Ni vijana wanaopatikana wakati wowote na mahali popote. Hata jambo likianza saa tatu asubuhi wao wapo. Hawana ofisi wala bosi wa kumwomba ruhusa ya kwenda kuandamana na kurusha mawe. Ndio hawa wanaonekana wamevaa ' Kata kiuno' na wengi wao hawajahi hata kuingia misikitini au makanisani.
Inakuawaje kijana wa kweli wa Kiislamu achome kanisa na kuiba kompyuta. Inakuawaje kijana na muumini wa kweli wa Kiislamu aonekane saa mchana wa jua kali akivamia baa na kukimbia na kreti za bia? Ni maswali yanayotutaka tutafakari kwa makini.
Maana, ninavyoamini mimi, uchumi na elimu duni ndio hasa vinavyochochea vurugu za kijamii, iwe za kidini au kisiasa, na hususan inapohusisha vijana. Vijana wetu hawana misingi mizuri ya elimu, na wengi hawana ajira pia.
Tuache mafundisho ya uogo hayata tusaidia, watoto wanajaribu mafundisho yetu je yapo sawa? kumbuka kila fundisho litajaribiwa na kizazi hiki hivyo tuwe makini na mafundisho yetu. je huyu mtoto mkristo aliitoa wapi qurani?
Mkuu,
Tukirudi katika kosa la huyu kijana nakubaliana na mawazo ya maggid kuwa busara itumike. Kwani sidhani makanisa au misikiti inahusika na matendo ya wanaadamu. Vile vile serikali iende mbali zaidi kushughulikia grievance za waislamu kwani yanayotokea Nigeria hayakuanza leo wala jana bali ya muda mrefu. Kinawashinda nini kuanzisha committee hiyo na ikawayasikiliza manunguniko ya waislamu na ikayasikiliza manunguniko ya wakristo then wakawaomba watanzania watoe mashauriano ili ipatikane solution kusudi tuishi kwa amani? Hivi wewe unadhani hali hii kutumia vitisho na mikwala ndio solution? Kuwakamata na kuwafunga watu ndio solution just think yourself utafahamu kuwa ninachokisema kina mantiki.
Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'
Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!
Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!
Naomba nikusahihishe,
Nimesoma kwenye gazeti moja na kwa mujibu wa watu walioko huko huyo kijana alikuwa ana miaka 14. Hata kama ana miaka 12 ni umri ambao vijana wengi wanakuwa washabaleghe na hivyo anajua fika anachokifanya.
Pili unaposema yule mtoto wa kiislamu anavyosema kuwa akiichezea Quran atageuka kuwa kichaa binafsi naona huyu nae ana kosa but haliko sawa na kukojolea Quran. Labda angelikuwa huyu kijana amekojolea biblia ningelikubaliana na wewe maana huwezi kuwa imani thabiti ya uislamu hadi uamini vitabu vyote vinne na biblia na quran ni mojawapo ya vitabu hivyo. Hivyo sikubaliani na wewe waadhibiwe sawa kwani mmoja amefanya mzaha na Quran na mwengine amekashifu Quran. Hawa wana adhabu mbili tofauti.
Kuhusu ghasia ninachokiona mie siamini hawa waislamu wanaoandamana au kufanya wengi ni waislamu bali ni wahuni na wasio na ustaarabu. Hata hivyo inawezekana baadhi yao ni waislamu na ukiangalia zaidi ni ufukara na chuki ya muda mrefu dhidi ya ndugu zetu wakristo ndio imepelekea hivi. Kwani wasichome masinagogi ya wahindi kule Temeke? Kwanini wasiharibu miti ya ibada ya wapagani bali wameenda makanisani? Haujiulizi why?
Ndugu zangu,
Moja ya hadithi za Mtume Muhammad S.A. W ni pale Mtume Muhammad alipokuwa msikitini na maswahaba wake. Mara akaingia msikitini mtu wa kabila la Mabedui na kuanza kukojoa. Maswahaba wa Mtume wakasimama kwa hamaki kutaka kumwadhibu Bedui yule.
Mtume akawasihi maswahaba wake wasifanye jambo lolote litakalomdhuru Bedui yule. Hapo ikavutwa subira. Bedui yule akakojoa na akamaliza. Mtume Muhammad alipomuhoji Bedui yule ikabainika kuwa alikuwa ni mtu wa hovyo na wala hakujua kuwa alimokuwa ni msikitini. Bedui yule akaelimishwa, akaelewa. Akarudi kwenye ustaarabu.
Ndio mkojo ule ulifutwa kwa maji na amani ikawepo. Wahenga walinena; Subira yavuta heri. Siku zote, hamaki si jambo jema. Kwa kutanguliza subira na kutumia hekima Mtume Muhammad aliivuta heri na kuepusha shari.
Maana, kama Mtume alisingewaasa maswahaba wake kuvuta subira, basi, makubwa matatu yangetokea ndani ya msikiti ule; Mosi, zingezuka vurugu na watu kuumizana na hata kutoana roho. Pili, mkojo wa Bedui yule ungesambaa msikitini kwa vile alishaanza kukojoa na isingekuwa rahisi kwake kukatisha mkojo wake. Tatu, Mkojo una madhara ya kiafya pia.
