Yahya Jammeh atangaza hali ya hatari

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
12,695
52,319
Yahya Jammeh ametangaza hali ya hatari nchini Gambia.

Amesema yeye ndiye rais ni mpaka uchaguzi mwingine utakapifanyika.

Amesema maandamano hayataruhusiwa.

Hiyo inatokea kabla ya siku moja muda wake wa kukaa madarakani ukiwa umebakiza masaa 24.

Mikusanyiko na maandamano ni marufuku.

Chanzo: BBC
 
Kuna haja ya umoja wa nchi za Kiafrika kuondoa hii aibu kwa kumtoa kwa nguvu madaraka, Aibu kubwa kwa viongozi wa nchi za kiafrika Shame on them.
 
Kuna ruwaza naiona hapa.
Mtoto wa raisi mchaguliwa anafariki kwa kung'atwa na mbwa.
Kisha Yahya anajitokeza na kutangaza hali ya hatari, huku akiwahi kuaminisha raia kua yeye ni mchawi wa wachawi.

Anatumaini kile kifo kimeleta hofu ya kutosha kwa wananchi mpaka waogope kumpinga, hata kama hahusiki nacho.
 
Uchawi wake umefika mwisho hawezi cheza na nguvu ya umma akamuulize Gagbo kilichomkuta wananchi walitaka kumchomea ikulu hadi alipokuja kuokolewa Kwa helicopter na wafaransa.Kuna maisha baada ya uongozi angeachia Kwa amani tu.Naona the Hague inamuita.
 
Ngoja tuone kama atapigwa na hizi nchi za West maana zilitishia kumtoa kwa nguvu kama atazingua.
 
Naona kaamua kufa kiume.
Sio kaamua kufa kiume. Yeye na Museveni hawana utofauti. Aliingia madarakani kwa mapinduzi (mtutu), anataka kutolewa kwa mapinduzi (mtutu). Ndio siri kubwa ya madikteta kote ulimwenguni. Kamwe hawaamini katika boksi la kura.
 
Back
Top Bottom