Hayajamani
JF-Expert Member
- Jul 2, 2012
- 883
- 272
Maggid,
As much as I agree na unachokizungumza pia uelewa yule Bedui alikuwa amelewa. Hivyo basi hujaelezea uhalisia wa jambo lilivyokuwa. Binafsi yangu I do not believe in violence but rather busara na hekima. Ndio maana nasema hivi suala la waislamu na wakristo ni vema likaangaliwa kwa macho mawili na uangalifu mkubwa. Niliwahi kushauri zamani kuwa iwepo TRUTH AND RECONCILIATION COMMITTEE. Watu wakanibeza but ukweli wa mambo ni kwamba waislamu wana joto lao moyoni linawauma. Waislamu wengi wanaamini Nyerere alitumika kuukandamiza uislamu (refer to Mohamed Said books). Vile vile baadhi ya mambo yanayofanywa na wakristo kukandamiza waislamu mfano wanapokejeli ati wao wamepeleka mwanzo MOU wakati sio kweli waislamu walipeleka mwanzo MOU ikapigwa chini (refer to Mohamed Said books), kunapelekea kuona waislamu wanaonewa.
Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe) hivyo basi anajua fika kitu anachokifanya na kwanini anafanya. Usimfananishe na mtoto wa miaka 7 ambaye hata kuoga hajui. Hapo Maggid unakosea. Vile vile mtume alitumia busara kuwaambia masahaba wamuachie yule bedui kwasababu alikuwa kwanza amelewa na pili hajui anafanya nini. Kisheria tunasema he is in the state of unsound mind. Hata kwenye macho ya kisheria ukiuwa katika hali hiyo unakuwa unapewa punishment pungufu kwasababu wanachukulia hukuwa unafahamu unachokifanya. Sasa huyu kijana alikuwa anajua fika analolifanya na sio kuwa alikuwa amelewa au hafahamu.
Hivyo nakushauri siku nyengine unapogusa suala la waislamu kuwa na ufahamu kidogo wa kitu unachokizungumzia. Yes hekima na busara ni muhimu katika jambo hili but GET YOUR FACTS RIGHT !!!!!
Nilikuwapo!!!!
Nikiungana na Mjengwa kwenye hili, moja ya hadithi za mtume Muhammad SAW aliwaambia maswahaba zake kuwa Uislamu ni usafi (al islam nadhif)hapa haku maanisha kuwa unadhifu wa uislamu uko kwenye kuvaa kanzu safi, bagharashia na kikoi au nguo safi pekee! Bali usafi wa muislamu uko mpaka kwenye matendo, moyo na mazingira yanayomzunguka.
Hivi karibuni kumetokea mambo kadhaa ambayo baadhi ya vijana/watu kwenye makundi ya yaliyojumuisha waislamu wamekuwa wanafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadali na utamaduni wa kiisalamu na hivyo kuchafua jina na taswira ya uislamu.
Uislamu ni dini ya amani kama zilivyo baadhi ya dini nyingine, matendo maovu ya wachache yanaharibu taswira ya uislamu, na hii inapelekea waislamu na uislamu kuingizwa na kujumuishwa kwenye kapu moja la mambo mabaya. Kwa neno hili la leo na haya machache ninayo andika, naamini waumini wengine watavaa hekima na busara zao kuuona uislamu na waislamu kwa ujumla kuwa sio dini ya fujo na vurugu, bali ndani ya dini hiyo wapo waumini wachache wenye hulka zenye mhemko kinyume na ustaarabu na hekima za uislamu kama jinsi walivyo kwenye dini nyingine.
Tuungane pamoja kukemea ovu litakalo sababisha kutugawa kwa dini zetu na madhehebu yetu. Tukikaa kimya tutaharibikiwa wote.
Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'
Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!
Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!
