kamanda Hannibal
Member
- Jan 24, 2018
- 15
- 12
Jana Mkuu ameshangazw na kitendo cha baadhi ya majaji kwenda likizo katika nchi za kifahari kupumzisha akili. Si hilo tu, bali kilichomshangaza ni kutumia gharama zao. Siamini kama Mopao hajui kuwa majaji wana maslahi manono sana.
Sheria ya Malipo na Stahiki za Majaji imewfanya wawe mithili ya wafalme. Jaji anapewa nyumba yenye hadhi ya daraja la kwanza, analipiwa housemaid, vyombo vya ndani anapewa, posho mbalimbali, akisafiri iwe kwa basi, meli, treni au ndege kwenda popote analipiwa yeye na mkewe ticket yenye darja la hadhi ya juu kabisa, anapewa gari binafsi na dereva pamoja na mafuta lita 70 kila wiki(maana yake ni sawa na lita 10 kwa siku sawa na km 80 kwa siku-mizunguko ya mjini tu unazimaliza vipi), matibabu yake mkewe na watoto wake analipiw na serikali, bills za maji, umeme seeikali inamlipia, airtime serikali inamlipia, housekeeping serikli inagharmia, akiwa likizo still mshahara analipwa ongeza na posho ya likizo.
Kwa mazingira haya kwanini mtu ashindwe kutunza viji Mil 10 akavitumia kwa likizo yake dubai au bondeni. Hakuna kosa kufanya vacation nchi yoyote.
Labda ipo hofu kuwa wakiwa huko wanahongwa au wanapata fadhila kwa kesi za nyuma walizoziamua. Ni jukumu la serikali kuchunguza kama kukaa kwao huko au pesa wanazotumia zinalipiwa na watu ambao kw namna moja au nyingine zinakiuka miiko ya ujaji.
Binafsi nilipata shaka kuwa yale ya wakuu wa mashirika kulipwa pesa nyingi yanaanza kutazamwa pia katika mahakama. Kama hivyo ndivyo basi azipungunze sababu sheria inampa mamlaka hayo. Lakini akumbuke kwanini sheria zinawataka majaji kulipwa vizuri; KUWAONDOLEA VISHAWISHI VYOVYOTE ILI WASIMAMIE HAKI BILA SHURTI YOYOTE.