GoLC
Senior Member
- Jul 10, 2025
- 135
- 212
Kuna matukio nikikumbuka huwa najisikia vibaya, fedheha, pengine na kujicheka ndani yake. Kwamba ndio kujifunza huko. Wakati fulani nafanya kazi za video shooting nilishoot dicumentary ya dada fulani (RIP) kwa ajili ya sendoff yake.
Dada alikuwa anaishi na jamaa yake na wana mtoto mmoja. Nilienda hone kwake kufanya hiyo shooting. Sasa nilicbukua maelezo na historia yake wee na jinsi jamaa yake alivyomsapoti kimaisha hadi kufikia levo fulani. Nilizama sana upande wa jamaa. Nikamalizia na shukrani kwa wazazi waliomlea. Nikaenda studio kuandaa documentary.Siku ya sendoff wakati wa maakuli nikaiweka ikawa inaplay kama kawaida. Kumbe waliomlea wanaifuatilia kwa umakini kweli. Nikiwa nimejipumzisha zangu akanijia ghafla mjomba wake ambaye ni mlezi wake.
Amefura! Akanieleza kwa ukali ni kitu gani hii inainyeshwa hapa. Zima haraka! Nikawa natoa tu macho na fasta nikazima kwanza ili kusikiliza shida nini. Mjomba mwenyewe tunafahamiana kupitia Bro, na ndiye aliyenipa hela ya shooting. Akawa amekasirika pale kwa nini nilishoot vile na kuegemea upande wa mwanaume...Kiukweli sikuwa nimewaza hayo. Niliwadhalilisha wazazi/walezi. Tukio hilo kiukweli lilionekana kuwaondolea furaha. Ni kwa vile walikuwa tu wananufahamu la sivyo wangeleta shida zaidi. MBAYA zaidi wakati naingia ukumbini nilikuwa nimezima mic kwa ajili ya kuchukua tu matukio ya video nije kuweka soundtrack.
Hadi wageni wanaingia na maharusi, bado mic ipo off, nami narekodi tu. Nilipokuja kushituka ni wakati wa kufungua kwa sala ndipo natazama sioni mic. Ipo kwenye begi. Nilipagawa. Haraka sana nilienda kwenye begi nikaichukua na kukimbia na kuichomeka. Nilikosa audio zote za mwanzo.Sherehe inaisha nawaomba waliochukua video sikupata hata mmoja! Hatari. Nilichofanya baada ya kurudi studio nilisikikiza sauti ya MC nikajaribu kuiiga nikachanganya na soundtrack hadi sala ilipoanza. Nashukuru hawakushitukia hilo. Shida ningechelewa kugundua sijui ningekimbilia wapi. Kuna kazi zingine changamoto sana