Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,094
- 9,261
1.0 Akaunti ya ESCROW
1.1 Kufungua ESCROW Akaunti
Mwaka 2004, TANESCO kwa ushauri wa Mkono & Co Advocates walitoa hoja kuwa gharama za kununua umeme zilikokotolewa kwa kutumia IRR ya asilimia 22.3 na makadirio ya gharama za mtaji wa asilimia 30 ambao ni Dola za Marekani milioni 38.16, wakati mtaji halisi (equity) wa IPTL ni chini ya Dola za Marekani 1,000. Hivyo, TANESCO walikuwa wakitoa notisi (dispute notice) kwa kila ankara ya malipo kupinga gharama hiyo kulingana na kifungu Na. 6.8 cha Mkataba wa PPA. Kifungu hicho kinaeleza kuwa ikiwa upande wowote haukubaliani na usahihi wa malipo katika ankara zilizowasilishwa kwa ajili ya malipo ya gharama za umeme wanatakiwa watoe notisi (invoice dispute notice) kwa upande mwingine. Vile vile, Mawakili wa TANESCO (Mkono & Co Advocates) wailishauri kwamba kutokana na pingamizi hilo, ifunguliwe akaunti maalum (Escrow Account) kwa ajili ya kuhifadhi fedha ambazo zilitokana na Ankara zilizokuwa zinapingwa Kiambatisho Na. 17.
Ushauri huo ulitekelezwa na TANESCO na mnamo tarehe 5 Julai, 2006, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Nishati na Madini (GoT), IPTL na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuzingatia kifungu Na. 6.6 cha PPA, walisaini Mkataba wa kufungua Akaunti Maalum (Escrow Account) kwa ajili ya kuweka fedha zote za ankara zilizopaswa kulipwa kwa IPTL (Kiambatisho Na. 18). Kutokana na makubaliano hayo, fedha hizo ziliwekwa kwenye Akaunti ya ESCROW iliyokuwa inasimamiwa na BOT kama "Escrow Agent". Ikumbukwe kwamba, fedha zilizokuwa zinawekwa katika akaunti ya ESCROW zilikuwa ni za IPTL na wala siyo za Serikali wala TANESCO.
Kwa mujibu wa Kifungu Na. 7.7 cha Mkataba wa ESCROW Akaunti, fedha zilizomo kwenye Akaunti hiyo zingeendelea kuhifadhiwa na "Escrow Agent", hadi muafaka utakapofikiwa kati ya TANESCO na IPTL kuhusiana na mabishano ya ankara. Kifungu hicho kinasomeka, nanukuu:
"In the event of any Dispute between the other Parties hereto resulting in adverse claims or demands being made in connection with the Escrow Account, or in the event that the Escrow Agent in good faith is in doubt as to what action it should take hereunder, the Escrow Agent shall be entitled to retain the Escrow Account until the Escrow Agent shall have received (i) a final award of the arbitrator pursuant to Section 8.6 hereof directing delivery of the Escrow Account (or funds therein) or (ii) a written agreement executed by the other Parties hereto directing delivery of the Escrow Account (or funds therein), in which event the Escrow Agent shall disburse the Escrow Account (or funds therein) in accordance with such order or agreement. Any arbitrator's award shall be accompanied by a legal opinion by counsel for the presenting Party reasonably satisfactory to the Escrow Agent to the effect that such award is final and non-appealable. The Escrow Agent shall act on such award and legal opinion without further question". Kiambatisho Na. 19.
1.2 Usimamizi wa Escrow Akaunti
Kwa mujibu wa Mkataba wa Escrow, BoT ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamamia na kuendesha Akaunti ya Escrow. Kutokana na majukumu yake, BoT, ilipewa mamlaka ya kutoa fedha (Right of Withdrawal) kwa kuzingatia vifungu Na. 4.1, 4.3 na 4.4 vya Mkataba wa Escrow. Pamoja na majukumu mengine, BoT ilikuwa na mamlaka ya kuwekeza fedha za Escrow katika miradi inayoruhusiwa (permitted investments) ya ndani na nje, na kutoa ripoti za mara kwa mara za maendeleo ya akaunti hiyo chini ya kifungu Na. 3.4 cha mkataba wa ESCROW.
Katika kutekeleza wajibu huu, BoT iliwekeza dola za Marekani milioni 22 nchini Ufaransa. Vile vile iliwekeza fedha za Kitanzania shilingi 148,071,613,572.93 katika Hati Fungani (Treasury Bills) za siku 182. Kiasi kingine cha shilingi 8,020,522,330.37, kilikuwa ni salio katika akaunti zilizowasilishwa baada ya uwekezaji kufanyika. Uwekezaji wa nje ulileta faida ya dola 198,544.60, wakati faida katika uwekezaji wa ndani ilikuwa shilingi 5,297,550,682.04.
1.3 Makubaliano ya ukokotoaji wa gharama za umeme
Baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, uliotolewa na Mhe. Jaji Utamwa wa kuiondoa IPTL kwenye ufilisi, na kuitambua PAP kama mmiliki wa asilimia 100 wa IPTL, TANESCO ilifanya mazungumzo na IPTL na kukubaliana kiasi ambacho TANESCO ilikuwa inadaiwa na IPTL (Kiambatisho Na. 20). Baada ya makubaliano kati ya TANESCO na IPTL, Serikali ilisaini makubaliano na IPTL, kuruhusu fedha za Escrow zilipwe kwa IPTL na kuagiza Benki Kuu ya Tanzania kulipa fedha hizo kwa IPTL na kufunga akaunti hiyo (Kiambatisho Na. 21).
Soma pia: Uzi maalum wenye matukio yote yaliyojiri kwenye sakata la ufisadi wa ESCROW
1.4 Kufungwa kwa Akaunti ya ESCROW
Tarehe 21 Oktoba, 2013, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini na IPTL walisaini Makubaliano ya Kutoa Fedha zilizomo katika Escrow Account ili zilipwe kwa IPTL (Kiambatisho Na. 22). Makubaliano hayo yalijulikana kama "Agreement for Delivery of Funds to Independent Power Tanzania Limited". Makubaliano hayo yaliambatana na Muhtasari wa kikao cha pamoja cha uhakiki wa malipo ya tozo kati ya IPTL na TANESCO, pamoja na barua ya Wizara ya Nishati na Madini, ikiwasilisha Makubaliano hayo na kuiomba BoT iruhusu malipo hayo kwenda IPTL kama uhakiki ulivyobainisha, na kwa vile matakwa ya kifungu cha 7.7 cha Escrow Agreement yalikuwa yametekelezwa kikamilifu.
1.5 Kinga dhidi ya Madai na Mashtaka
Baada ya makubaliano kati ya Serikali na IPTL kuhusiana na fedha za ESCROW kulipwa IPTL kwa kuzingatia amri ya Mahakama ya tarehe 5 Septemba, 2013, Serikali kupitia BoT iliitaka IPTL kuweka kinga ya kuhakikisha kwamba baada ya malipo hayo, hakutakuwa na madai au mashtaka yoyote dhidi yake. Na endapo kutatokea madai au mashitaka kuhusiana na fedha hizo, IPTL itachukua jukumu hilo Tarehe 27 Oktoba, 2013, IPTL ilitoa Hati ya Kinga (Indemnity) ambayo iliikinga GoT na BoT dhidi ya madai yote, ya sasa na ya baadaye (Kiambatisho Na. 23). Sehemu ya Kinga ya IPTL inasomeka, nanukuu:
"NOW THIS DEED WITNESSETH that IPTL do hereby agree and INDEMNIFY and keep INDEMNIFIED the Government and the Escrow Agent (jointly and severally) against all present and future claims, actions and legal proceedings that may arise in respect of and/or the losses, charges, costs, and expenses the Government and the Escrow Agent may suffer or incur consequent upon the release and payment of the funds in the aTegeta Escrow Account or part thereof to IPTL purusuant to the Agreement for Delivery of Funds".
1.6 Utoaji wa fedha za Escrow
Fedha za ESCROW zilizotokana na malipo ya capacity charges, zilikuwa katika makundi mawili; Moja ni fedha za Kitanzania na za dola za Marekani. Kufikia tarehe 25 Novemba, 2013, salio katika dola za Marekani, pamoja na faida lilikuwa ni dola 22,198,544.60, wakati salio katika fedha za Kitanzania lilikuwa ni shilingi 161,389,686,585.34, likijumuisha na faida katika uwekezaji ambayo ilikuwa shilingi 5,297,550,682.04. (Kiambatisho Na. 24).
