Miungu ya kale inaporejea kwa kificho

Miungu ya kale inaporejea kwa kificho

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,669
Reaction score
27,559
Tekinolojia na miungu ya kale.

Kuna movie moja niliona, inaongelea project ya mwaka 2050. Kwamba miaka hiyo kutakuwa na magari ya kupaa na maraboti yanayojiongoza(artificial intelligence). Na hiyo movie inamwongelea mungu wa Misri anayeitwa Horus, ambaye kila baada ya miaka 2000 anakuja duniani na kumuingia mwanaume aliyemwandaa, Kisha anamtumia kulala na mwanamke aliyemchagua. Tendo hilo lina chochea umilele wake. Ndani ya video hiyo walionesha magorofa marefu sana na technologia ya hali ya juu. Kuna mambo matatu hapa tunayapata.

1) Technology inakuwa sana kwa Kasi ya hali ya juu, na inakuwa kwa kiwango cha kustajabisha. Kuna faida kubwa katika ukuaji wa tekinolojia na Kuna hasara pia vile vile. Hebu tuongee kuhusu hayo magari ya kupaa, jana Japan wamezindua moja ya magari hayo kama mfano wa baadae, na si kwamba ni Japan pekee ndio wanayo, yapo, lakini hayatatumika ama kuuzwa sasa mpaka wakati watakaouamua wao yaani baada ya kuyawekea mifumo yake. Maana yatakuwa yana stand za juu pia, maana yamekusudiwa kupandisha watu kwenye magorofa marefu sana. Hivyo hizi movie za sayansi fiction ni mipango ya baadae, ni Kama jiwe la msingi tu.

2) Robot Kama tulivyokuwa tunaona katika movie miaka ya 80, 90 mpaka leo, tayari wapo kwa uhalisi. Anold Showzniger ametumika kuact movie za robots (Terminator-skynet) akionesha jinsi huko mbele robots watakuwa na uwezo wa juu sana. Hivyo watatumika vitani kama wanajeshi (machine soldiers) kuangamiza maadui ambao kimsingi ni wanadamu katika vita.

Miaka 15 iliyopita enzi za rais George W. Bush alisema tutaanza program ya kutengeneza wanajeshi wa mashine(machine solders) ili kupunguza vifo vya wanajeshi wetu, pia alisema ifikapo 2020 watakuwa tayari wamesha peleka vyombo Mars kwa uchunguzi wa uhai wa sayari hiyo ambayo wanataka baada ya mda fulani waitawale Kama wakoloni wa Sayari kwa Sayari.

Na sasa tunaona bidii kubwa ya vyombo kurushwa kuelekea Mars, Kumbuka miaka ya 80 Anold Showzniger alicheza movie ya maisha ndani ya sayari ya Mars, huko walijenga majengo ya vyuma na ndani wakaweka oxygen na maisha yakaendelea na baadae walifanikiwa kutokeza uhai katika sayari hiyo nyekundu. (Wenzetu wanamipango ya miaka na miaka hawakurupuki). Je wataweza kuishi Mars? Swali hili tutalijibu wakati mwingine.

Kuhusu marobot, Kama una kumbukumbuka juu ya project ya robot Sofia utanielewa vizuri hapa, kwanza project hii ilitengenezewa movie iliyochezwa na Will Smith, kulikuwa na marobot wengi wastarabu lakini mmoja akawa na uwezo wa ajabu, na baadae akaasi na kuanza kupigana na wanadamu. Kama Kuna mtu alikuwa anafuatilia mahojiano ya robot Sophia utaona Kuna wakati alihojiana na Will Smith, na Kuna mda Sophia alihojiwa na kusema kwamba wametengenezwa Kama marafiki wa wanadamu lakini program ya pili wataua wanadamu. Kuna aina mbili ya marobot, nitaeleza hili wakati mwingine. Lakini moja ya lengo la technology ya maroboti ni kupandikiza utisho, maana ambaye atamiliki technology ndiye atakaye tawala dunia.

3) Miungu ya kale inafufuliwa tena, swali ambalo najua utaweza kuuliza, je miungu hiyo itafufuliwaje? Ni kwa njia ya vitabu, makala, na movie ili iweze kukaa katika fahamu (mindset) za watu. Kwa Afrika Kuna kundi ambalo linatumika kuiamsha miungu hii ya kale kupitia makala, vitabu, video kwa jina la kurudia ukale wa Afrika (mababu) au kwa jina la ukiroho wa Afrika.

Huko Ugiriki pia wameanza kuirudia miungu ya kale kitambo tu, baadhi wameanza kumuabudu Zeus(Mungu Jua wa kigiriki), pamoja na miungu yote ya ugiriki. Pia tambua Zeus anaabudiwa kidunia kupitia mchezo wa Olimpic, Olimpic chanzo chake ni Zeus na ilifanyika kwa kila baada ya miaka 4 katika hakelu la Zeus, walimtukuza na kufanya michezo mbele zake. (Taz Swaddling 2000, p. 54). Video za Zeus zimetengenezwa huko Hollywood kwa lengo la uamsho huu. Hakuna jambo la bure, kila movie ina lengo.

