Habari zenu mashibiki wote wa Man U na wadau wote wa soccer,
Awali ya yote naomba ni declare interest, mi ni die hard Man U fan, nina zaidi ya mapenzi na timu hii mi nina mahaba na timu hii. na nasukumwa na mahaba hayo kuongea haya
Hadi hapo, nimeshakuona wewe siyo shabiki wa kweli wa United.....kwani mshabiki wa kweli na anayeifahamu United, hawezi kuiita Manchester United Man U....
Ni wazi kwamba wengi wa mashabiki wa timu hii tumeipenda timu hii sio tu kwa sababu ilikua inafundishwa na SAF bali ni kwa sababu ilikua ni timu ya washindi, timu yenekuleta ushindani mpaka dakika ya mwisho, how many times tumechomoa magoli dk za 90,94 au 96 wakati wapinzania washaamini ushindi upo kwao it was in our DNA, that is Manchester I used to know, je Man U hiyo imeenda wapi…?
Ni kweli unachokisema. Lakini, si sahihi kufikiri timu itakuwa ikichomoa magoli dakika hizo za majeruhi kwa kila mechi...kama ndivyo basi timu ingekuwa bingwa kila mwaka.....hapo huitaji kuwa na akili nyingi, zaidi ya kutumia common sense....
Naelewa na kuamini msemo usemao mvumilivu ula mbivu lakini vilevile dalili ya mvua ni mawingu na chelewa chelewa utakuta mwana sio wako.
Wapo wadu wanajaribu kusema hii hali ya timu yetu sa hivi ni kawaida tu hata SAF aliipitia, katika swala la kuipitia sina ubishi nalo ila kusema ni kawaida hapo ndio tunatofautiana, Hivi expectation za Man u wakati Fergie anakabidhiwa timu zilikua sawa na za Man U ya sasa…? Aliikuta timu hipo katika level gani katika timu za Uingereza…? Hivi expectations walizonazo washabiki wa Swansea kwa kocha wao mpya ni sawa na za mashabiki wa Man U…? je mnataka kusema lengo la kuleta kocha mpya ilikua ni kutoka level zetu za big 4 kwenda kuwa wafalme wa big 7…?
Tuliza boli arifu....ligi bado haijaisha...lakini kumbuka ukiwa mshabiki wa kweli, jiweke tayari kwa matokeo yoyote ya timu yako....iwe kushinda, kufungwa ama kudroo....hata kama kushuka daraja....
Mpaka hapo nimeshaonesha mlengo wangu ni hupi, YES simkubali Moyes na I put all blames on him kwa kiwango kibaya cha timu yetu cha kihistoria, wanao msupport Daudi wamekua wakisema tumpe muda anajenga timu, nafikiri wangesema tumpe muda maana anabomoa iliyokuwepo kwanza ndio baadae aje kujenge timu mpya….
Hicho ndicho alichoambiwa DM...mwaka huu aangalie ni wapi pana udhaifu katika timu na klabu kwa ujumla (yeye kama meneja)...kisha aanze kujenga timu....kujenga timu ilikuwa ni lazima kutokana na wachezaji wengi kuzeeka na kufikia ukingoni mwa uchezaji wao...pia nimekuwa nikisema kwamba, DM siyo SAF, SAF aliweza kumfanya Smalling acheze kama Franco Baresi, ama Tom acheze kama Xavi n.k. Sasaa DM anapaswa kuwa na breed yake ya wachezaji (keshaanza na Fellaini na Mata - amini nakwambia Fellaini atakuwa mzuri United) ili sasa hapo ndipo tuanze kumkaanga....angalia Maureen alivyofanya Chelskis na Mancini alivyofanya Shitty...walifanya complete overhaul na kuleta wachezaji wanaowataka ndipo wakafanikiwa...sasa DM hawezi kufanikiwa kwa kuendelea kuwa na wachezaji wa SAF....kwa mpira wa sasa (mpira pesa), United inahitaji top class players kama wanne ama watano..na hilo DM alisema toka awali...tusubiri next transfer window kwa kusema zaidi....
Timu hii iliyoonekana mbovu leo hii ndio timu hiyo hiyo iliyochokua vikombe msimu uliopita under SAF na benchi lake la ufundi, cha kustaajabisha daudi alipokuja akataka kuonesha ulimwengu ye ni mjuzi wa mambo akafukuza bench lote la ufundi nakuleta lake amabao limeprove failure,
SAF na DM ni aina ya makocha tofauti sana....SAF ni mchawi na jiniasi katika ukocha....nimeshasema hapo juu....hilo la kusema DM alifukuza benchi la ufundi, ni ishara nyingine kuwa huifahamu United vizuri....Rene na hata Phelan waliombwa kubaki, lakini wenyewe wakasema wanapenda kuondoka....sasa hapo unamlaumu vipi DM? Ulitaka awalazimishe? Benchi la ufundi limeprove failure kwa lipi wakati msimu bado haujaisha? Kwani unataka kusema hakuna msimu ambao SAF na benchi lake la ufundi waliondoka kapa? (kama kushindwa kuchukua kikombe ndio ishara ya failure)
Na ikumbukwe Moyes ni Manager na sio coacher/mkufunzi na kazi ya manager sio kumfundisha RVP kufunga au Vidic kukaba bali ni kuleta game plan afu wachezaji wanaifollow hiyo game plan, na ili kuwafanya wachezaji wamaiweze game plan yako kwanza ni mpka wae na imani na wewe, pili hiyo game plan yako hiwe workable na mwisho kabisa laziama uwe the good MOTIVATOR, na manager mazuri dunianiani ni good motivator hata kama timu inamapungufu as long as kocha wao yupo wataperform tu kwa kiwango sawa na timu zilizo bora, Moyes kashindwa kabisa hii….
Naona umemfahamu DM baada ya kuja United...eti siyo good motivator!! Unaweza ukamotivate wachezaji, lakini wasiporespond kwa hiyo motivation utafanyaje? Mfano ni game ya jana, dakika za mwisho, DM alikuwa anawapigia kelele wachezaji waende mbele kumalizia kwa mashambulizi, lakini wachezaji walikuwa wakirudisha pasi nyuma...sasa unataka aanze kuwapiga makonzi sio? Subiri apate wachezaji anaowataka, kisha uanze kumkaanga vizuri....
Mbinu za man U siku hizi the are very obvious and predectable mpaka timu zinazaotaka shuka daraja can crack our plans easily and use them against us, mfano game ya juzi na Fulham, mbinu za moyes zilikua old school kabisa, tanua uwanja then piga long crosses, by the way tulipiga cross zaidi ya 80 and then what…!! I wonder mata alinunuliwa kwa ajili gani kama hii ndio game plan ya Moyes
Kunaweza kuwa na ukweli kidogo...lakini husijaribu kujitoa ufahamu...kwani hata chini ya SAF, United ilishafungwa sana na vijitimu vidogo vilivyokuwa katika relegation battle, tena hata pale OT....katika game dhidi ya Fulham, ilikuwa ni vigumu mno kwa timu (hata ingekuwa Shitty ama Chelskis - uliona jinsi Chelsksis walivyoshindwa kuwafunga West Ham pale darajani?) kushinda kwa mfumo ule wa uchezaji...kama uliangalia gemu vizuri utanielewa...Fulhamu iliweka wachezaji 6 pale katikati...hawa sita walikuwa wakiungana na mabeki 4 katika kukaba, hivyo kupelekea wachezaji 10 wa Fulham kuwa wanakaba muda wote....hivyo kwenda mbele kwa kupitia katikati ilikuwa ni almost impossible....krosi zilikuwa ndio tactic nzuri, sema pengine walichokosea wachezaji ni kutopiga low crosses...high crosses kwa mabeki wenye futi 6+ dhidi ya washambuliaji wenye futi 5+ ni kazi bure...hivyo krosi za chinichini ndizo zingefanya kazi...si uliona goli la RvP, pale Mata alipopiga 'krosi' ya chini?
Nakushangaa kwa kushangaa kununuliwa kwa Mata!! Katika games zake 3 za kwanza, katoa pasi 3 za magoli! Na katengeneza nafasi nyingi za magoli kuliko alivyokuwa Chelsea kwa msimu huu...Mata ni perfect player katika kuanza kuijenga United mpya...heko kwa Ed Woodward kwa kucheza pele katika hilo....
"Moyes the chosen one" hii kauli ndio inatuua sasa man u, sijui ni nini SAF alikiona kwa Moyes mpaka akaamini is the right guy for the Job, na sijui alishindanishwa na nani na kuibuka kinara au kipi exactly walikiona kwa Moyes, binafsi nilipoona The Boss kampendekeza sikua na shaka kabisa ni kiaamini thr Boss siku zote huwa yuko sawa kwenye maaamuzi yake, ila sas nahisi na naaamini on this he gotta it all wrong,
Sawa kama wewe una akili za mpira kuliko SAF....basi nenda kapendekeze kocha mwingine kwenye bodi.....unam-judge kocha kwa miezi 6? Na utasemaje kwa Arsene Chenga aliyekaa miaka 9 sasa bila kikombe?
ikumbukwe huyo Fergie before coming to Man he was already the winner, he had already won the Scottish League with Aberdeen and he kills the domination of Rangers and Celtics akaja England akaikuta man U hiko dhoofu bin hali, lakini akawatoa waflme Liverpool kileleni, Moyes c.v yake inaonesha alishawai kushinda nini au nini kilichomfanya apewe timu kubwa kiasi hiki…?
Na SAF kabla ya Aberdeen alikuwa winner? Maureen kabla ya Porto alikuwa winner? Pellegrini kaenda Shitty alikuwa winner? Wenger alivyoenda goons kutokea Japan (nchi iliyokuwa haitambuliki kisoka) alikuwa winner? Brendan Rogers ashawahi kushinda chochote? Ukijibu hayo ndiyo utafahamu kuwa DM kaja United ili kuwa winner..inaweza isiwe mwaka huu na hata mwakani, lakini naye atakuwa winner akiwa United.
MWISHO; nothing personal, ila Moyes kaishaprove he gotta nothing to offer for Man U tukubali tu tulibugi hapo, na ka nakosa Moyes prove me wrong leta ushindi nyumbani, ntakuja hapa na kusema YES you are the right person for our team after all hakuna shabiki anafurahia kushindwa wala hakuna shabiki anajinyonga au kumchoma mtu kisu timu yake inaposhinda kwa kuwa hatupati ushindi as we used to get basi something is wrong somewhere, and it is my duty as a fan to shout about it
Huyo shabiki atakuwa hafahamu matokeo katika soka...kushinda, kushindwa ama kudroo. Sasa kama ukifahamu soka lina matokeo matatu, na wewe ukaamua kushabikia timu fulani, basi uwe tayari kwa tokeo lolote kati ya hayo matatu.
Naona mwishowe utapata presha ama kujitia kitanzi bure...kwani DM ndiyo ameshafika hapo United...angalia chifu usije ukututoka kabla ya siku zako....