Yale Matrekta Pale Mwenge Jeshini na Sera ya Kilimo kwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yale Matrekta Pale Mwenge Jeshini na Sera ya Kilimo kwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Stuxnet, May 11, 2011.

 1. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nisaidieni mwenzenu pengine ubongo wangu umefika mwisho wake wa kufikiria. Unapokwenda Tegeta kutokea Mwenge baada ya kanisa la Efata au la Mwingira, kuna kituo cha shirika la uchumi la JKT ambao wamerundila matrekta kwa ajili ya kuuza. Ingawaje sina takwimu za mauzo waliyofanya lakini nadhani kwa nchi iliyotamka kuwa KILIMO KWANZA basi si sahihi matrekta hayo kuwa hapo. Hayo matrekta yanapaswa kuwa yako huko Sumbawanga, Mbeya, Morogoro, Songea, Shinyanga kwa ajili ya kunyanyua kilimo chetu duni cha jembe la mkono. Kuyaweka hapo Mwenge hakuna tofauti na biashara za akina yakhe za show rooms za magari zilizoenea kila mahali DSM.

  Kama muhusika ni Jenerali Mwamunyange au Dr Hussein Mwinyi au kama ni Waziri Wa Kilimo basi nasema hawaisaidii chochote nchi hii kwa upande wa Kilimo. Najua watasema ni biashara lakini Kama wangewatumia wataalamu Wa biashara wangewaonyesha namna ya kuyauza kwa mifumo ya hire purchase
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Yule 'Shimbo' wa vitisho anaweza kuwa na jibu!
   
 3. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hii ni nchi ya mikakati na mitikasi, unafikiri yapo pale kwa bahati mbaya!
  Tetesi zinasema Nshimbo anapata fweza ya kusomesha watoto pale, usishangae yale matamko ya kutisha wapiga kura yalikuwa si bure.
  Upande wa pili, kilimo kwanza ndo kinatekelezwa kwa vitendo, kwa namna hiyo unayoiona.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hizo ni za dili za madalali wa ubepari na ujamaa kwa wakati mmoja, teh!
   
 5. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo akina Jenerali Shimbo ndiyo wale makuwadi wa soko huria walioongolewa na hayati Profesa Sethi Chachage
   
 6. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  We unauliza jibu!! Yameanikwa pale huoni? Yalikuja mabichi yakishakauka ndo tunawapelekea wakulima huko kwenu ulikotaja. Kwanza pale yanasaidia kukumbusha wapitao njiani, kuuliza ya kazi gani na hujibiana wenyewe 'kilimo kwanza' mtajuwaje kuwa mpango wa kilimo kwanza upo nyie watu wa Dar si ndo mnajifanya mnajua kuhoji kila kitu? Na tunampango wa kuyaanika mengine pale Ilala, Temeke Ubungo karibu na stendi ya mikoani ili unapokwenda kijijini uyaone na ukawaambie 'matrekta yapo yanakuja nimeyaona kwa macho. Mwisho tutayamwaga pale Jangwani sana tu. Ndo mtakoma kujifanya mnajua. SIKU UTAMSIKIA SHIMBO AKIMJIBU MWANDISHIWA HABARI ALIYEHOJI UWEPO WA MATREKA PALE LUGALO. si ajabu hana haya yule Baba.
   
 7. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,158
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Teh teh teheheheeee, kho... Stuxnet bana wanfurahisha bheye!!!!! Sio Kilimo kwanza, ni Biashara kwanza.....
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  May 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Bora yakae hukohuko Dar maana ndio wapo wenye uwezo wa kuyanunua, hapa kwetu Kavifuti labda watupe bure maana uwezo wa kuyanunua hatuna!
   
 9. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Huu ndio usanii wa Viongozi wetu.....Nimesikia wakitengeneza mchakato wa kuwakopesha wabunge hayo matrekta.......Sasa sijui mbunge analitoa hilo trekta kwa jimbo lake au analimia mwenyewe?!!!!Tanzania haiishi vioja na maigizo hakika
   
 10. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Ni kielelezo kwa wafadhili kuwa kweli tuna nia ya :"dhati" ya Kilimo kwanza!!! Yakiwa sumbawanga na huko kwingine yataonekana saa ngapi Mpwa?? serikali hii kwa dili...we acha tu
   
 11. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kinachojulikana ni kuwa yale matrekta hayafai kwa kulima ardi ya tz kwani yaliundwa kulima ardhi laini ya India sasa kilichotokea wale waliyoyaagiza japo walipewa hilo angalizo waliweka pamba kwenye masikio maana walishalamba 10% yao. Matokeo yake ndiyo hayo matrekta yamebaki kama mapambo.
   
 12. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Wachelewesha matrekta ya 'Kilimo Kwanza'

  MRADI wa matrekta kwa ajili ya mpango wa uboreshaji wa kilimo nchini-Kilimo Kwanza- umekwama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni mgogoro kati ya wafanyabiashara wawili nchini, Yussuf Manji na Jayantkumar Chandubhai Patel (Jeetu Patel), Raia Mwema limebaini.
  Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kwamba mvutano kati ya Jeetu na Manji, umechangia kwa kiasi kikubwa kuchelewa kwa mchakato wa upatikanaji wa matrekta hayo kwa ajili ya mradi wa Kilimo Kwanza, mradi wenye thamani ya Sh bilioni 50.
  Habari zinaeleza kwamba, kwa kutumia mtandao wa mmoja wa wafanyabiashara hao, baadhi ya maofisa wa Serikali wametumika kuuchelewesha na hivyo kuhujumu mchakato wa kukamilishwa kwa taratibu za uidhinishwaji wa fedha za ununuzi wa matrekta hayo.
  Mradi huo uliokabidhiwa kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia kampuni yake ya SUMA JKT, ulitakiwa kuanza mapema mwaka huu, lakini hauna dalili za kuanza kutokana na utata wa kisheria ulioilazimu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuingilia kati.
  Raia Mwema imethibitishiwa kwamba kampuni mbili za nchini India zilizoshiriki zabuni hiyo moja ikiwa imepata sehemu kubwa ya kazi ya kuingiza matrekta hayo, zimeridhishwa na mchakato wa zabuni hizo, lakini tatizo limekuwa kwa mawakala wao nchini ambao ni Manji na Jeetu.
  Malumbano hayo yameelezwa kuwagusa hata watendaji wa juu serikalini kabla ya uongozi wa juu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuingilia kati na kuamuru suala hilo likamilishwe na taarifa ziwasilishwe Wizara ya Fedha na Uchumi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Kijjah, ameliambia Raia Mwema kwamba Wizara yake haikuhusika kwa namna yoyote na ucheleweshaji wa mchakato wa Kilimo Kwanza kwa maelezo kwamba kilichochelewesha ni ushauri wa kisheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, jambo ambalo amesema sasa limeshapatiwa ufumbuzi.
  "Hakukuwa na tatizo la kiuhasibu ama kiuchumi. Lilikuwa ni tatizo la kisheria ambalo sisi hatuhusiki. Watu wa Exim Bank ambao ndio watoaji wa mkopo walitaka maoni ya kisheria kutoka serikalini na sisi tulilazimika kuwapelekea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kwa sasa ndiyo wametuletea na tumewapelekea Exim, wakishapitia watatujulisha kama wameridhika ama la," alisema Kijjah.
  Kijjah alisema fedha hizo ni mkopo kutoka serikali ya India kupitia Exim Bank, japo ni kwa riba nafuu mno kuliko ile ya taasisi nyingine za fedha na kwamba utalipwa na Watanzania wote wakati wake ukifika na hivyo ni lazima Serikali ijiridhishe na kila hatua kuhusiana na matumizi yake.
  Kumekuwa na maoni tofauti kuhusiana na jinsi Serikali ilivyolibeba suala la ununuzi wa matrekta hayo kutokana na kuhusishwa tena kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakihusishwa katika kashfa mbalimbali ikiwamo kashfa maarufu ya wizi wa Fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje Benki Kuu ya Tanzania (EPA).Mwishoni mwa mwaka jana baadhi ya vyombo vya habari vilimnukuu Manji akizungumzia kwa kina kuhusiana na zabuni hiyo ya matrekta ya Kilimo Kwanza, lakini Jeetu Patel amekuwa kimya kuhusiana na suala hilo akikwepa kuhusishwa nalo.Raia Mwema ilipomuuliza Jeetu Patel kuhusiana na suala hilo alikataa kata kata kulifahamu akidai kwamba hajawahi kuhusika kwa vyovyote katika zabuni hiyo na hana cha kuzungumza akisema, "sifahamu lolote kuhusu biashara hiyo… sina cha kuzungumza, ama unataka nikudanganye?"