Tarehe 25 Novemba, 2013, BoT iliwasiliana na IPTL, na ilitoa mapendekezo (Kiambatisho Na. 25) kwa IPTL kuhusu namna malipo hayo yatafanyika kwa kuzingatia "macro stability position" ya nchi kama ifuatavyo:-
(i) Kwamba Malipo ya Dola 22,198,544.60 yangelipwa mara moja ifikapo tarehe 26 Novemba, 2013;
(ii) Kwamba umiliki wa hati fungani zilizokuwa hazijaiva uhamishwe kutoka BoT kwenda IPTL;
(iii) Kwamba ulipaji wa uwekezaji huu ufanyike kila hati inapoiva na kama kutakuwa na ulazima wa kuvunja uwekezaji kabla ya muda wa kuiva kufika basi hilo lifanyike baada ya tarehe 1 Januari, 2014 ili kuepuka kuongeza ujazi uliopitiliza wa fedha katika uchumi, hasa katika mwezi wa Desemba, 2013; na
(iv) IPTL itoe taarifa za kibenki ili kuwezesha uhamishaji wa fedha zilizotajwa katika kipengele (i) hapo juu kwenda IPTL.
IPTL kupitia barua ya tarehe 25 Novemba, 2013 ilikubaliana na mapendekezo ya BoT (Kiambatisho Na.26). Aidha katika kikao cha pamoja kati ya BoT na IPTL cha tarehe 26 Novemba, 2013 (Kiambatisho Na. 27) ilikubalika kwamba:-
(i) Baada ya kupokea maelekezo kutoka IPTL, BoT itashauri juu ya utaratibu unaotumika katika kuhamisha umiliki wa hati fungani (Treasury Bills); na
(ii) IPTL iwasilishe barua ya maelekezo ya kuhamisha fedha zilizokuwemo katika Escrow Account. Barua hiyo ihusishe pia maombi ya kuhamisha hati fungani.
Baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa tarehe 5 Septemba, 2013 IPTL, kupitia barua ya tarehe 28 Novemba, 2013 (Kiambatisho Na. 28), ilielekeza Benki Kuu ya Tanzania ilipe fedha za ESCROW kwa IPTL na kumaliza mgogoro uliokuwepo.
1.7 Ulipaji wa fedha za ESCROW kwa IPTL
Kutokana na maelekezo ya IPTL, tarehe 28 Novemba, 2013 fedha taslimu, dola za Marekani 22,198,544.60 na shilingi 8,020,522,330.37 zililipwa katika Akaunti iliyotolewa na IPTL kama ilivyooneshwa hapo juu. Tarehe 5 Desemba, 2013 BoT ilihamisha Hati Fungani (Treasury bond) yenye thamani ya shilingi 153,369,164,254.97 kwenda IPTL na kuhitimisha jukumu la BoT la kuwa Escrow Agent. Tarehe 19 Desemba, 2013, BoT iliiomba Wizara ya Fedha kufunga rasmi Escrow Account, kwa vile madhumuni ya kufunguliwa kwake yalifika mwisho (Kiambatisho Na. 29).
1.8 Kufungwa kwa Akaunti ya ESCROW
Kufuatia maombi ya BoT kwenda Wizara ya Fedha ya kufunga Akaunti ya ESCROW yaliyozingatia kuisha kwa mgogoro kuhusu mali ya Uwekezaji na kwa kuzingatia uamuzi wa Mahakama, mwezi Desemba 2013 Akaunti ya ESCROW ilifungwa rasmi (Kiambatisho Na. 30).
1.9 Malipo ya TANESCO kwa IPTL
Wakati wa kufunga akaunti ya ESCROW mwezi Desemba, 2013 TANESCO ilikuwa ikidaiwa na IPTL jumla ya dola za Marekani milioni 79.05 sawa na shilingi bilioni 125.04 zilizotokana na ununuzi wa umeme (Capacity Charge) ambazo hazijalipwa.
Chanzo: Chief Isike na Nyaraka ya Siri kutoka serekalini.