Naam, kwa mwanadamu, ni muhimu kuwa na subra na kutafakari kabla ya kufanya maamuzi. Kwa ndugu zangu Waislamu, tunaona Mtume Muhammad ameweza kuonyesha hilo. Na kwa ndugu zangu Wakristo, kuna mifano pia ya Yesu Kristo kuonyesha subra.
Ndio, Uislamu, kama ilivyo kwa Ukristo na dini nyingi za humu duniani, msingi wake ni amani na upendo. Kitendo cha mtoto yule wa Mbagala kukojolea korani kitazamwe kwa sura ya kitendo kilichofanywa na mtoto .
Na kama ilivyokuwa kwa Bedui yule, kama pale Mbagala subira na hekima vingetangulizwa, basi, yumkini tungebaini kuwa mtoto yule hakujua madhara ya kitendo chake. Naye angekanywa kama tuwakanyavyo watoto wetu. Na hata kitendo hicho kingefanywa na mtu mzima, bado tulikuwa na haja ya kutanguliza subira na hekima kumhoji aliyetenda, yaweza akawa kama Bedui yule kwenye msikiti alimosali Mtume na maswahaba wake.
Na kwa kuangalia picha zile za Mbagala naiona hatari iliyopo sasa, kuwa tuna vijana wengi wasio na kazi; Wakristo kwa Waislamu. Vijana wasio na dogo. Ni kama moto uliofifia. Akipatikana kwa kuchochea kuni wanalipuka.
Ni vijana wanaopatikana wakati wowote na mahali popote. Hata jambo likianza saa tatu asubuhi wao wapo. Hawana ofisi wala bosi wa kumwomba ruhusa ya kwenda kuandamana na kurusha mawe. Ndio hawa wanaonekana wamevaa ' Kata kiuno' na wengi wao hawajahi hata kuingia misikitini au makanisani.
Inakuawaje kijana wa kweli wa Kiislamu achome kanisa na kuiba kompyuta. Inakuawaje kijana na muumini wa kweli wa Kiislamu aonekane saa mchana wa jua kali akivamia baa na kukimbia na kreti za bia? Ni maswali yanayotutaka tutafakari kwa makini.
Maana, ninavyoamini mimi, uchumi na elimu duni ndio hasa vinavyochochea vurugu za kijamii, iwe za kidini au kisiasa, na hususan inapohusisha vijana. Vijana wetu hawana misingi mizuri ya elimu, na wengi hawana ajira pia. Haya ni sawa na makombora yasiyo na gharama kubwa kuweza kutumiwa na wanasiasa wasio waadilifu na hata viongozi wa kidini wenye mitazamo mikali. Ni makombora yaliyoanza kutulipukia. Tuliziona ishara, tukazipuuzia.
Leo Kuna vijana watakaotumiwa au kutumia fursa hiyo kutenda maovu kwa kisingizio cha dini. Ni hawa wataoshiriki kuchafua taswira za dini husika pia. Tujiadhari, kabla ya hatari kubwa inayotujia. Hatujachelewa.
Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
Nadhani Mdondoaji unapoint hapa, binafsi sipendezwi na yanayoendelea huko Dar/Tz, hata hivyo ni ukweli kwamba serikali inabidi iingilie kati. Iingilie kati kutokana na yafuatayo:-
1. Nguvu za ki-ushindani wa nyanja zote(uchumi, siasa, utamaduni, ajira nk) duniani leo hii zinasimamiwa na Elimu. Ni elimu hiyo hiyo ndiyo inayoweza kutoa ishara ya Taifa/jamii flani itakavyokuwa katika kipindi flan kijacho. Sasa, tusirejee historia, tuanze hapa tulipo; turejee katika hali halisi kwa Tanzania, tuna shule (naomba niziweke katika namna tano) ; 1. Seminari za Kikiristo, Seminari za Kiislamu, Shule za Binafsi zisizo Seminari, shule za Serikali zenye performance afadhali( Mzumbe, Ilboru, Kibaha, nk) na shule za Serikali za Kata. katika matokeo yoyote ya Sekondari(O na A level, matokeo ya jumla yanaonyesha kuwa zaidi ya asilimi 90 ya shule za seminari za kikristo zinapata matokeo ya kuendelea hatua inayofuata ya masomo ilhali asilimia zaidi ya 90 ya seminari za kiislamu wanapata matokeo ya jumla yasiyo yenye kuendelea na hatua inayofuata. Vile kutokana na "historia" watoto wengi wa jamii za kiislam wanajiunga na shule za Kata au wazazi wao ima hawana uwezo wa kuwapeleka katika shule za binafsi kutokana na ukweli kuwa idadi kubwa ya jamii ya kii-islam wana maisha yasiyowezesha kuwapeleka shule hizo,au wanahitaji government intervention ya kuwapeleka katika shule binafsi; most likely ratio ya <10:90> inaendelea. Kwa kuwa mfumo wa elimu wa sasa, ni market based system na wazi kuwa jamii moja imeshindwa kucheza na market-based system hii, kanuni za kiuchumi zinabainisha government intervention inapotokea market failure imetokea. (Naomba niseme kuwa kuna market failure katika mfumo wa elimu uliopo baina ya waislam na wakristo hivyo si suala tena la kusema 'wenyewe hawataki kusoma' bali Serikali iingilie kati kwa kukusudia kuiondoa hii 10% ya wakristo wanaobaki uraiani na kuipunguza hatimaye kuiondoa hii 90% ya waislam wanaobaki uraiani. Serikali pamoja jamii ya kikristo ifanye yafuatayo ili kusawazisha tofauti hizi.
1.Kuanzishwe "Islamic Society enhancement programme" inayolenga kuongeza idadi ya watoto wa jamii ya kiislam kupata elimu kwa kuimarisha uwezo wa Shule zao, maabara, na waalimu hata ikibidi kuongeza idadi ya shule hizo na kulipa mishahara ili kupata waalimu watakao-stabilize katika shule hizo.(nimesema jamii ya kikristo inabidi ikubaliane na hili kama intervention kwa market force imefail, hivyo wasomi wa kikristo walielewe hili).
2. Ufanyike utambuzi wa uwezo wa kitaaluma kwa watoto wote ambao ni kweli wako katika mazingira magumu then serikali i-subdize waweze kusoma katika shule either za seminari, binafsi au serikali zenye viwango vinavyoendana na uelewa wao
3. Serikali ipige marufuku tamaduni za kucheza ngoma na sherehe za kipuuzi za namna hiyo.
Nitaendelea.....
Maggid,
Waislamu wengi wanaamini Nyerere alitumika kuukandamiza uislamu (refer to Mohamed Said books). Vile vile baadhi ya mambo yanayofanywa na wakristo kukandamiza waislamu mfano wanapokejeli ati wao wamepeleka mwanzo MOU wakati sio kweli waislamu walipeleka mwanzo MOU ikapigwa chini (refer to Mohamed Said books), kunapelekea kuona waislamu wanaonewa.
Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe) hivyo basi anajua fika kitu anachokifanya na kwanini anafanya.
Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'
Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!
Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!
Wengi tumezungumzia koran iliyokojolewa kwenye utani wa kitoto.
Bibilia zikachanwa na makanisa yakachomwa moto kama njia ya kulipiza kisasi.
Matukio hayo yanatuonyesha kwamba vitabu vya dini mbili viliharibiwa lakini bado damu za Watanzania zina kiu ya vita.
Tunakwenda wapi.......... bye bye Tanzania............ Vita inakupenda zaidi.
Sometimes tuwe tuna reason, hivi mie kuwa na miaka arobaini na familia ndio kuwa na akili timamu? Inawezekana mie ni mwendawazimu au nimekula ndumu, sitaki kuwabishia wale waliofanya walichokifanya, maana tumeona wamechoma nyumba za ibada na kuondoka na vifaa walivyoweza kuchukua, sitaki kuamini wameenda kuviuza ili kununua juzuu mpya. Read between the lines bro, Mungu haitaji mwanadamu ampiganie unless otherwise.Maggid,
As much as I agree na unachokizungumza pia uelewa yule Bedui alikuwa amelewa. Hivyo basi hujaelezea uhalisia wa jambo lilivyokuwa. Binafsi yangu I do not believe in violence but rather busara na hekima. Ndio maana nasema hivi suala la waislamu na wakristo ni vema likaangaliwa kwa macho mawili na uangalifu mkubwa. Niliwahi kushauri zamani kuwa iwepo TRUTH AND RECONCILIATION COMMITTEE. Watu wakanibeza but ukweli wa mambo ni kwamba waislamu wana joto lao moyoni linawauma. Waislamu wengi wanaamini Nyerere alitumika kuukandamiza uislamu (refer to Mohamed Said books). Vile vile baadhi ya mambo yanayofanywa na wakristo kukandamiza waislamu mfano wanapokejeli ati wao wamepeleka mwanzo MOU wakati sio kweli waislamu walipeleka mwanzo MOU ikapigwa chini (refer to Mohamed Said books), kunapelekea kuona waislamu wanaonewa.
Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe) hivyo basi anajua fika kitu anachokifanya na kwanini anafanya. Usimfananishe na mtoto wa miaka 7 ambaye hata kuoga hajui. Hapo Maggid unakosea. Vile vile mtume alitumia busara kuwaambia masahaba wamuachie yule bedui kwasababu alikuwa kwanza amelewa na pili hajui anafanya nini. Kisheria tunasema he is in the state of unsound mind. Hata kwenye macho ya kisheria ukiuwa katika hali hiyo unakuwa unapewa punishment pungufu kwasababu wanachukulia hukuwa unafahamu unachokifanya. Sasa huyu kijana alikuwa anajua fika analolifanya na sio kuwa alikuwa amelewa au hafahamu.
Hivyo nakushauri siku nyengine unapogusa suala la waislamu kuwa na ufahamu kidogo wa kitu unachokizungumzia. Yes hekima na busara ni muhimu katika jambo hili but GET YOUR FACTS RIGHT !!!!!
Nilikuwapo!!!!