Ningependa nikusahihishe kama ifuatavyo;Maggid,
As much as I agree na unachokizungumza pia uelewa yule Bedui alikuwa amelewa. Hivyo basi hujaelezea uhalisia wa jambo lilivyokuwa. Binafsi yangu I do not believe in violence but rather busara na hekima. Ndio maana nasema hivi suala la waislamu na wakristo ni vema likaangaliwa kwa macho mawili na uangalifu mkubwa. Niliwahi kushauri zamani kuwa iwepo TRUTH AND RECONCILIATION COMMITTEE. Watu wakanibeza but ukweli wa mambo ni kwamba waislamu wana joto lao moyoni linawauma. Waislamu wengi wanaamini Nyerere alitumika kuukandamiza uislamu (refer to Mohamed Said books). Vile vile baadhi ya mambo yanayofanywa na wakristo kukandamiza waislamu mfano wanapokejeli ati wao wamepeleka mwanzo MOU wakati sio kweli waislamu walipeleka mwanzo MOU ikapigwa chini (refer to Mohamed Said books), kunapelekea kuona waislamu wanaonewa.
Tukirejea suala la huyu kijana nadhani maggid you are misleading kwa sababu huyu ni kijana wa miaka 14 (inamaana ana fahamu zake na akili timamu kwasababu umri huo mara nyingi vijana wa kiume wanabelehe) hivyo basi anajua fika kitu anachokifanya na kwanini anafanya. Usimfananishe na mtoto wa miaka 7 ambaye hata kuoga hajui. Hapo Maggid unakosea. Vile vile mtume alitumia busara kuwaambia masahaba wamuachie yule bedui kwasababu alikuwa kwanza amelewa na pili hajui anafanya nini. Kisheria tunasema he is in the state of unsound mind. Hata kwenye macho ya kisheria ukiuwa katika hali hiyo unakuwa unapewa punishment pungufu kwasababu wanachukulia hukuwa unafahamu unachokifanya. Sasa huyu kijana alikuwa anajua fika analolifanya na sio kuwa alikuwa amelewa au hafahamu.
Hivyo nakushauri siku nyengine unapogusa suala la waislamu kuwa na ufahamu kidogo wa kitu unachokizungumzia. Yes hekima na busara ni muhimu katika jambo hili but GET YOUR FACTS RIGHT !!!!!
Nilikuwapo!!!!
Mdondoaji,
Nimejaribu kufuatlia hoja yako lakini nimeshindwa kuelewa una maanisha ni nini! Kwa hiyo, wewe kwa mtazamo wako, unadhani kwa kuwa kijana ana miaka 14 basi ni sawa kwa hao waumini kureact kwa kuchoma makanisa? Kweli akili ni nywele...
Ningependa nikusahihishe kama ifuatavyo;
*Kijana aliyekojolea Quran tukufu inaelezwa alikuwa ana umri wa miaka 12 kwa mujibu wa report ya polisi, vyombo vya habari na mahakama.
*Hakuna mahali popote kwenye uislam panapofundisha kuwa mtu akiidhalilisha Quran tukufu atageuka mnyama, kufa au kuwa kichaa.(Yule mtoto wa kiislam alikuwa anapotosha na kusema uongo kwa kumuhusisha Mwenyezi Mungu na jambo ambalo Mwenyezi Mungu hajalisema, kiislam huu ni sawa na ushirikina)
*Uislam haufundishi watu kufanya mizaha, kuthubutisha au kufanya majaribio kwenye Quran tukufu.
(Yule mtoto wa kiislam alipaswa kuadhibiwa kisawasawa na waislam kwani tunaamini anayajua hayo na alipaswa kuepusha yasitokee, na yule kijana wa kikristo alipaswa kufundishwa na kuonywa maana tunajua hajui nini maana ya Quran tukufu na mafundisho ya uislam kwa usahihi wake)
*Si sahihi kabisa kabisa kwa waislam kutaka kuamsha ghasia siku za leo kupitia matukio yoyote kwa kisa cha kudai waliwahi kuonewa siku za nyuma.(Kufanya hivyo hakuwezi hata sikumoja kuujenga uislam wa kweli, zaidi kutaleta uadui mkubwa na visasi)
MY TAKE
1/Wale watu wote waliofanya ghasia mbagala sio waislam sahihi, kwa kuwa uislam ni dini ya amani na masikilizano.
2/Hakuna mahali popote kwenye uislam panapotamka kuwa maadui wa waislam ni wakristo.
Kwahiyo maswahaba huwa hawana subra!
Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'
Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!
Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!
Dini zinatumika kama kisingizio tu!
vijana wanatumika kisiasa... ukosefu ya ajira tanzania nao unachangia hili ..
Hapo kwenye nyekundu ndo suala la subira linapozungumziwa. Kama walikuwa wamevumilia kitendo cha kukojolea kitabu ilishindikana vipi kuvumilia jibu la huyo mama hata kusababisha yote yaliyotokea? Cha msingi hapa ni kwamba kukitokea machafuko hakuna atakayeponywa na dini yake, tutaathirika wote kwa namna sawa. Uvumilivu ni kitu cha msingi sana.
I like the christians wanapenda amani bila kujali madhehebu yao japokuwa wana madhehebu meengi!Mshangao wa kwanza nilioupata katika maisha yangu ni pale rais wa nchi alipotangaza kuwa udini umekolea sana Tanzania. Nilishangaa maana nina jirani yangu Muislamu, wakai wa Idd huleta pilau kwenye hotpot. Wakati wa krismass napeleka. Wakati woote ni rafiki yetu. Hapa kazini, tunamchanganyiko wa waislamu na wakristu tunaishi kwa amani sana. Mwenzetu akipata shida au furaha ya mtoto Idara yote twaenda kwake.
Hivi mnafikiri nguvu na kiburi cha Ponda kinatoka kwa nani kama siyo kwa mkuu wa kaya ambaye alitumia mbinu hizo kulalalisha ushindi wake?
Na tushukuru wale waliochomewa na kuibiwa vitu vyao kwa mgongo wa waislamu hawakutaka kulipa kisasi, au walivaa busara za 'mtume' kwa bedui aliyeenda kukojoa msikitini, vinginevyo JK asingekuwa anakula pepo huko Oman.
BLUE:mkuu Mohamedi Mtoi plizzz reservve that words untill mbagalla issues,ponda issues,zanzibar issues are over and forgotten u cant even convince a very little child of 2yrs that is true about thee sayings ,but now we hope that to be but its not that way,nakiri ni taswira mbaya sana inajengeka pindi watoto wadogo wanapoona what islams do and you will agreed with me u cant change red to be white ,Nikiungana na Mjengwa kwenye hili, moja ya hadithi za mtume Muhammad SAW aliwaambia maswahaba zake kuwa Uislamu ni usafi (al islam nadhif)hapa haku maanisha kuwa unadhifu wa uislamu uko kwenye kuvaa kanzu safi, bagharashia na kikoi au nguo safi pekee! Bali usafi wa muislamu uko mpaka kwenye matendo, moyo na mazingira yanayomzunguka.
Hivi karibuni kumetokea mambo kadhaa ambayo baadhi ya vijana/watu kwenye makundi ya yaliyojumuisha waislamu wamekuwa wanafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadali na utamaduni wa kiisalamu na hivyo kuchafua jina na taswira ya uislamu.
Uislamu ni dini ya amani kama zilivyo baadhi ya dini nyingine, matendo maovu ya wachache yanaharibu taswira ya uislamu, na hii inapelekea waislamu na uislamu kuingizwa na kujumuishwa kwenye kapu moja la mambo mabaya. Kwa neno hili la leo na haya machache ninayo andika, naamini waumini wengine watavaa hekima na busara zao kuuona uislamu na waislamu kwa ujumla kuwa sio dini ya fujo na vurugu, bali ndani ya dini hiyo wapo waumini wachache wenye hulka zenye mhemko kinyume na ustaarabu na hekima za uislamu kama jinsi walivyo kwenye dini nyingine.
Tuungane pamoja kukemea ovu litakalo sababisha kutugawa kwa dini zetu na madhehebu yetu. Tukikaa kimya tutaharibikiwa wote.
Ndugu zangu,
Moja ya hadithi za Mtume Muhammad S.A. W ni pale Mtume Muhammad alipokuwa msikitini na maswahaba wake. Mara akaingia msikitini mtu wa kabila la Mabedui na kuanza kukojoa. Maswahaba wa Mtume wakasimama kwa hamaki kutaka kumwadhibu Bedui yule.
