Yajue Mataifa Yasiyoamini Uwepo wa Mungu

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,258
13606710_1556609547978896_2546632004266029989_n.jpg


HAKUNA MUNGU??? ZIJUE NCHI ZENYE WAPAGANI WENGI DUNIANI...............
Nimekutwa na tukio la kupotezana na rafiki yangu Mholanzi baada ya kumuuliza DINI yake alikasirika sana.......na nimegundua ni swali linalochukiza wazungu wengi siku hizi kwa kila uchao ....CHONDE Usithubutu na wewe kama hamna mahusiano ya KIROHO
Utafiti Unaonesha kwamba 63% ya watu duniani wanaamini uwepo wa Mungu, yafuatayo ni Mataifa yasiyoamini uwepo wa Mungu (Atheism). Yasemekana kiwango cha watu kuwa na imani na dini na uwepo wa Mungu kinazidi kupungua duniani huku makanisa mengi hasa Ulaya yakigeuzwa kuwa majumba ya starehe japo pia yasemekana kwamba watu wanatumia teknolojia zaidi hasa luninga kusikiliza mahubiri majumbani mwao huku wakituma sadaka kwa njia ya miamala kama za M-Pesa ama tiGO-Pesa
Wazungu wengi ambao ndio walisambaza dini huku Afrika kwa njia ya Umishenari wanaamini kwamba Dini ni jambo la kufikirika na kuogofesha tu ili kupunguza maovu duniani na kuwanyima watu KULA BATA huku wakiwakamua mapato yao kwa njia ya kinachoitwa ZAKA NA SADAKA....
1. Asilimia 75 ya Wachina hawana dini kutokana na kuaminishwa na Mao Zedong kuzama kwenye Ukomonist mwanzoni mwa miaka ya 70. Wachina wengi wanaamini katika 'CONFUCIUS' huku wakila chochote kilicho mbele yao, hata hivyo hali hii inasemekana kusababishwa na wingi wa watu nchini humo usioendana pengine Tanzania tunachagua kwa sababu bado tupo wachache na chakula kipo tele huku tayari Raisi wa Malwi akiamuru watu wale kula panya na panzi kwa kuwa wanapatikana kwa wingi nchini humo
3. Wajapani wengi hawajielewi na wengi wao wana dini zaidi ya moja yaani unaweza Ijumaa ukamkuta Msikitini, Jumamosi Usabatoni na Jumapili pia anazama kanisa lolote.
4. Huku Raia wengi wa Vietnam wanaabudu babu zao, yaani siku akijisikia kuabudu anakwenda kwenye kaburi la Babu yake anakula gombo na kurudi nyumbani. ....Ilihali Wahindi wengi wakiabudu wanyama aghalabu Ng'ombe kama Mungu wao
2. Jamhuri ya Czech ......wao wanaamini zaidi kwenye Ukomunisti, ni asilimia 21 tu wanaoamini uwepo wa Mungu....Hii pia imechangiwa na makatazo ya watawala wa kikomunisti tangu enzi za akina Milosovic ingawa wengi wa walioulizwa ni kama walikua hawajielewi kama wana dini ama la
2.2) Sweden & 3) Denmark. asilimi 17 tu ndio wanaamini kwamba Mungu Yupo na hii inawarahishia kutoishi bila hofu na kutenda dhambi yoyote waitakayo..........Waswidi na Wadenish wengi wamegeuza baa kuwa ndio 'makanisa yao'
5. United Kingdom (40% wenye dini) na Ufaransa (41%) na kwingineko kwenye nchi nyingi tu za ulaya magharibi na mashariki...Wanawake na Wazee tu ndio husali huku vijana wengi wakiendelea kula bata na kugeukia ushoga na usagaji ......Kuna marafiki zangu ni wafaransa hakika hawajui kitu chochote kinachohusiana na Mungu, si biblia wala Quran huwa hawaabudu kitu chochote
7. Hongkong pia ni moja ya nchi yenye wapagani wengi duniani (52%)...............nyingine zikiwa ni Norway (39%), Austria, Israel, .....


13566917_1556609614645556_7722403906168097730_n.jpg

 
Hiyo namba mbili nimeikubali watakuwa na karama za kufa mtu manake MUNGU! akitoka kusikiliza waislamu anakumbana na majamaa usabatoni akifikiri mi jamaa imekosea anakumbana nayo tena sunday tena makanisa mbadilisho! Duuh! Hatari
hao ndio maana labda wako mbali sana
 
Kwa hiyo mpaka huko ulaya kuna m pesa na Tigo pesa hatari Sana, VP kuhusu Tanzania?
sheria ya takwimu inanibana Tanzania lakini inasemekana wapagani na dini zingine ukiacha ukristu na uislamu ni 30%
 
Hilo tumemaliza, nauliza habari za dini hapa tz we unaonaje ndugu mchambuzi?
nimekujibu tayari ila kwa tathmini hata Bongo wahubiri wengi wananyang\anyana wafuasi kwa sasa inategemea karata zako unazichangaje
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom