Yaliyojiri Bungeni Dodoma leo Mei 23, 2016

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Mchango wa Joshua Nasari-Mbunge Arumeru Mashariki



Mh. Nasari analalamikia suala la serikali kushindwa kutatua migogoro ya ardhi na kuishia kutoa ahadi zisizotekeleka.

Hotuba ya kambi Rasmi ya Upinzani bungeni kuhusu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.



KUB inajikita zaidi katika swala la migogoro ya ardhi.

KUB inashauri serikali kuweka mipango itayosaidia kuondoa migogoro ya ardhi nchini.

KUB inalalamikiwa pia wizara kutengewa fedha ndogo kulingana na mahitaji halisi.

Pia kambi inalalamikia serikali kutotoa fidia wakati wa wananchi wanahamisha kupisha miradi mbalimbali.

Umiliki mkubwa wa ardhi na makampuni makubwa ambayo ilipatikana bila kuzingatia sheria za nchi.

Kambi inashauri serikali kulipa shirika la nyumba ili liweze kujenga nyumba za gharama nafuu.

Kambi imelalamikia serikali kuu kukusanya kodi ya majengo na kudai kitendo hicho ni cha kubana halmashauri zilizo chini ya ukawa.

============

Swali :Ni lini serikali itapeleka fedha kukamilisha chaguzi za vijiji kwenye kata Katumba?​

Majibu : H/mashauri inaendelea na maandalizi ya uchaguzi na pindi yakikamilika uchaguzi utafanyika, aidha serikali imetenga Tsh milioni 3.3 kufanikisha uchaguzi huo.

Sababu kubwa iliyochelewesha uchaguzi huo ni kutokana na wakimbizi wa eneo hilo walikuwa hawajapewa uraia.

Swali: Je serikali iko tayari kutekeleza ombi la H/mashauri ya Rungwe la kutengewa Tsh 7.9?

Majibu : Kutokana na fedha zilizotengwa kwa mwaka wa fedha 2016/17 kila h/mashauri itaweza kupata sh bilioni 1.3. Aidha serikali itaendelea kupeleka fedha kadiri zitakavyopatiana.

Swali: Je serikali ina mpango gani wa kuboresha makazi ya askari polisi na magereza?

Majibu: Serikali inafahamu hilo na imeanza ukarabati wa nyumba zilizopo na kujenga mpya. Mahitaji halisi ni nyumba ni nyumba 1450 wakati zilizopo ni nyumba 221.

Mikoa 15 ya Tanzania bara na mikoa 5 ya Zanzibar itanufaika na mpango wa nyumba za Magereza.

Swali : Je serikali haioni kuruhusu ndege ndogo kuongozwa na rubani mmoja ni kuyaweka rehani maisha ya abiria?

Majibu : Taratibu za kuongoza ndege huongozwa na miongozo ya kimataifa na iliyokubalika na bunge.

Marubani hupimwa afya zao na madaktari bingwa kila baada ya miezi sita.
Serikali inaruhusu kurusha ndege hizo ndogo zikiwa na rubani mmoja.

Aidha ndege kubwa zinatakiwa kuongozwa na marubani zaidi ya mmoja.

Serikali imejipanga kufunga vifaa vya kisasa katika viwanja vyote vya ndege nchini.

Swali : Ni lini barabara ya Norondo hadi Mpango itajengwa kwa kiwango cha lami?

Majibu: Serikali inatafuta fedha kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami. Aidha serikali kupitia TANROADS itaanza kwa kuijenga kwa kiwango cha changarawe wakati inasubiria kujengwa kwa kiwango cha lami.

Aidha serikali itaendelea kuboresha barabara nchini na kupiga marufuku magari yanayozidisha uzito kwani yanaharibu barabara.

Swali: Serikali ina mpango gani wa kuongeza usikivu wa matangazo ya TBC Songea?

Majibu : Ni kweli toka Julai 2013 mtambo haufanyi kazi. TBC imehamisha mitambo na kuifunga katika milima ya Matogolo ili kuboresha usikivu.

Aidha TBC imefanya upembuzi yakinifu kufunga mtambo wa FM katika eneo la Mbamba Bay ili kuboresha usikivu.

Swali : Ni lini serikali itajenga viwanda Simiyu?

Majibu : Moja ya vipaumbele vya serikali ni kujenga viwanda vinavyochochea matumizi ya maligafi za ndani.

Serikali inahimiza wananchi kuvumbua fursa za uwekezaji katika mikoa mbalimbali.
Aidha vijana ambao wanafikra za kijasiriamali wanahamasishwa kujiunga katika vikundi na kuwasilisha mawazo yao ili waweze kuapatiwa fedha kutekeleza.

Aidha serikali serikali itatoa status ya upatikanaji wa sukari nchi nzima.

Swali : Ni lini serikali itaanza ujenzi wa mradi wa EPZ ili kuboresha soko la Tanzanite katika H/mashauri ya wilaya ya Simanjro?

Majibu : Eneo hili kwa sasa liko huru na ujenzi utaanza muda wowote.
Serikali ina mpango wa kugeuza eneo la Mirerani kuwa special Economic Zone ili kudhibiti maligafi zinazozalishwa katika eneo hilo

Swali: Serikali ina mpango gani wa kuondoa tatizo la maji katika mkoa wa Songwe hasa katika wilaya ya Tunduma.

Majibu : Serikali imekamilisha usanifu katika kata ya Rua na Isongolwe na uandaaji wa zabuni kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa maji wilayani humo. Serikali inajadiliana na wafadhili kwa ajili ya kupata mikopo ya masharti nafuu ili kutekeleza miradi hiyo.

Aidha Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya upanuzi wa miradi wilayani humo.
 
Waziri Mwakyembe kukaimu nafasi ya KIONGOZI WA SHUGHULI ZA SERIKALI BUNGENI kwa kipindi ambacho Mh. Waziri Mkuu Majaliwa atakua kwenye ziara nje ya nchi.
 
Vipi kubana matumizi kwa Pm kusafiri nje ya nchi? Nimeamini tatizo ni ngeli ndio maana mkuu anakimbia
 
Hivi ndege Ndogo inaweza kukaa marubani wawili haya maswali mengine ni maajabu sana?Nafikiri tunafanya mistake kubwa sana kwenye kuchagua wawakilishi na inatugharimu sana.
 
Hivi ndege Ndogo inaweza kukaa marubani wawili haya maswali mengine ni maajabu sana?Nafikiri tunafanya mistake kubwa sana kwenye kuchagua wawakilishi na inatugharimu sana.

Mkuu kwa nini unaona hivo? Mbona helikopta inabeba watu wengi tuu?
 
SERIKALI jana ilitoa majibu mapya yenye ufafanuzi wa kina kwa swali lililojibiwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambalo pamoja na masuala mengine, limeeleza mkakati wa serikali kujenga nyumba zaidi ya 9,000 kwa ajili ya askari Magereza na Polisi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alijibu swali hilo jana lililoulizwa na Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) kwa niaba ya Mbunge wa Viti Maalumu, Devotha Minja (Chadema).

Akiuliza, Selasini alisema, “Sasa naomba swali namba 211 la Mheshimiwa Devotha Minja lililoleta kasheshe sasa lijibiwe.” Hata hivyo swali lililosababisha uteuzi wa Kitwanga kutenguliwa Ijumaa iliyopita, liliulizwa na Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga kwa niaba ya Minja kuhusu serikali kuwaboreshea askari makazi, ambalo hata hivyo ilibainika Waziri alikuwa amelewa.

Baada ya majibu ya Waziri Kitwanga, jioni yake, Rais John Magufuli alitangaza kumfuta kazi Kitwanga kwa kosa la kujibu swali akiwa amelewa. Baadaye Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) aliomba Mwongozo wa Spika akisema halikujibiwa kikamilifu kama kanuni zinavyoelekeza. Baadaye jioni, Kiti cha Spika kilijibu mwongozo huo na kuamuru kuwa swali hilo lijibiwe kikamilifu Jumatatu (jana).

Nyumba za Magereza, Polisi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alisema katika kukabiliana na tatizo hilo la makazi kwa askari, serikali imeendelea na mpango wa kuzifanyia ukarabati mkubwa baadhi ya nyumba kwenye baadhi ya Magereza na kujenga nyumba mpya.

“Mahitaji ya nyumba hivi sasa ni nyumba 14,500 wakati zilizopo ni 4,221 hivyo kuwepo upungufu wa nyumba 10,279 ambao unalazimisha baadhi ya askari kuishi nje ya kambi za Jeshi la Magereza,” alisema Masauni.

Alisema serikali kupitia Jeshi la Magereza, imesaini mkataba na Kampuni ya Poly Technologies ya China kwa kujenga nyumba 5,900 kwenye vituo vyote vya magereza nchini. Aliutaja mgawanyo wa ujenzi wa nyumba hizo ni Makao Makuu ya Magereza nyumba 472, Arusha 377, Dar es Salaam 952, Dodoma 356, Kagera 364, Kigoma 272, Kilimanjaro 290 na Lindi 233.

Nyingine ni Manyara 206, Mara 378, Mbeya 622, Iringa 622, Iringa 336, Morogoro 369, Mtwara 215, Mwanza 398, Pwani 384, Rukwa 358, Ruvuma 320, Shinyanga 337, Singida 299, Tabora 408, Tanga 382 na KMKGM Dar es Salaam 219.

Aidha, Chuo cha Ukonga 115, Chuo cha Kiwira 183, Chuo Ruanda 62, Chuo KPF 27, Bohari Kuu 82 na Bwawani 84. Akizungumzia Jeshi la Polisi, alisema serikali inakusudia kujenga nyumba 4,136 katika mikoa 19 ya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Serikali itaendelea kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mikopo yenye riba nafuu, miradi Shirikishi (PPP) na kwa kutumia fedha za bajeti ya serikali kadri hali ya uchumi itakavyokuwa ikiimarika,” alisema Masauni.

Akijibu maswali ya nyongeza ya Selasini, Naibu Waziri alisema si kweli kuwa magereza yameacha shughuli za uzalishaji uchumi kama kilimo, ushonaji na ufugaji. Alisema jeshi hilo lina mpango kabambe wa kuendesha miradi hiyo na imeshaandika andiko la miradi minane lililowasilishwa serikalini na pia tayari wameandaa mpango kazi wa kujitegemea.

Alitaja miradi hiyo kuwa ni ya kilimo, ushonaji viatu, samani, umwagiliaji, ufugaji ng’ombe, ulimaji alizeti na mpunga katika magereza yakiwamo ya Kigongoni, Karanga, na Songwe.

Habari Leo
 
Binafsi sijaridhika na namna alivyoondolewa kitwanga! Na kama kitwanga alitoa majibu ya kilevi bungeni, kiongoz wa shughuli za serkali bungen alipaswa aingilie kati kutjuza hilo na sio kusubiri mwongozo wa mzee Selasini! Pia nadhan bunge linayo kamati ya maadili ambayo inauwezo kumshughulikia kitwanga kabla ya mh. Rais kuingilia kati kwa kumtimua waziri!
 
Tumlaumu PM aliepeleka taarifa kwa Rais hata kabla hawajakaa na kamati ya maadili au tumlaumu nani? Kama sio PM kumpigia simu JPM nadhani angeonywa tu na mambo yangekuwa shwari! Je PM nae ametumika kumvurigia ulaji Kitwanga?
 
Binafsi sijaridhika na namna alivyoondolewa kitwanga! Na kama kitwanga alitoa majibu ya kilevi bungeni, kiongoz wa shughuli za serkali bungen alipaswa aingilie kati kutjuza hilo na sio kusubiri mwongozo wa mzee Selasini! Pia nadhan bunge linayo kamati ya maadili ambayo inauwezo kumshughulikia kitwanga kabla ya mh. Rais kuingilia kati kwa kumtimua waziri!
Walishindwa kumtimua Kitwanga kupitia Lugumi. Kwa sababu Lugumi inaihusisha Msoga. Unapotaja Msoga unataja Mwenyekiti wa Chama Cha Majipu (CCM). Na Magufuli akisikia CCM anakumbuka fadhila ya Urais, hapo ananywea na kunyamaza kimya. Magufuli hana Ubavu wa kupambana na giants wa Rushwa na Ufisadi, ataendelea kupambana na vijisababu vidogo vidogo vya papo kwa hapo.
Tumlaumu PM aliepeleka taarifa kwa Rais hata kabla hawajakaa na kamati ya maadili au tumlaumu nani? Kama sio PM kumpigia simu JPM nadhani angeonywa tu na mambo yangekuwa shwari! Je PM nae ametumika kumvurigia ulaji Kitwanga?
 
Binafsi sijaridhika na namna alivyoondolewa kitwanga! Na kama kitwanga alitoa majibu ya kilevi bungeni, kiongoz wa shughuli za serkali bungen alipaswa aingilie kati kutjuza hilo na sio kusubiri mwongozo wa mzee Selasini! Pia nadhan bunge linayo kamati ya maadili ambayo inauwezo kumshughulikia kitwanga kabla ya mh. Rais kuingilia kati kwa kumtimua waziri!

Kamati ya maadili ya bunge ni kuwazuia ukawa wasiwasilishe hoja za kutetea maslahi wa taifa. Huwezi kukuta kamati ya maandili inashughulika na mtu yeyote wa ccm.

Bunge la sasa halina kitu maadili na kutukana wabunge wa upinzani ni msingi halali bungeni ili kuwafanya wajisikie vibaya, wakose nguvu na kuwakatika tamaa ya kuwakilisha hoja zao.

Spker na msaizi wake wameungana kuhujumu haki za Watanzana za kuwakilishwa na wamesimama kidedea kugandanimiza upinzani kila mtu akiona.

Ulitegemea bunge la namna hiyo liseme Kitwanga kakosea mahali?

TUNADAI KATIBA MPYA. BUNGE NA NDUNGAI LINAONYESHA UBARADHULI MKUBWA SANA DHIDI YA HAKI ZA WATANZANIA.
 
... Pia nadhan bunge linayo kamati ya maadili ambayo inauwezo kumshughulikia kitwanga kabla ya mh. Rais kuingilia kati kwa kumtimua waziri!

Kuna vitu viwili hapo - ubunge na uwaziri. Uwaziri una mamlaka yake ya uteuzi na nidhamu ambayo ni Rais. Ni Rais pekee mwenye mamlaka ya uteuzi wa mawaziri na ndiye pekee mwenye uwezo wa kutengua na sio Bunge au chombo kingine chochote.
 
Tuesday, May 24, 2016
Waliokosa Ubunge Walipuliwa Bungeni,Mbunge Adai NHC Imepoteza Mwelekeo.
favicon.png


Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (CCM), maarufu kwa jina la ‘Maji Marefu’ amewalipua wabunge waliokosa ubunge katika kipindi hiki na vilivyopita kwa kuhodhi nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mjini Dodoma na kupangisha watu wengine kinyume cha utaratibu wa shirika hilo.
Alisema hali hiyo imefanya wabunge wapya, ambao ni asilimia 70 ya wabunge wote kwa sasa, kukaa nyumba za kulala wageni wakati zipo nyumba hizo kwa wabunge kulingana na mkataba na NHC.
Mbunge alisema wapo watu wamepangishwa na wabunge hao wa zamani, ambao wamegeuza nyumba hizo kama kitega uchumi kinyume na taratibu.

Ngonyani alisema hayo bungeni mjini hapa jana wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Alimuomba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kufuatilia suala hilo na shirika kwa ujumla, aondoe wapangaji hao waliowapangishia wengine kinyume cha utaratibu na kuwapatia nyumba wabunge wapya ambao hawana nyumba za kuishi.
Alisema wabunge hao waliokosa nafasi ya kurudi jimboni miaka tofauti, mkataba wao wa kupangishwa nyumba hizo umekwisha, kwani ukishakosa ubunge hauna dhamana tena mpaka utakaporudi.
“ Kuna wapangaji wengi ambao ni wabunge waliokosa nafasi hiyo ambao wamepangishwa na shirika na badala yake hadi leo wamezishikilia nyumba hizo hawataki kuziachia, ”alisema Ngonyani.
Alieleza kuwa baada ya kukosa nafasi za ubunge na kushindwa kurudi bungeni, wabunge hao walipaswa kurejesha nyumba hizo kwa shirika, ambalo ndilo lenye mamlaka ya kupangisha na si wao kupangisha wapangaji wengine kupitia mikataba yao.
Hata hivyo, taarifa kutoka NHC, Dar es Salaam jana kuhusu nyumba hizo zilifafanua kuwa hazikutengwa kwa ajili ya wabunge pekee, bali hata watu wa kawaida na kila mtu anaingia mkataba binafsi na shirika.
Pia zilieleza kuwa, nyumba hizo zilikodishwa awali kutokana na mahitaji ya wabunge uliokuwapo na wapo walionunua, hivyo wana dhamana nazo.

Aidha ilieleza kuwa ikiwa kuna mpangaji aliyepangisha mtu mwingine bila kujali alikuwa mbunge au la, anakwenda kinyume cha utaratibu, watafuatilia suala hilo.
Katika hatua nyingine, Ngonyani alisema bungeni kuwa NHC imebadilisha dhana na kutoka kwenye kujenga nyumba za bei nafuu, kusaidia wananchi wenye uwezo mdogo sasa inafanya biashara, kwani inajiendesha kibiashara na si kwa lengo la kuundwa kwake.
Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulya (CUF) alisema nyumba za shirika hilo zimejengwa kwa ajili ya mabepari kwa sababu wananchi wa kawaida kutozimudu kutokana na bei zake za kati ya Sh milioni 40 hadi milioni 60.
Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso (CCM) alitaka shirika lijenge nyumba kulingana na uwezo wa watu wa eneo husika kutokana na kuwa wanajenga nyumba za gharama kubwa.

Alisema ujenzi huo uzingatie katika miji inayokua kuiweka katika mandhari nzuri na wakazi wa maeneo husika kumudu kupanga na kununua.
 
Tumlaumu PM aliepeleka taarifa kwa Rais hata kabla hawajakaa na kamati ya maadili au tumlaumu nani? Kama sio PM kumpigia simu JPM nadhani angeonywa tu na mambo yangekuwa shwari! Je PM nae ametumika kumvurigia ulaji Kitwanga?

PM ni Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni na pia ndiye "Msimazi Mkuu" wa utendaji wa kila siku wa Serikali. Msimamizi Mkuu ni pamoja na kuhakikisha nidhamu ya anaowaongoza na kama kuna tatizo ni kuchukua hatua. Kuchukua hatua ni pamoja na kuadabisha pale ambapo mamlaka yake inaruhusu vinginevyo anapaswa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili ichukue hatua stahiki. Suala la Kitwanga angeonekana wa ajabu kama angekaa kimya eti ili "kuficha uozo".
 
Tumlaumu PM aliepeleka taarifa kwa Rais hata kabla hawajakaa na kamati ya maadili au tumlaumu nani? Kama sio PM kumpigia simu JPM nadhani angeonywa tu na mambo yangekuwa shwari! Je PM nae ametumika kumvurigia ulaji Kitwanga?

PM was right. Maamuzi legelege ya kulindana hayana nafasi awamu hii.
 
hivi ni kwanini maswali bungeni huwa yanajibiwa jibiwa tu ili kumridhisha aliyeuliza?
 
Tumlaumu PM aliepeleka taarifa kwa Rais hata kabla hawajakaa na kamati ya maadili au tumlaumu nani? Kama sio PM kumpigia simu JPM nadhani angeonywa tu na mambo yangekuwa shwari! Je PM nae ametumika kumvurigia ulaji Kitwanga?
kwanini usimlaum mlevi unamlaumu aliyeripoti ulevi?
 
Back
Top Bottom