Yahoo yadukuliwa taarifa za watumiaji wake

Yahoo yadukuliwa taarifa za watumiaji wake

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Mtandao wa Yahoo umethibitisha kuwa wadukuzi wamedukua taarifa za zaidi ya watumiaji milioni mia tano katika akaunti zake za watumiaji.

Hata hivyo Yahoo imesema inaamini kuwa shambulio la kimtandao la mwaka 2014 lilikuwa limefadhiliwa na serikali.

Data zilizoibwa ni pamoja na majina, anuani za barua pepe, namba za simu, tarehe za kuzaliwa na nywila za watumiaji ama (Password). Lakini wadukuzi hao hawakugusa kadi za malipo na taarifa za akaunti za kibenki.

Watumiaji wa mtandao huo wameshauriwa kubadilisha nywila zao (password) zao ili kuepuka udukuzi wa kimtandao.

yahoo.jpg

xyahoo-logo.jpg.pagespeed.ic.dFjkGoMqpS.webp
 
Washenzi wametuma picha ya passport ya Michelle Obama mtandaoni!

Myspace 117 milioni walidukuliwa mwaka 2011

Tumblr watumiaji 65 milioni mwaka 2011

Ashley Madison watumiaji milioni 32 mwaka huu

Udukuzi bado unaendelea kimyakimya, watu wajihadhari.
 
Back
Top Bottom