Yahusu Demokrasia

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Ni matumaini yangu kwamba nitakachoandika hapa leo kitakuwa ni chenye manufaa na chenye kunyanyua uwezo wa akili na kufikirisha.

Tafakuri yangu ni kuhusu nchi ya demokrasia. Na ninadhani ya kwamba sisi kama watanzania kwa umoja wetu tumedhamiria kujenga nchi ya namna hiyo na huo ndio muelekeo wetu kama taifa.

Na mawazo yetu yanapaswa kuongozwa katika mkondo huo. Ambao ndio msingi mkuu wa kulinda uhuru wa watu. Na tunapaswa kujua kwamba misingi ya demokrasia ni ipi ili tuweze kujenga msingi hiyo katika mioyo ya watu. Kwasababu watu wanapaswa kufahamu demokrasia ni nini na watashiriki vipi katika ujenzi wake.

Pamoja na kwamba nchi yetu inasema kwamba ni ya kidemokrasia bado tuna changamoto nyingi ili kufikia huko. Baadhi ya changamoto hizo ziko katika serikali na nyingine ziko kwa wananchi . changamoto ambazo ziko kwa wananchi ni kwamba waliowengi hawajitambua vya kutosha ama kuwa na elimu ya kutosha ya utaifa na ushiriki wao katika ujenzi wa utaifa na uzalendo. Lakini hili nadhani ni wajibu wa serikali kulifanya kama tumedhamiria kwa dhati kujenga nchi ya kidemokrasia.

Watu wanadhani kujenga utaifa ni kujenga majengo si kweli ni kuunganisha watu kwanza, lakini pili kuelekeza akili na mioyo ya watu kujenga taifa ili kufikia malengo tuliyojiwekea. Utaifa ni watu. Na taifa imara ni taifa ambalo watu wake ni wamoja. Taifa ambalo watu wao mawazo yao yamegawanyika katika ubinafsi na sio utaifa haliwezi kuendelea. Katika taifa kuna weza kuwa na mawazo yaliyo gawanyika lakini ni katika malengo chanya ya ujenzi wa utaifa na taifa na sio ubinafsi.

Kwahiyo tuna taifa ambalo kikundi cha watu wanadhani wana mamlaka ya kutawala wengine na mamlaka hayo hayapaswi kuondoka mikononi mwao.
Hivyo hufanya mbinu zozote ili wabaki madarakani. Na kama wana fikra hizo uhuru wa kweli bado hatujaufikia.

Demokrasia ya kweli haiwezi kufikiwa kama watu wana mawazo ya namna hii. Tunatakiwa kubadili mwelekeo wa mawazo yetu. Demokrasia ya kweli watu ndio wenye uamuzi na mamlaka ya mwisho ya hatma ya nchi yao.

Sasa hivi tunaona polisi wakitumiwa kama chombo cha kulinda chama fulani na kukikandamiza kingine. Nadhani huu sio mwelekeo mzuri kwa uhuru na hatma ya demokrasia nchini. Ni matumizi mabaya ya jeshi la polisi. Wanaofanya hivi wanastahili kuwajibishwa.

Jeshi la polisi linapaswa kufuata sheria zinasemaje na kuwa neutral. Kwasababu hii ina madhara makubwa na tumeishaona kwamba imeishajenga uhasama kati ya wananchi na polisi wao ambao kwa hakika wanajukimu la kuwalinda na sio kujiingiza kwenye siasa. Jukumu lao ni kuhakikisha sheria zinafuatwa. Na watu walio madarakani wanapaswa kufuata sheria. Na sio kutumia uwepo wao madarakani kukandamiza haki na uhuru wa vyama vingine.

Tunajua demokrasia inahitaji nidhamu. Inahitaji watu waliopevuka kiakili na kuelimika ambao wanauwezo wa kufanya maamuzi yenye hekima kwaajili ya hatma ya nchi yao. Na uhuru wa watu unalindwa vyema katika mazingira ambayo kuna demokrasia. Ambayo yanafanya uwepo uhuru wa fikra, Majadiliano, kuandika na kutoa mawazo yako kwa uhuru.

Na kama tunapenda kuwa huru tunapaswa kulinda demokrasia. Huku tukijua katika uhuru kuna wajibu. Kwamba tunawajibika kwa wengine na future ya taifa hili. Tunahitaji watu wetu kupevuka kiakili na kujua kilicho muhimu kwa taifa lao na kuvua vazi la ubinafsi. Na kujua kwamba majaliwa ya taifa hili yanamtegemea kila mmoja wetu.
 
Back
Top Bottom