Yaliyojiri bungeni Dodoma leo tarehe 06/06/2016

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Maswali na Majibu
Swali: Je serikali ina mpango gani wa kukamilisha upanuzi wa Hospitali ya Tumbi Kibaha?​

Majibu: Serikali mpaka sasa imetumia kiasi cha shilingi bilioni 5.98 kwa ajili ya upanuzi wa hospitali hiyo.

Katika bajeti ya mwaka 2016/2017 serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kuendeleza upanuzi wa hospitali hiyo.

Swali: Je serikali imejipanga vipi kuhakikisha utekelezaji wa dhana hii ya elimu bure ili kuepusha migogoro kati ya wakuu wa shule, walimu, wazazi na wanafunzi?

Majibu: Serikali inatuma kiasi cha shiliing bilioni 18.77 kila mwezi kugharamia mitihani, chakula na kununua vifaa vya kufundishia.

Ili kuepusha migogoro Serikali imetoa miongozo kila mkoa ikifafanua juu ya utekelezaji wa mpango huo.

Swali: Ni jambo gani linazuia utumizi wa vyumba vya upasuaji vya vituo vya Bukene na Itogo?

Majibu: Ni kutokana na kukosekana kwa mtaalamu wa usingizi, ambapo aliyekuwepo amesimamishawa kwa tuhuma za rushwa. Serikali inafanya juhudi kuhakikisha mtaalamu huyo anapatikana.

Swali la Nyongeza: Je serikali ina majibu gani kuhusu majengo ya hospitali yanayojengwa bila kukamilika?

Majibu: Tatizo ni bajeti. Serikali imeelekeza halmashauri kuwasilisha mchanganuo wa majengo yote ambayo hayajakamilika toka mwaka 2007.

Swali: Ni mafanikio gani yamepatikana kutokana na kutumika kwa sheria ya makosa ya mtandao?

Majibu: Kuimarika kwa matumizi wa mtambuka katika biashara na nyanja nyingine.

Sheria imesaidia kupungua kwa uchochezi, imesaidia kupungua usambazaji wa picha za ngono na usambazaji wa nyaraka za siri za serikali.

Tangu sheria hii kuanza kutumika, mafanikio yafuatayo yamepatikana;

Kabla ya sheria :Matukio 459 ya picha za ngono yaliripotiwa- baada ya sheria tukio moja la picha za ngono limeripotiwa.

Kabla ya sheria :matukio 119 ya uchochezi yaliripotiwa- baada ya sheria,hakuna tukio la uchochezi lililoripotiwa

Kabla ya sheria : matukio 9 ya usambazaji wa nyaraka za siri za serikali yaliripotiwa- baada ya sheria, matukio 2 ya usambazaji wa nyaraka za siri za serikali yameripotiwa.

Swali: Serikali ina mpango gani wa kutengeneza barabara ya Karagwe na Kerwa kwa kiwango cha lami?

Majibu: Barabara ni ya changarawe na inapitika wakati wote pia ina urefu wa km 112.

Jumla ya km 10 zimeshawekwa lami. Kwa mwaka2015/16 km 42 zimewekwa katika hali nzuri na km moja zaidi itajengwa kwa kiwango cha lami

Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuifanyia upembuzi yakinifu ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami.

Swali: Je sera ya elimu ya mwaka 2004 itaanza kutekelezwa lini?

Majibu: Utekelezwaji utaanzwa baada ya kupitishwa kwa sheria ya elimu.

Kuna upungufu wa walimu 22,460 wa masomo ya sayansi na hisabati. Pia kuna upungufu wa walimu 7688 wa masomo ya sanaa.

Katika bajeti ya mwaka 2017 serikali imetenga kiasi cha bilioni 48 kwa ajili ya kuboresha shule za msingi na sekondari

Aidha serikali inatarajia kuajiri walimu 35,411 kwa mwka 2016.

Swali: Serikali ina mpango gani wa kuondoa kero ya maji katika manispaa ya Morogoro?

Majibu: Upanuzi wa mtandao katika maeneo yasiyo na mtandao wa maji, kufunga pampu katika eneo la Mizani. Eneo la Mindu kuna mradi wa maji unaoendelea kwa ajili ya kata ya Kisangu.

Aidha serikali imeanzisha mradi mkubwa utakaotatua kero ya maji mpaka mwaka 2025, mradi huu unafadhiliwa na serikali ya Ufararansa na Ujerumani na utagharimu kiasi cha Euro 40,000.

Katika bajeti ya mwaka wa 2016/17, serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 4 kuendelea kukamilisha miradi ya maji.

Swali: Ni lini serikali itawapatia maji wananchi wa jimbo la Lushoto?

Majibu: Serikali inatekeleza miradi ya maji Lushoto kama ifuatayo: Mradi wa maji wa Mlola umekamilika kwa 50%, mradi wa maji wa Malindi umekamilika kwa 80%.

Miradi mingine imewekwa katika mradi wa maji wa awamu wa awamu ya pili. Miradi ambayo itatekelezwa na halimashauri.

Katika bajeti ya mwaka 2016/17, serikali imetenga kiasi cha 3.4 kukamilisha miradi inayoendelea katika Manispaa ya Lushoto.

Swali: Je serikali itatekeza lini ahadi yake ya kukamilisha usambazaji wa umeme katika jimbo la Hanang?

Majibu: Serikali itakamilisha ahadi hiyo katika mradi wa REA awamu ya tatu. Serikali imetenga shilingi bilioni 15.8 kwa ajili ya kukamilisha mradi huo.

Wananchi 15,000 wa awali wanatarajiwa kuunganishwa katika mradi huu.

Swali: Je serikali imepanga kujenga majengo mangapi katika wilaya ya Itilima na Busega na je ina mpango gani wa kuboresha makazi ya askari katika wilaya hizo?

Majibu: Kwa mwaka huu wa 2016/17 wilaya hizo hazikutengewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za jeshi la polisi.

Wizara itaendelea na juhudi mbadala za kuendelea kuhamasisha wananchi na wadau wa maendeleo kuchangia ujenzi wa nyumba hizo.

Aidha katika mradi wa serikali wa ujenzi wa nyumba 1331, mkoa wa Simiyu utajengewa nyumba 150 kwa ajili ya makazi ya Polisi.
 
Wabunge ni wabunge kwa sababu majina tunayajua. Majimbo ndiyo hewa kwa sababu ulienda Bungeni viti vya majimbo hayo utavikuta viko wazi.
 
Wabunge wa upinzani wametoka wamebaki wabunge ndiyo hivi nyie wazee wa sukari buku saba kg 1 mbona kama......bahati yenu tcra wananichora ningewa....
 
Back
Top Bottom