Yah:dhana ya ushirika kuleta mageuzi ya kilimo kwa walio wengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yah:dhana ya ushirika kuleta mageuzi ya kilimo kwa walio wengi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kupelwa, Jun 23, 2012.

 1. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  nathubutu kuthibitisha kuwa, ushirika ni dhana muhimu na mwafaka kujenga uchumi wa kilimo , kwa wakulima wadogowadogo na wakubwa, ili kuongeza uzalishaji, kupata masoko , na kuongeza thamani ya mazao kama pamba, korosho nk.Nachela kuthibitisha kuwa miak ya nyuma ushirika ndo kilikuwa chombo na kimbilo la wanyonge na vilikuwa vina nguvu mpka kuwa vyombo vya kuleta mageusi ya kilimo na kupigania uhuru.
  Kwa sasa dhana ya ushirika ni mfu kwa mapungufu mengi sana kama kukosa ufahamu kwa wananchama, wizi, ubadhirifu kwa watendaji, sera na sheria zinazokizana na kutoa mwanya wa utendaji mbovu, chama cha ccm kuwa msemaji wa wanachama wa ushirika .
  Bado dhana ya ushirika ili kuleta mageuzi ya kilimo kwa walio wengi ina nguvu ,ila serikali inatakiwa kuonyesha dhamira ya kweli kuujenga aina ya ushirika wa kweli kwa (capacity building).Pia dhamira hiyo ni lazima iende kwa kutunga sera nzuri ya kujenga ushirka wa kweli, sheria sitahiki inayokubalika kuliko bora liende.
  Ninao ushahidi kuwa, utafiti mkubwa ulikuwa woga wa CCM kuruhusu ushirka uwe na nguvu , sababu wanachama wake wangekuwa na maisha bora na kukipa kisogo chama.Kumekuwa na viongozi na watendaji wabovu wanatetewa au kukingiwa kifua na ccm huku wakiwa wamehujumu ushirika kwa kiasi kikubwa.
  nasihi ,serikali fedha zilizotengwa kwenye bajeti ya maendeleo ya kilimo ambazo zapata shs 192.2 zijenge ushirika ili walio wengi wapate chombo cha kuwatetea na kuendeleza mageuzi ya kilimo kwa kuanzisha mashamba makubwa, kuendeleza wakulima wadogowadogo na hivyo kupunguza nakisi ya chakula ambayo inajitokeza na kusababisha mfumko mkubwa wa bei.
   
Loading...