Yahya Jammeh apewa muda wa mwisho mpaka leo mchana

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wamempa muda wa kuondoka iwe mchana wa leo Rais alieshindwa wa Gambia Yahaya Jammeh awe ameachia ofisi ikulu ili mwenzake alieshinda aanze kazi.Mwenyekiti wa Ecowas Marcel Allain de Souza amesema muda aliopewa ukipita hakutakua na mazungumzo tena bali ni kumvamia kijeshi.

Rais wa sasa Adama Barrow aliapishwa jana Alhamisi. Majeshi ya Ecowas yanayoongozwa na Senegal tayari yameingia nchini Gambia na yamepewa amri ya kuwa tayari kuvamia Ikulu na kumtoa kwa nguvu ukipita muda wa mwisho aliopewa Yahaya Jammeh
 
Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wamempa Rais alieshindwa wa Gambia Yahaya Jammeh awe ameachia ofisi ikulu ili mwenzake alieshinda aanze kazi.
Rais wa sasa Adama Barrow aliapishwa jana, Majeshi ya Ecowas yanayoongozwa na Senegal tayari yameingia nchini Gambia na yamepewa amri yabkuwa tayari kuvamia ukipita muda wa mwisho aliopewa Yahaya Jammeh
Na hawa wababaishaji, wajumbe elfu na moja wamekuja, amekataa, wanambembeleza nini? Ameua wangapi? ameua sana! Just kill him also, he has killed many innocent civilians
 
Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wamempa Rais alieshindwa wa Gambia Yahaya Jammeh awe ameachia ofisi ikulu ili mwenzake alieshinda aanze kazi.
Rais wa sasa Adama Barrow aliapishwa jana, Majeshi ya Ecowas yanayoongozwa na Senegal tayari yameingia nchini Gambia na yamepewa amri yabkuwa tayari kuvamia ukipita muda wa mwisho aliopewa Yahaya Jammeh
Igwe keep us posted
 
Hivi viongozi wa Afrika mbona hawana uchungu na wananchi wao jamanii....hivi angeondoka mapema angepungukiwa nini
 
Ukisikia sikio la kufa halisikii dawa ndo hii sasa unapewa fursa ya kuishi salama hutaki.
 
Yaani huyo Mkuu anafuata nyayo za Laurent Gabgo wa Ivory coast alitolewa kwa aibu sana
 
Mwenye Enzi Mungu atuongoze waafrika milele yote. ..Amen RA
 
Haaahaaa!!! Nimeona mseven povu linakutoka kwenye ukurasa wake wa tweter amesema Gambia ni nchi huru si vema kuivamia kijeshi!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom