php


Matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yatawashangaza wengi sana, Ikulu haichukuliwi "kimaigizo". Arusha inarudi mikononi mw CCM na hamtaamini masikio yenu. Mjiandae kisaikolojia, kuna maisha baada ya uchaguzi. #HapaKaziTu
 
Kuhusu swala la arusha kurudi ccm ni ngumu sana
Ila kwakua bdo kuna siku kadhaa mbele ngoja tuone
Ila mona ban mikutano yake
Nmehudhuria mara 3 anazidiwa hata na Ally Bananga
 
Mgombea waCCM, Magufuli amendelea na zaira za kuomba kura katika mikoa ya Arusha na Kilmanjaro ambapo ameweza kuvunja ngome za CHADEMA alipokuwa Arusha ambapo wanachama marufu wa CHADEMA walirudisha kadi na kujiunga na CCM ambapo wao ndio walio muingiza Lema ubunge mwaka 2010 na kusema wamechoshwa na ulaghai unaoendelea ndani ya CHADEMA.

Kadhalika alipokuwa Kilimanjaro maeneo ya hai na Moshi viwanja vya Mashuja makada wengine wengi walirudisha akiwemo katibu wa CDM wilaya ya Hai na wengine wengi huku wakisema wanakimbia aibu isije ikawakuta hali hIyo inazidi kumpa kiki Magufuli na kuona njia ya kwenda ikulu, hali hIyo imezoa taharuki ndani ya UKAWA na kujiona wao si chochote mbele ya moto huu wa Magufuli.

Tumpe kura za ndiyo Dr.John Pombe Magufuli kuwa rais wa Tanzania wa awamu ya tano.........................................................
 
Magufuri hakuna asikokinukisha mpaka kwenye ngome za wapinzani ..ni balaa
 
kaskazini msifikiri ni malofa kihivyo,subirini tarehe 25 ndiyo mtatujua.tusingeacha kwenda kusikiliza vihoja vya magufuli eti tanesko wanamhujumu wanamkatia umeme,eti atafufua viwanda.hizi ngonjera tulishazisikia tangu enzi za kale.utaanzishaje viwanda wakati hakuna umeme.inawezekana magufuli akapata uraisi au asipate na kama akipata miaka mitano maisha kwa ccm hayatabadilika kamwe.watawala ni wale wale waliotemwa kwenye kura za maoni za ubunge sasa ni wakuu wa wilaya.watu hawa tumewasikia tangu miaka 40 iliyopita serikalini mpaka leo hawajaweza hata kuweka umeme wa uhakika leo wakina magofuli watajenga viwanda wapi na wapi.ni ujinga sana kuwachagua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom