Ya Mungu na ya kaisari - wapi na wapi ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Mungu na ya kaisari - wapi na wapi ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mag3, Oct 20, 2008.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mwinjilisti: Mbeya kulaaniwa na Mungu

  Na Charles Mwakipesile Mbeya

  MRATIBU wa Maombi wa huduma ya Tanzania Itubu Taifa, Mwinjilisti Ambokile Mwasomola, amesema kitendo cha wananchi wa Kijiji cha Kanga Chunya, kupiga mawe magari yaliyokuwa kwenye msafara wa Rais Jakaya Kikwete, ni laana mbele ya Mungu kutokana na ukweli kuwa kiongozi huyo kuwekwa madarakani na Mungu.

  Akizungumza juzi na mwandishi wa habari hii kuhusu sakata hilo, alisema wananchi hao wameonesha tabia ya ajabu ambayo kama Watanzania hususani wa Mkoa wa Mbeya hawatafanya maombi makubwa kwa ajili ya toba mbele za Mungu, ni wazi kuwa laana kubwa itashuka.

  Alisema Biblia inasema mamlaka zote zinazotawala zimewekwa madarakani na Mungu na hivyo ngazi ya Rais haitakiwi kufanyiwa mchezo wa aina yeyote.

  Mratibu huyo wa maombi alisema sababu kuwa walitaka kumuona Rais kamwe haitoshi kufanya fujo hizo na hivyo kinachotakiwa ni wahusika na waombaji wa Mkoa wa Mbeya, kufanya maombi maalumu kama njia ya kutubu.

  Mmmm!!! Naambiwa Mungu wa kweli anachukia uwongo, wizi, uzinifu, uonevu n.k. - na vyote amevibatiza jina moja DHAMBI. Viongozi kwa upande mwingine huingia madarakani kwa njia tofauti kama ulaghai, rushwa, mapinduzi n.k - je ni kweli wamepata baraka za Mungu. Mbona Tanzania tuko tayari kutumia jina la Mungu kuhalalisha matendo maovu ama mungu wetu ni wa kwetu peke yetu. Vitendo vinavyofanywa na viongozi wetu wa dini kwa kuhusisha jina la Mungu vinaashiria tulivyotumbukia kwenye tope la uovu.

  Mwinjilisti Ambokile Mwasomola aombe radhi watu wa Mbeya na watanzania kwa jumla atubu mbele ya Mungu kwa kuingia kwenye kundi la wanaotumiwa na shetani. Matamshi yake yalaaniwe kwa nguvu inayostahili ili iwe fundisho kwake yeye binafsi na wengine kama yeye wanaotumia jina la Mungu kujinufaisha na kujitafutia umaarufu wa bure.
   
 2. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Naona ni ule mzimu wa Mwankupili unaendeleza fujo zake. Kwa hiyo Bwana Ambokile unatuambiaje kuhusu Pol Pot, Iddi Amin, Adolf Hitler, Emperor Bokassa, Verwoerd, na wengine wa jinsi hiyo, hawa nao waliwekwa na Mungu? Ni mungu yupi huyo anayetajwa na "mwinjilisti" Ambokile?
   
Loading...