Hivyo hii harakati ya video za miungu si harakati ndogo, kuna ibada inaitwa Baal Peor, inaadhimishwa sasa, nilifanikiwa kuona video ya waumini wa Baal Peor, Kumbuka ibada hii ndio iliwaangusha wana wa Israeli kwa ushawishi wa nabii Balamu na mfalme Balaki wa Moabu wakati Waisrael wanatoka Misri kwenda Kanaan. Ibada ya Baal Peor ni ibada ya kuabudu wafu-mizimu ya mababu na inaambatana na uzinzi, na inasimamiwa na wanawake waliovaa kiashiiki. (Taz Hesabu 25:1-5, Zab 106:28; Uf 2:14).

Moja ya movies za miungu zilizotengenezwa ni wrath of the Titan, Clash of the Titan, Hercules, God's of Egypt na zinginezo. Titan kwa English ni Satan, kiarabu ni Shaitwani, na Hercules ni mwana wa Zeus(mungu jua), ni masihi ambaye anapigania wanadamu, hana tofauti na Horus wa Misri ambaye pia baba yake ni Osiris (mungu jua wa Misri).

Hizo movie watoto wetu na vijana wetu wanazitazama pasipo kujua siri ya ndani, na huko ni kuandaliwa kuipokea miungu hii ya kale iliyotoweka kwa kushindwa na Ukristo, ingawa leo imejificha katika ibada za wakristo fulani hivi kwa kubatizwa kwa majina ya watakatifu. Sasa miungu hii imejitokeza wazi wazi na inaishi katika fahamu za wengi kupitia msukumo wa movie, makala, vitabu, pamoja na watu ambao wamejitokeza kuiabudu waziwazi kwa kivuli cha kurudia ukale wa mababu.

Hivyo tupo katika vita vya mawazo (mind battle) ambayo ndio vita vya kiroho. Hivyo Mambo yote yanayoendelea duniani Kama Vita, movie, siasa, technology, uchumi nk, kwanza yanafanyika ndani ya fikra, na yote yanahitaji nafsi ya mwadamu. Mtume anasema,

"Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome😉 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
2 KOR. 10:3‭-‬5 SUV"

Linda fikra zako kwa silaha za Mungu ili usiwe mateka. Kwa taratibu tutaendelea kujifunza mambo haya.

FB_IMG_1745856653959.jpg
FB_IMG_1745856651444.jpg
FB_IMG_1745856648706.jpg
FB_IMG_1745856655993.jpg
 
Nazikubali sana hizi movies kuna moja inaitwa immortal du kuna Zeus mule anakichafua, appolo anashuka kumsaidia binadamu choosen one anapiga bahari kwa fimbo mpaka oil inatoka hatari sana.....
 
Flying cars zikianza kutumika.matukio ya ugaidi yqtaongezeka maradufu.
 
Sasa hiyo Miungu ikiabudiwa ninyi wengine mnaumia nini? Binadamu anao uhuru wa kuabudu atakacho, lkn maajabu kuna hizi dini mbili za kihuni(ukristo&uislamu) zimejizolea uhalali wa kujiona ndio dini pekee za kufuatwa, wakati huo ukristo+uislam ni dini za juzi tu, kabla yake, maelfu ya miaka kulikuwako imani za kale zaidi ya hizo dini mbili, pia zipo imani ambazo zilishafutika sababu ya kupoteza ushawishi ktk jamii baada ya watu kuhoji uhalali wake.

Watu wa dini mtambue kuwa ukristo na uislamu sio iman wala dini za kipekee kuna maelfu ya dini/imani zilizojizolea umaarufu na idadi ya waumini kwa maelfu ya miaka kabla hata hizo dini zenu hazijaundwa.

Msingi wa ukristo umeundaa kutoka ktk hizo hizo imani za miungu ya ugiriki ambao nao waliunda iman zao kwa kucopy imani za misri nao misri walicopy imani kutoka ktk tamaduni za waafrika wa kale zaidi, ukristo baadae ndio umeunda huo uislamu wa juzi ambao waumini wanadanganyana misikitin kuwa ni dini ya zamani tangu adamu, adamu mwenyewe hajawai kuwepo kaundwa undwa kutoka kwa hadithi za warumi.

Kama ilivyo imani za kale zilivyokufa na kupotea hata ukristo+uislamu utakufa na kupotea zitaibuka imani mpya ambazo zitaendana na matakwa ya vizazi vijavyo, ndiomaana mnaziona hizi dalili siku hizi watu kuamka na kuachana na dini, wengine wanazitusi adharani hawana uoga tena kama waliokuwa nao mababu zetu waliopewa hizi dini.

Narudia tena, hizi dini zenu miaka michache ijayo zitakufa na kusahaulika kama dini zingine za kale zilivyokufa na kusahaulika, wataibuka ma Heroes wengine ambao watakuwa kama watetezi wa jamii dunian, heroes ambao wataziba nyufa za stories za akina yesu na hao miungu wenu Allah sijui yehova,

hilo halina ubishi ,mkubali au mkatae lkn miaka michache ijayo itakuwaka kawaida mtu kumuabudu Superman/Spiderman kama mtetezi na mkombozi wake kuliko kuabudu hizo imagination za kale za akina yesu na akina Allah, ndiomaana juhudi kubwa ktk tasnia ya filamu za wazungu inafanyika ili kuendana na matakwa ya kizazi kipya.
 
Shida jamaa yangu masomo yako hayanaga mwendelezo

Lakini Asante sana kwa somo zuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom