Yaliyojiri Bunge la Bajeti Dodoma Mei 14, 2015

Yaliyojiri Bunge la Bajeti Dodoma Mei 14, 2015

" Wazee ilisemwa watatibiwa bure lakini haifanyiki hivyo...wazee watambue CCM ni waongo na haiwajali"- Owenya
 
" Polisi bado wanaishi kwenye full suit bati kuanzia juu mpaka chini...makazi yao ni mabovu na wala hamuwajali"-Owenya
 
" Sisi watanzania tunaishi kwa kudra za mwenyezimungu na sio Sera na bajeti au mipango ya CCM"-Mchuchuri
 
" Wakulima wanaishi kwa kudra za mwenyezimungu na sio Sera na mipango ya CCM"-Mchuchuri
 
" Watu wakisema CCM wamechoka hawabahatishi....mambo yenyewe yapo wazi"-Mchuchuri
 
" Vikundi vinapewa jumla ya milioni moja, laki tano ama milioni mbili....kwenye kikundi kuna watu 50 hivi ndio tunawawezeshaa watu kwa namna hii?"-Mchuchuri
 
" Nampongeza Raisi kwa kuwafariji na kuwatembelea waathirika wa mafuriko Dar"- Idd Azzan
 
" Naomba Serikali ipime viwanja vingine ili kuwasaidia waathirika wa mafuriko dar es salaam"- Idd Azzan
 
Hilo bunge... nadhani wasome budget tu ya MKuya na Mwigulu ambayo Lissu alishasema ni silly season manake hamna cha maana humo zaidi ya kupandisha kodi za mafuta, pombe na sigara!! Wasome hiyo budget kila mtu arudi jimboni kwake wasubirie hasira zetu..

Wanachofanya sasa hivi ni vituko tupu, Hivi mchango wa KIbajaji jana unaweza kusema huyo mtu analipwa posho kwa kutumia kodi zetu kweli?
 
" Ujenzi wa bara bara wa mabasi yaendayo kasi imeharibu miundo mbinu ya jangwani hivyo kusababisha maji kupita juu ya bara bara mvua zikinyesha"- Idd Azzan
 
" Watu wengi wanaishi mashuleni...kwa jamaa zao....tunaomba Serikali itusaidie...mfuko wa maafa utusaidie watu wa Dar"- Idd Azzan
 
Back
Top Bottom