Yah: Uyoga, Vipepeo na Midoli Bunge la Watanzania

Na kwa nini JF ifungiwe? Kwani TBC imefungiwa? Nijuavyo mimi Serikali imesema Bunge litarekodiwa na kuonyeshwa jioni na kurudiwa wkend sasa sijui tatitzo liko wapi hapo?

Na hii siyo TZ peke yake nchi nyingi Duniani hata zile tunazoziiga kwa mambo ya kiutawala ambazo kila siku hulaumu Serikali yetu kwa nini haifanyi kama wao hufanya hivi kwamba Bunge huonyeshwa jioni!

Marekani kuna chanell maalum ya bunge ambayo hurusha live mijadala so usiongelee jambo usilojua.Pili tusiwe double standards,kama tunasema kurusha live ni gharama basi serikali iiagize TBC kutokurusha matangazo yoyote live kwasababu tunabana matumizi,hii ijumuishe sherehe za kitaifa,dhima na hata hotuba za Rais na matukio mbalimbali yanayofanywa na serikali yarekodiwe na kuja kurushwa usiku,hapo tutaona dhamira ya kweli ya kubana matumizi.
Posho za wabunge kwa mwaka ni zaidi ya bilion 15,kwanin tusianze hapo tuzifute.Mwenge,madc na marc ni mzigo kwa taifa,kwanin tusiwafutilie mbali kubana matumizi?
uchaguzi zanzibar ni zaidi ya bilion 9,kwann tusirudie uchaguzi ili kubana matumizi?

NB;Hata kama matangazo hayatarushwa live,haina maana tutaokoa hiyo bilion 4 yote,no just a small fraction of it.
 
sihitaji mashoga kama wewe, kabanjuliwe na mandingo
Kama baba yako anavyobanjuliwa , au siyo?
b6edd597a778aa0e51c165e1c461f0d2.jpg
 
Bungeni-Dodoma.jpg

Ugomvi wa Kifikra: Mojawapo ya upotoshaji mkubwa uliotokea ni kuwaaminisha watu kuwa ipo haki fulani inaitwa "ya kupata habari live". Kwamba, usipopata habari "live" basi haki yako hiyo imevunjwa. Haki hii haipo mahali popote duniani, na haijawahi kutambuliwa na serikali yoyote duniani! Hakuna haki ya kupata habari "live"!


Ipo haki ya kupata na kutoa habari. Haki hii ni miongoni mwa haki za msingi za binadamu. Haki hii imeanishwa katika Azimio la Wote la Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Binadamu la 1948 (Kifungu cha 19) ambalo nchi nyingi duniani nazo zimeikubali.


Tanzania nayo inatambua haki hii na tumeiweka Katika Katiba yetu Ibara ya 18. Haki ya kupata habari ni haki ya msingi ya binadamu, kwamba huwezi kumnyima mtu habari. Ningekuwa miongoni mwa watu ambao wamekasirika na kuja kuu kama Serikali ya Magufuli ingedai au hata kupendekeza kuwa Watanzania wasiambiwe au wasisikie kinachotokea Bungeni. Ningeungana na wengine kupinga vikali endapo angesema kuwa Serikali imeamua kuwa kuanzia sasa habari za Bunge hazitawekwa wazi kwa wananchi. HIlo lingekuwa ni kuvunja Ibara ya 18 ya Katiba na kwenda kinyume na Azimio la Umoja wa Taifa la Haki za Binadamu ambayo Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoliridhia.


Kama Magufuli na Serikali yake wangekuja na pendekezo kama hilo nina uhakika kesi rahisi kabisa ya Kikatiba ingeweza kufunguliwa dhidi ya uamuzi huo na kwa asilimia 100 Serikali ingeshindwa.


Binafsi naamini ipo haki kubwa zaidi ambayo inatishia Watanzania kupata habari sahihi kutoka kwa wawakilishi wao Bungeni. Wabunge wamechaguliwa na wananchi kuwawakilisha Bungeni; nii ni pamoja na kushiriki mijadala, kutoa maoni, kusimamia serikali, lakini kubwa zaidi kutunga sheria na kubadilisha sheria mbalimbali. Mbunge ambaye haendi Bungeni, au ambaye anatoka Bungeni kwa sababu tu hajapenda uamuzi fulani wa Kiti cha Spika au kupinga maamuzi fulani ya kisiasa anawanyima wananchi waliomwakilisha kupata habari sahihi - kwani akija na kuulizwa kuhusu jambo ambalo yeye hakuwepo Bungeni hawezi kutoa habari sahihi na hivyo atakuwa anawanyima wananchi haki yao chini ya Ibara ya 18 ya Katiba na chini ya Azimio la UM la Haki za Binadamu.

Ndugu zangu, kama kuna sababu ya wabunge kulumbana na kucharuka ni kuhusiana na wao kutokuwepo “live” Bungeni wakati mijadala mbalimbali inafanyika na wao kutoa mawazo au kutoa hoja na kupendekeza Sheria au Mabadiliko ya Sheria mbalimbali Bungeni. Kuna faida gani kwa wananchi kuona kinachotokea Bungeni “live” kama wale waliowatuma huko Bungeni hawapo “Live”. Mwananchi wa jimbo fulani atafurahia nini kuona Bungeni kinachofanyika “live” wakati Mbunge wa jimbo lake hayupo “live” Bungeni?

Mwananchi ambaye anamuuliza Mbunge wake kuhusu suala fulani ambalo alitakiwa awe ametolea maoni nay eye hakuwepo “live” Bungeni atafaidika nini kuambiwa kuwa ameona jinsi watu walivyozungumza kwa ukali mambo ambayo yeye hayamgusi na mbunge wake hakuwepo Bungeni? Hili ndilo jambo hasa la kulizungumzia.

Binafsi, ningekuwa na uwezo nisingejali sana hili la kuona au kutoona “live”; ningejali zaidi kile kinachofanyika “live” Bungeni hata kama mimi mwenyewe sioni kwa macho! Kwa sababu macho siyo chombo cha kuaminiwa sana kwa kukupa taarifa sahihi; vinginevyo, mazingaombwe yangekuwa yanaamini ni ukweli. Kuona tu haitoshi; tunataka tujue nini kinafanywa na wabunge wetu Bungeni.

Lakini ningeenda mbali zaidi; na ninatumaini Serikali ya Mabadiliko ya J.P. Magufuli itakuja na mabadiliko ya sheria ambayo wabunge wote watafurahia ambayo yataweka adhabu kwa wabunge watoro Bungeni. Kama wafanyakazi wengine kwenye makampuni wanapewa kiasi tu (limited) cha siku ambazo anaweza kusema alikuwa mgonjwa wabunge nao wapewe siku (na zisizidi siku saba) kwa mwaka (ambapo kikao cha Bunge kinafanyika) ambapo ataweza kutoa udhuru kuwa hawezi kuwepo Bungeni. Isipokuwa kwa Mbunge ambaye yuko mahututi amelazwa au amepewa leave na Daktari kwa muda fulani. Wengine wote watatakiwa wawepo Bungeni au kwa kila siku, saa ambayo hawapo wakati vikao vya Bunge vinafanyika “live” watakatwa kwenye mishahara yao shilingi 50,000 kwa kila saa ambayo hawapo Bungeni au kwenye vikao ambavyo wanatakiwa wawepo. Hatutaki tuone Bunge “live” tunataka tujue wabunge wako “live” bungeni – mbele ya Luninga au hata nje ya luninga!

Nje ya hapo, ni lazima tukatae sanaa za maigizo ambazo zinajaribu kuwashikisha Watanzania wanasesere na kuwaambia waimbe “mtoto, mtoto!” na wengine kweli wanadakia “ni mtoto mtoto!” ati kwa vile mdoli huyo unafumba na kufumbua macho na unacheka kwa sauti zinazotokana na spika zinazoendeshwa na betri tumboni! Wakati wa kuwalazimisha Watanzania washike vipepeo na kuimba “uyoga uyoga” umepita! Tusiwafanye watu wetu waamini haki ambazo hazipo zipo na zile haki zenyewe za msingi wasijue kuwa zipo na wanatakiwa kuzidai!

Lakini kuna kubwa zaidi; kama kweli Wabunge wanataka kulazimisha kitu fulani kifanywe na chombo cha serikali ni wao wenye jukumu la kutunga sheria na kutenga fedha kwa chombo chochote cha serikali. Kama Nape ameona kuwa ni gharama kubwa kurusha vipindi “Live” badala ya kususa na kukasirika wabunge wanaweza hata kutoa hoja ya dharura ikajadiliwa Bungeni na kuamuliwa ili Serikali ipeleke fedha za ziada kwa TBC ili irushe Bunge live. Na hata Bunge likirushwa “live” masaa 24 – wabunge wawemo au viti tu vinavyozunguka zunguka – bado Watanzania watakuwa wanadai haki yao ya kuona wabunge wao wapo Bungeni “live” na wanashiriki ipasavyo kwenye mijadala muhimu na inayogusa maisha yao.

Mengine haya ni vipepeo na uyoga tu! Sidandii hata.

MMM
I can say more! Umemaliza hii ndio point yaani unatoka nje kisa tu kutooonekana??? seriously?!?!?! Na ni kweli iwekwe sharia ya kuwawajibisha watu. Inakuwaje watu wananfanya wanayotaka. Walimu wana mwangapi alikini hawagomi kuwafundisha watoto wetu?? No this is more than enough. Watanzania tuamke!
 
Marekani kuna chanell maalum ya bunge ambayo hurusha live mijadala so usiongelee jambo usilojua.Pili tusiwe double standards,kama tunasema kurusha live ni gharama basi serikali iiagize TBC kutokurusha matangazo yoyote live kwasababu tunabana matumizi,hii ijumuishe sherehe za kitaifa,dhima na hata hotuba za Rais na matukio mbalimbali yanayofanywa na serikali yarekodiwe na kuja kurushwa usiku,hapo tutaona dhamira ya kweli ya kubana matumizi.
Posho za wabunge kwa mwaka ni zaidi ya bilion 15,kwanin tusianze hapo tuzifute.Mwenge,madc na marc ni mzigo kwa taifa,kwanin tusiwafutilie mbali kubana matumizi?
uchaguzi zanzibar ni zaidi ya bilion 9,kwann tusirudie uchaguzi ili kubana matumizi?

NB;Hata kama matangazo hayatarushwa live,haina maana tutaokoa hiyo bilion 4 yote,no just a small fraction of it.


Kwa hiyo kama Marekani wanarusha moja kwa moja na sisi ndiyo tufanye hivyo? Mbona Singapore, Uingereza, AK n.w wanarekodi kama sisi tunavyotaka kufanya?
Yaani wanarekodi na kuonyesha usiku tena mara nyingi ni kama kuna vipindi maalumu vya Bunge ambavyo wao wanaona ni muhimu mbon,a Wabunge wao wa Upinzani hawagomei na ktk nje kwa kuwa hawaonekani kwenye TV live?

Kuhusu fedha za kukatwa Posho za Wabunge hilo swali ulipaswa uwaulize hao Wabunge vilaza wanaoharibu Bunge kwa siku nzima wanatoka nje lkn wanachukuwa laki tatu kila mmoja wao kwa kutokufanya kazi kabisa yaani wanakuja asubuhi wanachukuwa laki tatu (300 000) halafu wanarudi nyumbani kulala, na hawa ndiyo watunga sheria wetu hivyo ulipaswa uwaulize hilo swali labda watakupa jibu la kukuridhisha!
 
Mzee mwenzangu siku za hivi karibuni umebadilika sana hawa vijana wamekuwa sio wale wa kukuheshimu kama zamani
Anyway heshima sio jambo la muhimu kwako hilo najua najua pia umewahi kusema huyumbishwi kwenye misimamo yako ila kwa kweli kwa hili umetereza
Labda nikwambie tu
Serikali ya chama cha mapinduz ina sababu zake tofauti kutoonyesha live matangazo ya bunge tofauti na inavyotetea uamuzi wake wa kupunguza gharama
Ungeainisha hizo sababu ingekuwa safi sana
 
Mzee Mwanakijiji,

Ni uhuru wako kabisa (na kwa Mtanzania yeyote) kutoa maoni yako na fikra zako maana ni haki ya kikatiba ili mradi huivunje sheria. Nimesoma mtazamo wako juu ya wabunge wa upinzani wanaotetea kwa nguvu haki ya watanzania kupata habari ya vikao vya bunge moja kwa moja (live coverage). Nimesoma pia maoni ya wachangiaji wa post yako, na jinsi na wewe unavyochagua hoja za kujibu huku ukiacha hoja za kufikirisha bali unajibu zilizo nyepesi. Mfano mchangiaji mmoja ameuliza..... kwa kuwa kusubiri kupata habari iliyorekodiwa kunaweza kumpa fursa mhariri kuihariri kwa manufaa ya watawala (jambo linalowezekana kabisa na wewe unajua hivyo), je mtanzania atakuwa amepata haki ya kupata habari?...sijaona jibu lake. Labda hujaona post hiyo!!!!! Umenikumbusha wakati Prof Shivji anaanza kuwaeleimisha watu juu ya katiba mpya, sijui nini kilimpata maana aligeuka nyuma na mara akageuka jiwe la chumvi.
Mimi Mkristo, Yakobo 3:1 maandiko yanatuonya hivi; Ndugu zangu, wengi wenu msiwe walimu. Kama mjuavyo, sisi walimu tutapata hukumu kubwa zaidi kuliko wengine. Kama wewe Mzee Mwanakijiji ni Mkristo, tafakari maneno hayo, kama si mkristo basi tafakari ya mstari huo ni kuwa, ukipotosha watu kwa makusudi,utahukumiwa pakubwa.

Nakutakia tafakari njema.
 
Muwe mna jibu hoja za MM sio munapayuka tu, kama kuna mtu angeweza kujibu hoja hii tu angalau angekuwa amesaidia jamii yetu hii mfu itoke huko gizani ilipokuwa,kama alivo uliza MM kuna kifungu gani kwenye katiba kinasema ni lazima mwanachi apate habari live? aje na iko kifungu sio ndombolo. MM simple wewe ni wakutolewa mfano big up.
 
Mzee MM ungekuwa unajiheshimu ungekuwa umeacha kuanzisha mada hapa Jf. Kusema kweli nilikuheshimu sana, lakini leo huna tofauti na Lizaboni, Ritz, Hamy-D na Laki si pesa wa wakati ule. Nisamehe sana mzee wangu tangu umekuwa kama ulivyo sikuwahi kukujibu, lakini nahofu wewe Dr Mihogo ktk fake ID
Ukawa hampendi kusikia habari hasi dhidi,hata usipomuheshimu wewe ataheshimiwa na watoto wake na mkewe inatosha kabisa
 
House of Commons la Uingereza linaonyeshwa Live masaa yote. Wana Tv yao ya Bunge inaitwa(BBC Parliament TV) Vikao vyote vya Bunge vinaonyeshwa Live muda wote. Hiyo Stesheni ni Bunge tu 24/7.

Acha kudanganya Watu.

Usikurupuke tu kuandika nimeelezea kuhusu hio hapo juu soma.

Hio BBC Parliament ni sister channels na zingine BBC1,2,3 na 4 na zote zipo chini ya mwanvuli wa BBC.

Na nimesema hata hivyo BBC ilinunua channel hiyo ilokuwa ni private mwaka 1998.

Hivyo TBC haiwezi kwa sasa kujigawa na kuwa na channels kama vie TBC Parliament na zimgine mambo hayo yanahitaji watu wenye ubunifu na dira, kwa sasa haina uwezo huo kifedha na kiubunifu.

Halafu isitoshe, wazungu hawashindi kutwa wanaangalia hio BBC Parliament bali wapo kazini wanachapa kazi na ndio wamefikia hapo walipo.

Isipokuwa Channel hio inatumiwa sana na waandishi wa habari,watafiti na wadau wa masuala ya kisiasa na bunge kupata habari na kuziandika kutokana na uchambuzi wao.
 
Tukisoma bandiko la MM kuna mahali amelaumu wapinzani kuondoka bungeni na kushauri iwepo sheria ya kukatwa mishahara ikitokea hivyo. Anaaminisha wanaondoka tu bila sababu za msingi, fair enough!

MM anasema wabunge wakiondoka bungeni ni kwa njia gani wanawakilisha wananchi wao?

Kuondoka kwa wabunge kuna ashiria mambo mengi.
Kwamba, hawaridhiki na yanayotokea, hawasikilizwi, wanaburuzwa au kuna ukiukaji wa taratibu na sheria n.k

Juzi walipoomba mwongozo, kiti kilikataa na hata yale waliyosema hayakujibiwa.

Kiti kilisisitiza shughuli za bunge ziendelee bila kuingiliwa na miongozo.

Kwa maneno mengine hoja za wapinzani 'zilikuwa upuuzi' na kupoteza muda tu.

Hoja hii ndiyo iliyomsukuma MM kuandika kuhusu ''utovu wa nidhamu'' wa wabunge wa upinzani

Masaa 24 baadaye, wapinzani wakaomba mwongozo kuhusu uwasilishwaji wa mpango wa maendeleo wa serikali. Kama kawaida ya wakapuuzwa na kiti na kwa mtazamo wa MM, ilikuwa sahihi kutowasikiliza ili shughuli za bunge ziendeleee

Wabunge wa upinzani hawakutoka pengine wakizingatia hoja ya MM.

Walichokifanya ni kukataa waziri wao kivuli kuwasilisha mpango wao kwasababu taratibu za bunge zilikiu kwa kwa kuwasilisha mpango wa mwaka mmoja badala ya miaka 5.

Waziri kivuli akakaa chini ili 'kuwawakilisha' wananchi kama anavyoshauri MM

Masaa machache bunge likaahirishwa, na sasa imeonekana wapinzani wana hoja za nguvu na za maana

Hapa ndipo tunapotakiwa kujifunza. Kwamba, kuna umuhimu wa kusiilizana na kuzungumza kwa kanuni, sheria na taratibu.

Huu mpango wa kukurupuka usiotakiwa kuhojiwa umedhihirika pa si na shaka kuwa ni uzembe tunaouita #Hapakazi. Ni uzembe tuanoupaka manukato kwa kusingizia wapinzani ni watovu

Swali la shari kwa MM, je bado unasimama na kauli yako kuhusu tuhuma dhidi ya wapinzani kutoka bungeni?

Kama hawasikilizwi nini unashauri wafanye?

Na je kuna mantiki kwao kususia au bado ni 'uzembe' kama ulivyoainisha hapo juu?
 
Mzee MM ungekuwa unajiheshimu ungekuwa umeacha kuanzisha mada hapa Jf. Kusema kweli nilikuheshimu sana, lakini leo huna tofauti na Lizaboni, Ritz, Hamy-D na Laki si pesa wa wakati ule. Nisamehe sana mzee wangu tangu umekuwa kama ulivyo sikuwahi kukujibu, lakini nahofu wewe Dr Mihogo ktk fake ID


Huyu mzee naona kipaji chake kinaanza kuzeeka! ni bora akastaafu ulingo kabla ya kuchezea kichapo kutoka kwa wajukuu zake!
 
NN, of course siwezi kuitetea CCM bado sijapata sababu; Napenda ukweli tu. Fikiria watu wanasema "haki ya kuona Bunge live". Na wapo watu wanaamini kweli haki kama hiyo ipo! Wanalilia "haki yetu kuona live". Ama neno "haki" lina maana au halina. Na kama lina maana hakuna mahali popote haki hiyo imewahi kutambuliwa. Tatizo utaona ni kuwa wapo watu wanafikiria wapinzani wakisemana kusimamia jambo basi jambo hilo linakuwe la kweli! Sijawahi kuwa shabiki tu wa kufuata watu wanaoshabikia ati kwa sababu nikipinga nitaonekana sijafuata ushabiki.

Unafikiri kweli hiyo haki ipo kweli hadi watu wagome na kutoka Bungeni?


"haki ya kuona Bunge live". Na wapo watu wanaamini kweli haki kama hiyo ipo! Wanalilia "haki yetu kuona live". Ama neno "haki" lina maana au halina"

MM, Neno haki ni pana sana. kuna watu wanadai haki ya kusoma bure? Wamepewa? Kulala mahali pazuri. Wanalala? Kula vizuri. Wanakula? unaweza tafsiri kwa jinsi inavyoweza kukidhi haja yako.

But haki inayodaiwa na watanzania na wapenda democrasia ni kuendelea kuona wabunge wao wakijadili hoja zao bungeni live.. nothing more.. Tumeshuhudia serikali ya JK ilivyotoa kwa asilimia kubwa uhuru huu na matokeo chanya tuliyopata.. Viongozi kuwajibika kutokana na msukumo wa bunge na wananchi kutokana na mijadala moto bungeni. Mzee Mwanakijiji uliweza kukosoa mambo mengi kutokana na haki hii na viongozi wengi wakubwa ndani ya serikali waliweza kuwajibishwa au kuwajibika kwa taifa kutokana na mijadala mikali iliyoanzia bungeni na hivyi kutoa msukumo mkubwa kwa wananchi nje bunge kushinikiza serikali au Rais kufanya maamuzi

Tukiruhusu hili, kesho watasema report za CAG zisijadiliwe bungeni, Tunataka mabadiliko ya kutupa uhuru zaidi ya kuwawajibisha viongozi wetu wasioleta tija ndan ya bunge
 

Bunge ni Muhimili mkubwa sana katika nchi na bunge sio January mpaka December laonyeshwa live kumbukeni hilo lina nyakati zake katika mwaka sasa linapo fika wananchi ndipo wanapo taka kujua fika mwenendo wa Nchi yao inaendaje je vilitekelezwa vingapi na vitatekelezwaje lini na lini na kupata mrejesho.


Tulipita na Mkapa/ JK hapakuwa na shida as we much further kumbe tunataka kurudishana nyuma pale tunapotegemea mabadiliko zaidi ya live na ya kidemocrasia wenzetu wanapanga hapana haistahili iyo khaaa jamani tunaelekea dunia ya utandawazi mnataka tuishi stone age style kweli?


Hoja hii ilipaswa kutetewa na wabunge wa upinzani kwa kueleza faida na hasara ambazo zingetokana na zuio la Serikali, siungi mkono kile ilichofanya Serikali lakini hoja inajibiwa kwa hoja ili kuweka uwanja mpana bila ushabiki kama ilivyo sasa tumekua kama Kasuku kila anachosema Mbowe kila mtu anakalili.

Hata kama Mzee wa makengeza pamoja na kamati ya uongozi ilizuia muongozo huu bado kulikua na njia mbadala ya kufikisha ujumbe wakati wa kuchangia hotuba ya Rais kwa sababu huchaguliwi jambo la kuongea, tumemuona mchungaji msigwa akiwapiga vijembe wabunge wa CCM kwamba wanajikomba yeye Jimboni kwake ana maji 90% na barabara kibao za lami kwa nini isitumike njia hii badala ya kukimbia huu ni UJINGA WA HALI YA JUU.
 

Asilimia ngapi ya wapigara kura TanZania wanaweza kuangalia Bunge live kupitia TV ? Kumbuka hapa ni Bongo na siyo Marekani ambapo kila mtu ana TV, hapa TZ watu wenye TV hawafiki hata asilimia 10 (10%) ya Watz wote, sasa hiyo haki yao ya kuangalia TV live inatokea wapi?
Kwanza bora hata ingekuwa mnapigania redio hapo kidogo ingekuwa labda sawa kwa maana Watz wenye uwezo wa kusikilitza redio ni wengi lkn siyo TV!

Kwa hiyo kwasababu watanzania wengi hawana uwezo wa tv, ndio basi iwe sababu ya kuwanyima fursa hata wale wachache wanaoweza kuangalia? dont be so shallow...
 
Tukisoma bandiko la MM kuna mahali amelaumu wapinzani kuondoka bungeni na kushauri iwepo sheria ya kukatwa mishahara ikitokea hivyo. Anaaminisha wanaondoka tu bila sababu za msingi, fair enough!

Nguruvi, ndugu yangu maswali yako ni mazuri sana lakini nitajibu kama ifuatavyo.

Leo wingi wa CCM Bungeni haujatokea kwa bahati mbaya; umetokea kwa sababu kuna watu ambao walikuwa na miaka mitano wakijipanga kuing'oa CCM madarakani wakafika dakika za mwisho wakajivuruga. Leo hii CCM imepata wingi ambao haikupaswa kuwa nao. Binafsi, hili sionei huruma, wakitaka kucontrol kinachotokea Bungeni ni lazima wapunguze wabunge wa CCM, na ili wapunguze wabunge wa CCM ni lazima wao wenyewe wajipange. Hadi hivi sasa sidhani kuna mtu yeyote CHadema anayetafakari kwanini CCM ilipata wabunge wengi; of course, tafakari yoyote inayofanywa inafanywa kwa kubebesha lawama zote CCM kana kwamba wao CHADEMA hawakuvuruga au kufanya mambo fulani yaliyochangia hili.

SUala la hoja kuna njia nyingi; kutaka mwongoza ni jambo moja tu. Lakini zipo njia nyingine rasmi za kushughulikia jambo Bungeni na tumeshaona wakizitumia huko nyuma kwa mujibu wa Sheria na taratibu za Bunge. Wabunge wana haki sawa Bungeni. Mbunge anaweza kuleta hoja rasmi, hoja ya dharura au hata kutaka kanuni fulani itenguliwe. Lakini pia wana utaratibu wa kuletwa miswada binafsi ambayo inajadiliwa na inaweza kabisa kupitishwa na kuwa sheria.

Linalotokea ni kuwa njia hizi hazina drama sana na hazioneshi ubabe na kukamiana. Suala hili la kurushwa live linaweza hata sasa kushughulikiwa vizuri na kwa njia za kidemokrasia. Mwenyekiti anaweza kuzuia mwongozo lakini hawezi kuzuia ujio wa hoja mahsusi, hoja ya dharura au hata mswada wa sheria (ukiwa umefuata taratibu zake). Kwanini njia hizi hazitumiki kueffect mambo Bungeni?

Of course jibu mojawapo ni kuwa "CCM wako wengi" na ukishatoa hili jibu nitarudisha hiyo point yangu ya kwanza hapo juu. Na hili la wingi wa CCm nilishawahi kulizungumzia. Ukishakubali kanuni za mchezo na ukaingia ukazidiwa basi inabidi ukubali. Demokrasia yetu tumejariu kuijenga hivyo. SAsa siku hizi kinachotokea ni kuwa wapinzani hawataki kuulizwa, hawataki kupingwa, hawataki kukataliwa. Ukipinga, ukiuliza au ukikataa basi unaonekana tayari umeshakuwa CCM! WAnataka kila wanachosema kikubaliwe kwa sababu tu kuwa kimesemwa na wapinzani! Hapo hatujengi wala hatujitendei haki sisi wenyewe.

Tunataka tuaminishwe kuwa wapinzani ndio pekee wanaojua kilicho sahihi na pekee ndio wanasimamia maslahi; ukweli ni kuwa Watanzania walienda kupiga kura na hawakuwaamini kuwapa wapinzani Bunge. Sasa, hili ni baya lakini ndio ukweli. Na wengi - CCM wanatumia - wingi wao kwa haki hata kama tunaweza kuona ni kwa namna gani si kwa maslahi ya taifa. Watanzania hawa hawa wataendelea kuona na watataka kushawishi watu waone ubovu wa CCM na watapiga kuwakataa wabunge wake. Lakini kama tulishindwa kuwashawishi 2015 kuikataa CCM kwa kujivuruga sisi wenyewe tutaweza vipi sasa. Fikiria mfano mbaya tu, kuna watu wameshtuka sana ati Chenge mwenyekiti wa Bunge; wanashangaa mtu huyo aliyetajwa kwa kashfa mbalimbali kuchaguliwa; hao hao hawatashangaa ilikuwaje wao wampendekeze Lowassa kuwa Rais.. watasema "kwani ameshtakiwa na mahakama yoyote" na watasema "aliseham hausiki". Hoja hiyo hiyo ikitumiwa kwa Chenge utaona wanaruka! Kumbe ni kweli kwa Lowassa lakini si kweli kwa Chenge!

Halafu binafsi bado sijaona msingi wa kutaka "kuona wabunge wakifanya kazi"; hivi mbona hatuoni watu wanagombania kuona Ikulu au Rais anavyofanya kazi na kufanya majadiliano mbalimbali ili tujue kweli anafanya kazi? Si ingekuwa faida kweli kuona jinsi gani Rais anafanya kazi na Watanzania wakamsikia? Mbona hatutaki kuona mahakama zinavyofanya kazi "live" ili tujue kinachofanyika ni cha maslahi ya Watanzania? Hoja ya "live" siyo hoja kwa kweli.
 
Usikurupuke tu kuandika nimeelezea kuhusu hio hapo juu soma.

Hio BBC Parliament ni sister channels na zingine BBC1,2,3 na 4 na zote zipo chini ya mwanvuli wa BBC.

Na nimesema hata hivyo BBC ilinunua channel hiyo ilokuwa ni private mwaka 1998.

Hivyo TBC haiwezi kwa sasa kujigawa na kuwa na channels kama vie TBC Parliament na zimgine mambo hayo yanahitaji watu wenye ubunifu na dira, kwa sasa haina uwezo huo kifedha na kiubunifu.

Halafu isitoshe, wazungu hawashindi kutwa wanaangalia hio BBC Parliament bali wapo kazini wanachapa kazi na ndio wamefikia hapo walipo.

Isipokuwa Channel hio inatumiwa sana na waandishi wa habari,watafiti na wadau wa masuala ya kisiasa na bunge kupata habari na kuziandika kutokana na uchambuzi wao.

SAsa kuna ubaya gani kutunga sheria Bungeni ya kuunda channel maalum ya mambo ya Bunge na wao wabunge waitengee fedha (ama chini ya wizara ya habari au chini ya Bunge)? si wao ndio wanaotunga sheria na kutenga fedha?
 
Back
Top Bottom