turashashe jr
Member
- Dec 25, 2014
- 45
- 35
Siku hizi kuna maji ya upako vitambaa vya baraka nk nk imani imehamia kwenye vitu vya kidunia kuliko uchaji wa rohoni
Siku hizi mtu akihubiri vizuri madhabahuni anatunzwa na kwakweli mahubiri yenyewe si lolote bali mipasho
Siku hizi huna haja hata ya kwenda kanisani unafungulia TV halafu unamwangalia kidume anavyomwaga mbwembwe kishapo anaweka namba za simu halafu unatuma sadaka/ mchango wako naye anakuombea
mtaani kwetu lilikuja kanisa la mungu bendera,
acha wamama walivyopapatikia,
wanaambiwa wapeleke mafuta ya vaseline
ili wakapwe eti kuondoa mikosi,
sasa uliza hayo mafuta wanapakwa wapi, ni aibu.
Umeongea ukweli yani hadi inakera wakristu wamekua bendera fuata upepo,neno lnasema jaribuni kila roho inayodai inatoka kwa Mungu siyo unaenda tuu kama gari bovu
yani haya makanisa haya ndiyo maana yanendeshwa na matukio ... kwa sasa wapo kwenye ulingo wa siasa ,.. wizi tu
sio wote tutake radhi tasvali !!
anti walikuwa wanapakwa wapi?
Umenikumbusha mchungaji mmoja mwaka 2010 alikuja kwa mzee Wangu apate dawa za mvuto na kuwa na nguvu ktk kanisa lake tena alikuja na wanasiasa 2 ni maalufu sana hapa mjini basi mzee wangu akawambia kazi zao zote zinafanyika usiku maeneo ya makabulini kunduchi ilipofika usiku wa saa sita tukaenda wote nikiwemo na Mimi mwenyewe basi kufika makabulini ikanyunyizwa dawa kwenye makabuli 2 ya dini yake yakasemwa maneno flani pale ya lugha maalum Mara yakafunguka ukatoka moto mkubwa sana ukiambatana na radi nusra jamaa wakimbie basi tukaona watu wanatoka mle na kuuliza kwa lugha ileile aliyoongea mzee wangu akawatajia Shida za wale jamaa wote watatu wakaambiwa wavue nguo pale pale wasogee basi wakafanya kama walivyoelekezwa na wale watu wakaanza na yule mchungaji kwa nguvu alizokuwa anataka akapewa ila kwa makubaliano maalumu na wale wengine ambao mmoja ni mbunge maarufu wa upinzani na mwingine sasa ni wazili wakafanyiwa vile walivyoomba kazi ikawa imekwisha mchungaji ana kanisa bagamoyo road linajaza huwa nawaonea huluma waumini mana wana abudu wasichokijua na nikikutana nae nikumtania mana najua nguvu sio ya mungu yeye huniambia namshukulu malehemu mzee wako nisingekuwa tajiri kama sio yeye
Siku hizi kuna maji ya upako vitambaa vya baraka nk nk imani imehamia kwenye vitu vya kidunia kuliko uchaji wa rohoni
Siku hizi mtu akihubiri vizuri madhabahuni anatunzwa na kwakweli mahubiri yenyewe si lolote bali mipasho
Siku hizi huna haja hata ya kwenda kanisani unafungulia TV halafu unamwangalia kidume anavyomwaga mbwembwe kishapo anaweka namba za simu halafu unatuma sadaka/ mchango wako naye anakuombea
na ni kweli wizi mtupu, maana hawa akina gwajima miaka michache walikuwa watu wa kawaida sana sasa hivi ni matajiri wa kutupa kwa wizi wanaoufanya kwa waumini wao.
kwani hata pana jina basi,
ni hekaheka tupu.
duuu nawe....! Lol