Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Kila nikifanya tafakuri sipati jibu. Tangu jana nimejitahidi kufikiri na kufikiria bila ya kupata nini hasa kilisababisha. Kitendo cha Waziri wa Uchukuzi, Dr.Harrison Mwakyembe kuikana UDA kuwa haiko Wizarani mwake bado sikielewi. Ni usahaulifu au alilenga jambo fulani?
Dr.Mwakyembe ni kati ya Mawaziri wasomi wabobezi ambao Serikali ya Rais Kikwete inao. Ni Msomi wa Sheria ambaye anaaminiwa na kutarajiwa kujua madaraka yake;mipaka ya madaraka yake;walio chini yake na walio nje ya uwanja wake wa kujidai wa Wizara ya Uchukuzi. Uchukuzi ni usafirishaji.Sasa iweje Shirika la Usafirishaji la Mkoa wa Dar es Salaam lisiwe chini ya Wizara ya Uchukuzi?
Nasema tena kuwa hadi leo bado siamini maneno ya Dr.Mwakyembe. Siyaamini kwakuwa yanatisha sana. Inawezekana wapo Mawaziri ambao hawajui wanaowaongoza. Sasa wanaongozaje? Sakata la UDA 'lilishazimwa' kimahakama.Hakukuwa na sababu za kukana haraka vile. Nitoe wito kwa viongozi wetu-wa ngazi zote kutambua wanaowaongoza/wanavyoviongoza ili uongozi wao uwe na maana,tija na faida.
Ndugu zangu siyo kweli mnachoamini hapo. Dkt. Mwakwembe anamaanisha hivyo anavyomaanisha. Kama amekataa kuhusu UDA, yawezekana siyo chombo ambacho kimo ndani ya wizara yake. Mbona Vyombo vingine vimeainishwa katika taarifa na bajeti ya wizara yake na kwa nini isiwe hiyo. Unajua watu tusichanganye mambo, fuatilieni kwanza kabla ya kumshangaa mtu. Wizara ina watendaji wengi wakiwemo wakurugenzi wa idara na wataalamu, je sasa iweje wote wakatae
Kila nikifanya tafakuri sipati jibu. Tangu jana nimejitahidi kufikiri na kufikiria bila ya kupata nini hasa kilisababisha. Kitendo cha Waziri wa Uchukuzi, Dr.Harrison Mwakyembe kuikana UDA kuwa haiko Wizarani mwake bado sikielewi. Ni usahaulifu au alilenga jambo fulani?
Dr.Mwakyembe ni kati ya Mawaziri wasomi wabobezi ambao Serikali ya Rais Kikwete inao. Ni Msomi wa Sheria ambaye anaaminiwa na kutarajiwa kujua madaraka yake;mipaka ya madaraka yake;walio chini yake na walio nje ya uwanja wake wa kujidai wa Wizara ya Uchukuzi. Uchukuzi ni usafirishaji.Sasa iweje Shirika la Usafirishaji la Mkoa wa Dar es Salaam lisiwe chini ya Wizara ya Uchukuzi?
Nasema tena kuwa hadi leo bado siamini maneno ya Dr.Mwakyembe. Siyaamini kwakuwa yanatisha sana. Inawezekana wapo Mawaziri ambao hawajui wanaowaongoza. Sasa wanaongozaje? Sakata la UDA 'lilishazimwa' kimahakama.Hakukuwa na sababu za kukana haraka vile. Nitoe wito kwa viongozi wetu-wa ngazi zote kutambua wanaowaongoza/wanavyoviongoza ili uongozi wao uwe na maana,tija na faida.
Kwa wanazuoni, kama mtu akikana andiko lake la PhD taratibu zikoje ili mtu huyo aweze kuendelea kutambilikana miongoni mwenu. Je ni kweli kuwa mtu huyo itambidi aandae andiko lingine ili atunukiwe PhD halali?mwakyembe ile sumu aliyowekewa naona inamchanganya mpaka anakuwa msahaulifu sikuizi,ukijumuisha na kuikana dessertation yake iliyompa phD kwenye bunge la katiba.inanitia mashaka uwezo wake wa maamuzi na utambuzi wa daktari huyu nguli wa sheria.
Kwa wanazuoni, kama mtu akikana andiko lake la PhD taratibu zikoje ili mtu huyo aweze kuendelea kutambilikana miongoni mwenu. Je ni kweli kuwa mtu huyo itambidi aandae andiko lingine ili atunukiwe PhD halali?
Nafikiri chuo alichosoma ndo wanajukumu la kumvua hiyo degree waliyomtunuku, Ref: Mgabe vs Vyuo vya uingereza. Kwa hiyo nategemea UDSM imvue huo udaktari na kumwamru aandike thesis nyingine kama atahitaji kuwa daktari tena.kabla ya kuandika jipya anajivua kwanza UDAKTARI wake , amekwishafanya hivyo ?
Unataka kusema jamaa kwa sasa hana sound mind?polonium sio dozi ya kitoto, lazima ubongo upoteze maana.
tamisemikwahiyo uda iko wizara gani?
Nafikiri chuo alichosoma ndo wanajukumu la kumvua hiyo degree waliyomtunuku, Ref: Mgabe vs Vyuo vya uingereza. Kwa hiyo nategemea UDSM imvue huo udaktari na kumwamru aandike thesis nyingine kama atahitaji kuwa daktari tena.