Habari.....
Ipo hivi jana nilikuwa nimetoka zangu kinondoni narudi home kimara- suka
nilipofika usalama nikaanza kutafuta daladala ya kwenda suka kama ww
mwenyeji wa dar utakuwa unajua usafiri wa kwenda mbezi usiku unavosumbua
sijazoea kugombania daladala lakini baada ya kukaa sa 1kituoni bila
kupata gari ikabidi nikubaliane na hali halisi ya kugombania,ikaja
daladala ambayo ilikuwa inaishia suka ndipo nilipo amua kuingia hvyo
hvyo bila kujali
Kiukweli tulikuwa tumebanana sana hakkuwa na namna sababu ilikuwa kama
sa 2 usiku inaenda sa 3 nilisimama usawa wa kiti ambacho dada mmoja
mweupe alikuwa kakaa hapo kwa jinsi tulivyo banana niliamua kugeukia
kutazama dirisha sasa mkono mmoja ulipita juu ya kichwa cha yule dada na
nikashika nguzo ya dirisha mkono wa kulia ukashika kiti kilicho kuwa
mbele ya yule dada na hata gari ingedunda vipi nisingeweza kumgusa ....
Nilizubaa mbele kumuangalia mzee mmoja ambae alikuwa na smartphone
huawei kilicho fanya nizubae kuangalia ile simu ni kuwa yule mzee
alikuwa kama wa miaka 55 hadi 60 hivi lakini nilishangaa kuona aki click
JF application na kufika hadi kwenye jukwaa la MMU na kufungua
Lakini nilishindwa kuona ni uzi gani aliufungua kwani nilishutuliwa na
vibao viwili vya mkononi kutoka kwa yule dada na akanza kuongea we kaka
vipi unataka kunitoboa macho utanizaa ukinifanya nikiwa kipofu
alinifokea sana bila kuelewa kosa langu ni lipi na akanivyonza sana hata
mama angu mzazi hajawahi nifokea vile abiria wote walishikwa na butwaa
kuona yule dada alivyo kuwa akinifokea na kuongea maneno yasiyo na
hekima nilipandwa sana na hasira nikashindwa kuongea hata sikumjibu kitu
nilimwangalia usoni kama dakika 1 hivi nikajisema moyoni malipo ni hapa
hapa duniani,
Ndipo abiria wakanza kumsema yule dada na kumuonya kuacha hiyo tabia
Yule mzee wa MMU alikuwa mstari wa mbele sana kumsema yule dada sijui
anatumia ID gani humu ningemtaja lakini bila shaka huu uzi anausoma na
atakuwa shahidi wa kile kilicho tokea na kuja kushuhudia hapa nilipenda
san alivyo mpa makavu yule dada lengo langu lilikuwa ni kufika manzese
nishuke kwa hasira nilizo kuwa nazo lakini sikushuka kwa jinsi abiria
walivyo mshambulia yule dada akiwepo mzee wetu wa humi MMU nilimsikia
akisema ndo maana yeye kamua kumuozesha binti yake kwa laki 2 kwasababu
ya tabia za ajabu za akina dada walizo nazo na kuhofia isije siku
wakachana afu akashindwa kurudisha mahali
Mzee najua unanisikia plz njoo uwe shahidi wa haya bahati mbaya kimara
mwisho yule mzee alishuka
Inaniuma sana kwa alichonifanyia yule dada sitamsahau leo hadi kesho
kwanini anifanyie vile mm binadamu mwenzake,mimi nilimkosea nini kama
alikuwa hataki kubanwa kwanini alipanda daladala ni kujiona au nini
inaniuma sana nyie akina dada sijui nani ali walaani
Eeeh Mungu baba msamehe kwani halijui alitendalo