Yajue yote kuhusu ESCROW AKAUNTI

Yajue yote kuhusu ESCROW AKAUNTI

Tatizo ni kukimbilia jf kuanzisha thread.
Sasa wakague pesa gani wakati zimeshakwapuliwa!?
Na hata kama ni justification, pesa zilitolewa bila kufuata taratibu na kama ulimsikiliza Prof. Mwandosya kwa umakini Bungeni alisema wazi kuwa BoT ni mali ya umma na irregulalities zozote za kutoa pesa ni uhalifu.
Lakini.... PAP does not exist na hao walioidhinisha walijua hilo ndio maana BRELLA wana signs tu bila majina ya signatory alafu unaongelea kwenda tena kwa CAg badala ya kwenda INTERPOL au polisi!
 
Njia bora ya kumaliza utata juu ya umiliki wa fedha za Tegeta Escrow Account ni vyema IPTL na TANESCO wawasilishe mahesabu na nyaraka zote zinazothibitisha madai yao kwa CAG ili atoe tamko rasmi kama fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow ya Tegeta ni mali ya IPTL au umma.

Mkuu mangaukawa, kama huyo CAG hakupitia nyaraka zote ulizotaja kabla ya kukabidhi ripoti yake rasmi basi naye atapaswa aundiwe "Tume ya kumchunguza"!!!
 
Kwanini fedha za TANESCO zikae akaunti ya escrow?

Akaunti ya Escrow ya Tegeta kati ya Serikali ya Tanzania na IPTL ilifunguliwa Benki Kuu kwa lengo la kushughulikia mzozo wa malipo ya tozo ya uwekezaji ("capacity charges") ambayo TANESCO ilitakiwa kuilipa IPTL. Ilidaiwa kuwa hata baada ya usuluhishi wa ICSID mwaka 2001, IPTL ilikuwa inatoza gharama kubwa zaidi kuliko ilivyotakiwa. TANESCO kujiepusha na gharama hiyo kubwa ikalazimika kutangaza mgogoro wa malipo ya tozo ya uwekezaji na IPTL.
Mwaka 2006 pande zote zilikubaliana kuwa "Escrow Account" ifunguliwe Benki Kuu ili TANESCO iwe inafanya malipo kwenye akaunti hiyo badala ya kuilipa IPTL moja kwa moja. Ilikubaliwa pia kuwa kungefanyika mahesabu kuonyesha ni kiwango gani kilikuwa halali kulipwa na TANESCO. TANESCO walipaswa kulipia tozo ya uwekezaji ("Capacity charges"), kwa kiwango kilichokubaliwa na Mahakama ya ICSID mwaka 2001 cha dola za Marekan milioni 2.6 kwa mwezi badala ya Dola za Marekani milioni 3.6 kwa mwezi. Hadi sasa maamuzi ya ICSID ya 2001 hayajatenguliwa.
 
Tafsiri kuwa akaunti yoyote iliyo Benki Kuu ni lazima iwe na fedha za Serikali tu haiwezi kutumika katika Tegeta "Escrow Account" kati ya IPTL na Serikali kwa sababu ni dhahiri kwamba fedha hizo ni tozo ya uwekezaji ("Capacity charges") kwa IPTL. Fedha hizo ni wazi kwamba ni za mlipwaji ambaye ni IPTL na si ya mlipaji ambaye ni Serikali. Ni vizuri kukumbushana pia kuwa ziko "Escrow Accounts" nyingine Benki Kuu kwa sasa hivi ambazo zina fedha ambazo siyo za Serikali.
 
Njia bora ya kumaliza utata juu ya umiliki wa fedha za Tegeta Escrow Account ni vyema IPTL na TANESCO wawasilishe mahesabu na nyaraka zote zinazothibitisha madai yao kwa CAG ili atoe tamko rasmi kama fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow ya Tegeta ni mali ya IPTL au umma.
Haina maslahi kwa mtanzania. Tunachohitaji ni tuelezwe kwa nini IPTL/PAP wameongezewa mkataba wakati mkataba wao ulikuwa unafikia ukomo 2015? Nani aliwezesha mchezo huo mchafu!
 
Kumejitokeza tafsiri kuwa iwapo kuna fedha zimewekwa kwenye akaunti yoyote katika Benki Kuu ya Tanzania, basi fedha hizo ni lazima ziwe za Serikali au za Umma. Tafsiri hii si sahihi. Akaunti ya Escrow ya Tegeta iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania, kushughulikia masuala ya IPTL na TANESCO. Mazungumzo yaliyokamilishwa katika mijadala iliyoendelea katika Bunge la Tanzania kikao kilichomalizika Novemba mwaka huu yalitoa tafsiri kuwa fedha yote inayowekwa kwenye Escrow Account iliyofunguliwa Benki kuu ya Tanzania ni mali ya Serikali au Umma wa Tanzania. Hiyo tafsiri sio sahihi na inaweza kuwatisha wale wanaotaka kufanya biashara hapa nchini.
 
Back
Top Bottom