  Kwa upande wake Manji alitoa taarifa akidai kutoridhishwa kwake na mchakato wa zabuni hiyo ambayo imeelezwa kwamba tatizo kubwa lilikuwa ni "kuzidiana kete" kati ya wafanyabiashara hao wa Tanzania, katika kamisheni ambayo ingetokana na biashara hiyo kutoka kampuni za nchini India.
  Katika mradi huo, Jeetu anatajwa kuwa mwakilishi wa Kampuni ya Escort hapa nchini, yenye makao makuu yake nchini India, ambayo imeshinda zabuni hiyo, wakati Manji anatajwa kuwakilisha kampuni ya Mahindra ya India, ambayo nayo imepata kiasi kidogo cha zabuni hiyo.
  Hata hivyo, baadaye Manji ambaye ni mmiliki kampuni ya Quality Group, alinukuliwa na gazeti la serikali la Habari Leo akisema kwamba ameridhishwa na mchakato wa zabuni hiyo na kukanusha taarifa za awali kwamba amekuwa akitaka kuanika anachofahamu kitakacholenga kuchafua wahusika katika zabuni hiyo ikiwamo JKT.

  Awali ilielezwa kwamba zabuni hiyo ya matrekta ilipitishwa ngazi zote ikiwamo hatua ya Baraza la Mawaziri na kupatiwa baraka zote za kulitekeleza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga, Dk. Hussein Mwinyi, alinukuliwa akisema kwamba hakuna utata wowote katika utekelezaji wa mradi huo, isipokuwa linaweza kufanywa ajenda ya kuchafuana na watu ambao wana malengo binafsi na mradi huo.Dk. Mwinyi alinukuliwa akisema kwamba kampuni zaidi ya 10 ziliomba zabuni hiyo na hatua zote zilipitiwa kwa uangalifu mkubwa na kwamba watakaolalamika wanalenga kuchafuana kwa malengo binafsi.
  [​IMG]
   
 13. ALLEX

  ALLEX JF-Expert Member

  #13
  May 12, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 2,046
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  mbona mnazunguka sisi mpaka tushauriwe na imf
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  May 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  Nduugu miradi ya watu ile trekta ailipiwi ushuru inauzwa million 45 si nikanunue scania uk nilete kwa million 53 mpaka na kodi..stupid mtupu..we waangalie wanajeshi nao wameona huu upuzi watakula wapi kila sehemu kuna mafisadi ila ufisadi wao wa kutukuza k-kwanza
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  May 12, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Jayantkumar Chandubhai Patel aka Jeetu Patel

  hii ni sintofahamu
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  May 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nilikuwa sijawahi kuona Showroom ya Matreka kwa mara ya kwanza nimeiona hapo Mwenge SUMA JKT, si ajabu yako chini ya kiwango kama zile Power Tiller ndio maana yamelundikana tu hapo
   
 17. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #17
  May 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Hahahaaaa, sijui tyukalime nini na wapi?? yaani kweli serikali nzima hakuna mwenye akili hata mmoja ya kuendeleza nchi yake?? kweli??? nadhani tumerogwa somewhere, sasa nin maana ya MAISHA? I better Die
   
 18. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Yaani jamani ina maana Tanzani bila Jeetu Patel haiwezekani? Jeetu yuko kwenye tuhuma za EPA na Manji anatajwa kwenye Kagoda, sasa haya makesi yaliyopo mahakamani Ina maana ni kiini macho tu? Halafu tunauliza kwa nini Tanzania ni maskini wakati tunajipeleka wenyewe kwa mafisadi?
   
Loading...