Mtume akawasihi maswahaba wake wasifanye jambo lolote litakalomdhuru Bedui yule. Hapo ikavutwa subira. Bedui yule akakojoa na akamaliza. Mtume Muhammad alipomuhoji Bedui yule ikabainika kuwa alikuwa ni mtu wa hovyo na wala hakujua kuwa alimokuwa ni msikitini. Bedui yule akaelimishwa, akaelewa. Akarudi kwenye ustaarabu.
Ndio mkojo ule ulifutwa kwa maji na amani ikawepo. Wahenga walinena; Subira yavuta heri. Siku zote, hamaki si jambo jema. Kwa kutanguliza subira na kutumia hekima Mtume Muhammad aliivuta heri na kuepusha shari.
Maana, kama Mtume alisingewaasa maswahaba wake kuvuta subira, basi, makubwa matatu yangetokea ndani ya msikiti ule; Mosi, zingezuka vurugu na watu kuumizana na hata kutoana roho. Pili, mkojo wa Bedui yule ungesambaa msikitini kwa vile alishaanza kukojoa na isingekuwa rahisi kwake kukatisha mkojo wake. Tatu, Mkojo una madhara ya kiafya pia.
Naam, kwa mwanadamu, ni muhimu kuwa na subra na kutafakari kabla ya kufanya maamuzi. Kwa ndugu zangu Waislamu, tunaona Mtume Muhammad ameweza kuonyesha hilo. Na kwa ndugu zangu Wakristo, kuna mifano pia ya Yesu Kristo kuonyesha subra.
Ndio, Uislamu, kama ilivyo kwa Ukristo na dini nyingi za humu duniani, msingi wake ni amani na upendo. Kitendo cha mtoto yule wa Mbagala kukojolea korani kitazamwe kwa sura ya kitendo kilichofanywa na mtoto .
Na kama ilivyokuwa kwa Bedui yule, kama pale Mbagala subira na hekima vingetangulizwa, basi, yumkini tungebaini kuwa mtoto yule hakujua madhara ya kitendo chake. Naye angekanywa kama tuwakanyavyo watoto wetu. Na hata kitendo hicho kingefanywa na mtu mzima, bado tulikuwa na haja ya kutanguliza subira na hekima kumhoji aliyetenda, yaweza akawa kama Bedui yule kwenye msikiti alimosali Mtume na maswahaba wake.
Na kwa kuangalia picha zile za Mbagala naiona hatari iliyopo sasa, kuwa tuna vijana wengi wasio na kazi; Wakristo kwa Waislamu. Vijana wasio na dogo. Ni kama moto uliofifia. Akipatikana kwa kuchochea kuni wanalipuka.
Ni vijana wanaopatikana wakati wowote na mahali popote. Hata jambo likianza saa tatu asubuhi wao wapo. Hawana ofisi wala bosi wa kumwomba ruhusa ya kwenda kuandamana na kurusha mawe. Ndio hawa wanaonekana wamevaa ' Kata kiuno' na wengi wao hawajahi hata kuingia misikitini au makanisani.
Inakuawaje kijana wa kweli wa Kiislamu achome kanisa na kuiba kompyuta. Inakuawaje kijana na muumini wa kweli wa Kiislamu aonekane saa mchana wa jua kali akivamia baa na kukimbia na kreti za bia? Ni maswali yanayotutaka tutafakari kwa makini.
Maana, ninavyoamini mimi, uchumi na elimu duni ndio hasa vinavyochochea vurugu za kijamii, iwe za kidini au kisiasa, na hususan inapohusisha vijana. Vijana wetu hawana misingi mizuri ya elimu, na wengi hawana ajira pia. Haya ni sawa na makombora yasiyo na gharama kubwa kuweza kutumiwa na wanasiasa wasio waadilifu na hata viongozi wa kidini wenye mitazamo mikali. Ni makombora yaliyoanza kutulipukia. Tuliziona ishara, tukazipuuzia.
Leo Kuna vijana watakaotumiwa au kutumia fursa hiyo kutenda maovu kwa kisingizio cha dini. Ni hawa wataoshiriki kuchafua taswira za dini husika pia. Tujiadhari, kabla ya hatari kubwa inayotujia. Hatujachelewa.
Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765