Jana jioni (kwenye saa 11 hivi) nilikuwa nikisikiliza Radio One. Nilimsikia Mh. Jery Slaa akipinga kwa nguvu zote amri ya Dr. Magufuli ya kuondoa mabango kwenye hifadhi za bara bara. Sababu kuu aliyokuwa akito ni kuwa eti, utekelezaji wa amri hiyo utashusha kwa kiasi kikubwa sana mapato ya Manispaa hivyo huduma kwa wananchi zitateteleka. Pamoja na mambo mengine, matamshi yake yalionesha kuwa Mh. Magufuli atumii busara katika maamuzi yake, anatumia madaraka vibaya na hawajali wapiga kula wake.
Baada ya kusilikiza mjadala ule nilijipa muda wa kutafakali na nimeona kuwa hizi kelele wanazopiga waheshimiwa madiwani sio bure kuna faida wanayoipata kutokana na mradi huu wa mabango. Sababu za kusema hivyo ni hizi:-
1. Kama kweli waheshimiwa hawa wanaona mabango yakiondolewa wananchi wataumia sana mbona hatujaona wakitoa hata neno moja wakati nyuma za wananchi hao zikibomolewa tena bila fidia.
2. Kama Sheria ipo na Mh. Magufuli anaitekeleza hapa Mh. Pombe hana kosa labda Mheshimiwa Slaa awashauri wabunge walio katika jimbo lake (ambao tena ni wajumbe wa baraza la madiwani) wakaichakachue bungeni kama ile ya Chama kikuu cha upinzani bungeni. Vinginevyo Magufuli songa mbele.
3. Eti mabango yakiondolewa mapato yatashuka! Duh! Hapa ndio nilichoka kabisa. Sasa kama mapato yenyewe yanapatika kwa biashara haramu anataka Mh. Magufuli afumbe macho tu eti kwa kuwa manispaa inameki! Kama ni hivyo basi mie namshauri Mh. Slaa aishauri manispaa ya Ilala ianze biashara ya Madawa ya kulevya au Walime mashamba ya Bangi kule chanika manake biashara hii inalipa sana. Alafu tutaona kama kamanda Kova akifanya vitu vyake atamwambia unajua tunalima bangi ili tujenge bara bara na hospitali kila kata.
Mie namshauri Mh. Jery Slaa aache kuleta ubishi ambao hauna maana na ajaribu kutafuta vyanzo halali vya mapato.
Big up Mh. Dr. JP Magufuli!