CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,627
- 5,044
Hatimaye PPP ya David Kafulila iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 103 ya mwaka 2010 na kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2014, 2018 na 2023 sasa rasmi imeanza kuzaa matunda chanya kwa manufaa ya Watanzania hasa baada ya kuanza kutumika kwa marekebisho mapya ya Sheria hiyo ya mwaka 2023 ya Sheria hiyo Namba 103.
PPP kwa kumtumia mbia mzawa toka kampuni ya Tosh Logistics Limited wanajenga jengo kubwa huenda ikawa ni zaidi ya lile la Mlimani City kwa gharama ya TZS 36.7bn wakati matumizi yatagharimu kiasi cha TZS 13.3bn litakalokuwa na wapangaji zaidi ya 900 lenye ghorofa 10 kwenda juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa PPP-Centre Bw. David Kafulila ameiambia kamati ya Bunge ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuwa Dar es Salaam City Council's Economic and Development Corporation (DDC) katika wakati wote wa Ujenzi wa mradi huo kila mwaka watajizolea kiasi cha TZS 2 bilioni na baada ya mradi huo kukamilika watalipwa kiasi cha TZS 2.5 bilioni kama kodi ya jengo tu bila kuhesabu kodi za TRA pamoja na shuru zingine mbalimbali lakini kubwa zaidi baada ya muda wa mkataba kuisha jengo hilo litasalia kuwa ni mali halali ya serikali ya Tanzania.
Mkurugenzi huyo ameiambia kamati hiyo ya Bunge kuwa Ujenzi wa mradi huo ni miongoni mwamiradi yenye mikataba bora zaidi ya uwekezaji na Ubia kuwahi kushuhudiwa hapa kwenye ardhi ya Tanzania.
Mkurugenzi huyo ameishukuru na kuipongeza kamati hiyo ya Bunge kwa kutembelea mradi huo wa Ubia huku akiomba ushirikiano zaidi kati ya TAMISEMI na PPP ili kwa pamoja waweze kuvuta mitaji zaidi toka sekta binafsi ili kujenga miradi yenye tija na thamani halisi ya fedha kwa manufaa ya Taifa kwani miradi hii itaipatia Serikali Kodi pamoja na tozo mbalimbali na hivyo kuchochea ukuaji wa Uchumi endelevu huku Serikali ikiachwa ifanye au itekeleze miradi ile tu ambayo haina sura ya kibiashara na hivyo kuipa nafuu zaidi Serikali katika kutafuta Mikopo na misaada mbalimbali toka kwa wahisani na mashirika mbalimbali nje na ndani ya nchi ili kutekeleza miradi hiyo.
Pia soma Prof Kitila: Bajeti ya 2025|26 miradi mikubwa itatekelezwa kwa PPP